Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,238
Huu ujinga unaotendwa na watendaji wa vijiji na kata nchi nzima wa kuhakikisha fomu za wagombea wa upinzani hazipokelewi kwa udi na uvumba, haujawahi kuwepo kwa kiwango kama hiki tangu nipate akili, sijawahi kuona serikali ya ccm isiyojiamini kama hii tangu nchi hii iachwe na wakoloni, ni aibu kubwa sana.
CCM imeishiwa pumzi kabisa ! bila watendaji hakuna kitu.
Natoa wito kwa Waziri Jaffo kujiuzulu mara moja kwa vile ameshindwa kusimamia mchakato wa haki wa uchaguzi wa serikali za mitaa, fomu za wagombea zinachanwa, zinakataliwa, wengine wanakimbiwa na watendaji hadi kufikia baadhi ya watendaji kuvunjika miguu baada ya kuanguka kwenye korongo, huku Waziri akinyamaza tu.
Aibu iliyoletwa awamu hii haijawahi kuletwa kwenye nchi hii tangu mfumo wa vyama vingi uanze.