Kwa ugumu wa maisha nilionao, michango inayoendelea inanifikirisha sana

Tabia ya pesa inapenda uthamani(value) ndio maana watu smart wanakwambia jiengezee Value ndio pesa itakifata...ni rahisi kwa Maxence Mello kupata uCEO wa AirtelTZ kuliko wewe usie na value, Rahisi MilladAyo kupata mchango wamatibabu akiumwa kuliko wewe, Rahisi Diamond kupata Deals za MaBillion kuliko muuza nazi mtaani.

Value ya Mbowe huwezi ifananisha na yako na value hiyo Mbowe hakuitenheneza Overnight inaelekea kipindi ambacho ndio wazo la ku-engage kwenye politics watu walimuona hana kazi yakufanya ila leo anauwezo wakichangiwa mpaka 500M kwa value aliyoitengeneza.

So usipende Shortcut tafuta vibarua, kazi za Ali ya chini, jiajiri locally ukishapata pesa utaiyengeneza Value yako zaidi.

Portfolio | 2020
Nimekuelewa vyema sana ,wala sijapenda shortcut kuna muda tu mtu unawaza mpaka unafikia mwisho wa kuwaza/kufikiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamechanga watu wengi sana, kw kuchangia kitu kinachowaunganisha pamoja kisiasa na kijamii.

Hivyo, hata wakichanga kidogo kidogo kila mmoja, hela zinapatikana nyingi.

Na kwa kweli, kitu walichochangia ni cha msingi, kwa sababu hatuwezi kumaliza matatizo ya kiuchumi yanayokufanya ulalamike, kama hatujamaliza matatizo ya msingi ya kisiasa.

Nchi inayoendeshwa kiimla bila kufuata katiba, kwa kutishia tishia watu, ni vigumu kupata maendeleo ya kiuchumi.

Kuhusu suala lako, tunasaidiana kadiri tunavyoweza, ila, nchi yenye matatizo mengi ya kiuchumi, wanaoomba msaada nao ni wengi mpaka inakuwa si rahisi hata mtu mwenye nia njema kusaidia wote.

Hapo tunahitaji wananchi wapiganie fursa sawa kwa wote, mikopo ya riba nafuu kwa wajasiliamali kuanzisha biashara ndogondogo etc.

Watu wangapi wanashinikiza wabunge wao kwenye haya?
 
Hakuna mtu timamu wa kuchangia kwa sababu una akili kama jiwe/bashite
Hellow poleni na majukumu
Ni jioni tulivu namshukuru Mungu ninaafya tele

Tumeona hukumu ya viongozi wa chadema
Mamilioni ya mapesa
Basi ile sijakaa sawa nikaona kwenye mitandao hamasa ya michango
Namba zikatolewa za kutosha
Basi giza tororo likazidi na joto likanizidia mana hata hela ya umeme sina nikapitiwa na usingizi nikala
Asubuhi baada ya shuhuli hapa na pale naona michango imetimizwa ya mamilio ya mapesa
Kigogo kaposti na risiti tena ya kawaida si ile ya EFD tulohamasishwa tuzitumie.

Imenifikirisha mno juu ya hali ngumu niliyonayo ambayo nakosa hela kidogo ya mtaji ili niweze kujiingizia kipato
Maajabu ni kwamba kwa maelezo hela imechangishwa na wananchi

Wapendwa wanaJamii Forum wenzangu hebu naombeni tu mnipe kazi ya kufanya na mimi nipate kipato ama wa kunikopesha mtaji na mimi niweze kuanza biashara ,si mchango wa haya mamilioni hapana ni mataji tu wa laki 5 kwani nina watu nyuma wananitegemea mnoo

Natanguliza shukrani zangu za dhati ,,ila kiukweli bado nafikiria yale mamilioni yaliyochangishwa kwa haraka vile sijui wenzangu wanapataje hela na mimi nakwama wapi!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini kumbuka tu, hakuna mwanasiasa nchi hii anaweza kubadilisha hali yako, pambana tu mkuu. Hizi za tusirudie makosa ni propaganda tu ili tubadilishe walaji wa mkate wetu wa taifa, kiuhalisia wewe na mimi ndio tupambane na hali zetu.
Mkuu kudhani kuwa siasa haikuhusu ni utoto. Kaa utafakari vizuri utagundua kwa hali yoyote uliyo nayo huwezi ikwepa siasa,wanasiasa ndio wanaamua mambo yaende vipi.

Hata uwe na uwezo kiasi gani huwezi jenga shule ili wanao wasome, huwezi jenga barabara ili usafiri, huwezi jenga hospitali ili utibiwe, huwezi tunga sheria zako, huwezi kuwa na jeshi, huwezi kuwa na mfumo wako wa uwekezaji, huwezi jitungia sera zako na mengine mengi huwezi kujifanyia.

Unahitaji entities za kushughulika na hayo mambo,ndipo issue ya serikali na organ zake na siasa zinapata mashiko.

Kuna wengi walikuwa wanajifanya hawajishughulishi na siasa kwamba wana vishughuli vyao eti watapoteza muda,leo hii vimekufa kwa siasa za awamu hii ndio wanastuka kuwa kumbe siasa ni sehemu muhimu ya maisha wakati ni too late.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si umesikia Mama mmoja huko Kakonko ameenda kuuza kuku na mayai ili achangie, jitume ili na wewe uwe miongoni wa kuchangia sio kulalamika na wewe uchangiwe. Hyo simu uza nunua mahindi mabichi tafuta jiko la mkaa anza kuuza, simu uza nunua mzani anza kupima watu uzito, sasa hivi kuna hatari ya Corona nenda maduka yanayouza madawa nunua mask na gloves wauzie watu waambie zinaadimika muda so mrefu watanunua, nenda kibaha nunua maziwa dumu uanze kuuza rejareja, maisha ni kupambana kijana, usitegemee kuna mtu atakusaidia kuimprove maisha yako
 
Apart from ths kama anaweza ajifunze ufundi cherehani....! Kuna wanawake wanamake hela ndefu kupitia hii kazi ..! Unajikuta umeajiri na watu kabisa! Km hataka biashara za uchuuzi
 
Inamaana pik piki yako ndio aniandalia uzi kabisa?? Duh
Ama kwa kuwa ni ya mkataba ndio mana akataka kujua je? Itaweza kurejesha deni la mkataba na ikabaki na hali nzuri ya yeye kumuingizia kipato?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama ni ya mkataba ...!! Ila kengele imeshaanza kugonga kichwan wengi wanalizwa sana unaweza kujidai mwema umsaidie ukapigwa ,

sent from toyota Allex
 
Mimi ni Ke ,, asante sana inamaana wapo wengi nyuma wanaopitia hali kama yangu siyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo wengi tu sister,ni kupambana tu,hakuna mbadala!
Kipindi bado ni mwanafunzi wa chuo,nilikuwa naishi na Anko wangu aliye kuwa ameishia Std 7,(tulikuwa tunakutana kwa kaka mkubwa chuo kikifungwa),
Anko wangu,alikuwa ananiona kama vile Mimi kusoma chuo,nimeyapatia sana maisha,akawa ananiuliza,na yeye afanyeje atoke kimaisha,kwanza alianza kuuza mitumba,baadae akaona hailipi,akaniomba nimsaidie kuandika mchanganuo wa mradi,ili autumie kuomba mtaji kwa ndugu yeyote.
Miaka ya 2000,kulikuwa na biashara sana ya vibanda vya simu,tukaandika mchanganuo,tukapitisha bakuri,ndugu na jamaa wakachangia,wengine walikuwa kwenye haya makampuni ya simu,enzi hizo buzz Gsm(tigo),wakampa vifaa,akafungua vibanda kibao vya kupiga simu,
Baada ya miaka miwili,jamaa alikuwa ana cash ya kutosha mpaka akaagiza container zima la computer ili afungue internet cafe,
Uwezi amini,by the time namaliza chuo,pocket money ya kuzungusha bahasha mjini,nilikuwa naomba kwake,
Jipange tu mdada,kutoka inawezekana,
Too bad,Anko wangu alifariki 2005,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apart from ths kama anaweza ajifunze ufundi cherehani....! Kuna wanawake wanamake hela ndefu kupitia hii kazi ..! Unajikuta umeajiri na watu kabisa! Km hataka biashara za uchuuzi

Akianza uchuuzi anaweza akaboost kipato kidogo ikafanya mambo mengine makubwa, alafu kujifunza fani kunahitaji muda kidogo ili uweze kuwa mzoefu na kupata connection but uchuuzi hautaji mtaji mkubwa na uzoefu unajifunzia humo humo
 
Si umesikia Mama mmoja huko Kakonko ameenda kuuza kuku na mayai ili achangie, jitume ili na wewe uwe miongoni wa kuchangia sio kulalamika na wewe uchangiwe. Hyo simu uza nunua mahindi mabichi tafuta jiko la mkaa anza kuuza, simu uza nunua mzani anza kupima watu uzito, sasa hivi kuna hatari ya Corona nenda maduka yanayouza madawa nunua mask na gloves wauzie watu waambie zinaadimika muda so mrefu watanunua, nenda kibaha nunua maziwa dumu uanze kuuza rejareja, maisha ni kupambana kijana, usitegemee kuna mtu atakusaidia kuimprove maisha yako
Asante sana ,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom