Kwa ubunifu huu wa CHADEMA, CCM itasambaratishwa kirahisi sana!

jebibay

JF-Expert Member
Nov 3, 2012
1,431
640
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikishangazwa na vyama vya siasa kutokutumia ipasavyo fursa za mawasiliano zilizopo kutokana na maendelea ya ki-tekinolojia !. Sote tumekuwa tukipokea matangazo mbali mbali yakija kwa njia ya SMS kwenye simu zetu za mikononi na nimeshindwa kuelewa kwa nini vyama vya siasa havitumii utaratibu huu...

Kwa mfano, kama ambavyo mtu unaweza kupokea msg ambayo source yake ni CRDB, M-PESA etc, imagine uwezekano wa watu kupata msg ambayo inaonyesha kwamba inatoka CHADEMA na ambayo inahimiza watu wakajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura na mambo mengine kama hayo !. Ni njia ambayo itawawezesha chama kuwafikia mamilioni ya watu in a matter of minutes na kufikisha ujumbe unaokusudiwa !. Pamoja na kuwaza huku, bado nilikuwa na wasiwasi kama CCM itakubali kirahisi wapinzani wawe na uwezo wa kuwafikia wananchi kwa njia hii na kwa urahisi hivi.....most likely wangeweza kuwatumia TCRA, kujaribu kuibua sababu mbali mbali za kuzuia kitu kama hiki......

Mimi naamini kwamba ubunifu wa Chadema kwa kuanzisha program zao tatu, utawezesha hiki nilichokiongelea hapo juu, kufanyika kwa ufanisi mkubwa !

Program hizo tatu ni :

E-membership --- kama inavyojieleza kwa jina lake itawawezesha wale wanaotaka kuwa member wa chama kuweza kufanya hivyo kwa njia ya mtandao....

E-media ---- itawawezesha wanachama na wananchi kwa ujumla kuweza kupata taarifa mbali mbali za chama baada ya kujiunga na hiyo huduma

E-movement ---- baadhi yetu tayari tumeitumia hii huduma siku ya uzinduzi. Kwa kutumia njia hii watu mbali mbali wanaweza kuchangia harakati za chama kirahisi tu kwa njia ya mtandao.

Nitatoa maeleozo ya ziada kidogo kwa huduma mbili (e-movement na e-media) :

E-MOVEMENT
Kilichoanzishwa na CDM kupitia hii huduma ni kitu kikubwa sana !. Sio tu kwamba tarehe 31 October 2014, kulifanyika fundraising kwa kupita hii huduma, bali kikubwa zaidi kulianzishwa utaratibu wa kuchangisha fedha endelevu ambao watu wanaweza kuhamisishwa kuchangia kwenye kila mkutano wa hadhara na hata mitaani kwenye interactions za kila siku !. Imagine katika kila mkutano wa CDM watu wawe wanahimizwa kuchangia (wale wanaoweza) angalau alfu moja kwa njia ya mtandao hapo hapo mkutanoni !. Wengine watachangia hata zaidi ya hiyo 1000 na wanaweza hata kuendelea kuchangia baada ya mkutano. Kwa mfano mimi nilichangia hela nzuri tu kwenye uzinduzi na nitaendelea kuchangia kiwango kama hicho kila mwezi. Vile vile nikiwa katika maongezi ya kikazi na mtu mmoja, nikatumia muda huo kumshawishi na yeye achangie na akakubali kuchangia hela kubwa tu ! Ninaamini uhamasishaji ukiwa mzuri, tutakuwa na hela za kutosha sana kupitia utaratibu huu ambazo zitatusaidia katika harakati zetu kama CDM kwa kushirikiana na UKAWA kuitoa CCM madarakani....

E-MEDIA
Kwa mawazo yangu hii program ndio funga kazi !.

Kama watu wataweza kusubscribe bure kwenye hii huduma na kuweza kupata bure, taarifa za CDM na hata UKAWA kupitia SMS, then ninaamini tutapata mafanikio makubwa sana !. Kazi ambayo inabidi ifanywe kwa nguvu mara baada ya huduma hii kuwa hewani, ni kuwashawishi watu wote wanaohudhuria mikutano mbali mbali ya chama kusubscribe/kujiunga na huduma hii. Ikiwezekana katika kila mkutano au mkusanyiko wa kisiasa, dakika kama tano zinaweza kutumika kwa wale wote ambao hawajajiunga waweze kujiunga hapo hapo kama watapenda kufanya hivyo.

Watu vile vile wawe encouraged kuwashiwishi ndugu, jamaa na marafiki zao wajiunge na huduma hiyo !. Tukifanya hivi katika miezi michache ijayo tunaweza tukawa na mamilioni ya watu ambao wamejiunga na huduma hii !. Imagine kabla ya uchaguzi mkuu, tuwe na watu wanaofikia million kumi waliojiunga !.....Uzuri wa hii huduma ni kwamba watu wanajiunga wenyewe na wengi wa hao watakuwa na interest na hivyo kwa kujua idadi yao tayari tutakuwa na indication ya watu ambao most likely watatusupport katika uchaguzi.

Faida ya hii huduma, mimi ninavyoiona, si kwa taarifa mbali mbali kutoka kwenye uongozi, bali zaidi faida ninaiona katika kutoa maelekezo au instructions kwa wale waliojiunga !. Itakuwa rahisi kwa mfano, kuhamasisha watu kuchangia shughuli za chama kupitia huduma ya e-movement !

Hebu fikiria hizi possibilities..........

  • Imagine siku mbili au tatu kabla ya muda wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu kwisha, ujumbe wa SMS unaingia kwenye simu za watu wapatao million kumi ukihimiza watu kwenda kujiandikisha na wakati huo huo ukihimiza watu hao wote wausambaze ujumbe huo kwa ndugu jamaa na marafiki zao !.

  • Imagine siku moja kabla ya uchaguzi, ujumbe wa SMS unaingia kwenye simu za watu wapatao million kumi ukikumbusha kupiga kura siku inayofuata bila kujali hali ya hewa ya siku hiyo kwani kila kura ina thamani na kuwahimiza vile vile wawahimize ndugu, jamaa na marafiki kuhakikisha nao wanapiga kura !

  • Imagine wakati fulani katikati ya campaign kukatokea uhitaji wa hela kwa ajili ya kuwasaidia wagombea mbali mbali wa UKAWA na hapo kukatumwa ujumbe kwa watu wote waliojiunga ukiwahimiza kwamba siku hiyo hiyo kwa wale wanaoweza wachange angalau 500 kila mtu ili kufanikisha harakati za campaign !. In just one day unaweza ukapata billions !

Kwa ubunifu huu, kinachotakiwa ni kuhakikisha tu kwamba watu wengi sana wanajiunga na huduma hii na baada ya hapo, the possibilities are endless !. Ninaamini IKAWA unaungwa mkono na mamilioni ya watanzania na uwezekano wa kupata watanzania wanaofikia million kumi kuweza kujiunga na huduma hii ni jambo ambalo linawezekana kabisa.

Tukiwa na idadi kama hii itarahisisha sana kuiondoa CCM madarakani kwani :

  • Hawa ndio watakaoshawishiwa waipigie kura UKAWA hasa kwa jumbe zilizosukwa kitaalamu kwa kuvishirikisha vyama vingine vya UKAWA na kufikia wote waliojiunga kwa njia ya SMS,

  • Hawa watasaidia kusambaza jumbe hizo kwa ndugu, jamaa na marafiki wao, wajiandikishe na kuipigia kura UKAWA

  • Na hawa hawa ndio ambao hata kama wakitakiwa kuchangia miatano kila mmoja (pale inapobidi) , kwa wingi wao watawezesha kupatikana kwa billions of money in a matter of days

The possibilities are endless !
 
Dunia inahamia kwenye 'digital era', na kwa baadhi ya nchi tayari kuna mambo yafanyikayo kimtandao...

Fursa hii bila shaka CDM wameiona na wameitumia...
 
Mtahangaika kila njia, wachagga kuongoza nchi hii mtapasikia kwenye redio tu.
 
bila kumun'gunya maneno;cdm ni chama pekee Afrika Mashariki,inayoongozwa kwa akili,na kisasa.

HAUTAKII UNACHA
 
kwa kuwa wewe ni mvivu wa kuvikiri na kufuatilia mambo unaona kuwa cdm wamebuni kitu kipya.Ukweli kwamba wachofanya cdm ,kilifanyika na ccm,pale mlimani city mwaka 2010
 
Kwa matumizi ya teknolojia, kiukweli cdm wanastahili pongezi. Ila kikwazo kikubwa ni kwamba baadhi ya simu huwezi ukapata herufi 'm' kwenye kuandika namba ya siri kwenye m-pesa, ili kupata neno M4c. Sijui kama watu wa cdm wameliona hili.
 
Sasa nyie mnahamasisha njia za kuchanga pesa tu lakini hamtaki kuleta marejesho kwa wachangaji mnadhani mtafanikiwa, angalia juzi mwitikio wa harambee yenu Tanzania nzima kupitia ITV watu walivyowatosa.
 
Mtahangaika kila njia, wachagga kuongoza nchi hii mtapasikia kwenye redio tu.

Wachaga zamani tuliaminishwa ni wezi na ukimpa nchi itauzwa. Nakuuliza wewe ajuza. Mbona wakwere wezi, unasemjaje? Mbona CCM ina wezi mpaka kupitiliza, wao ni wachaga? Embu siku moja moja post mambo yenye mashiko bibi kizee.
 
kwani operesheni Sangara, Operesheni Okoa Kusini na M4C zimeishia wapi? Maneno ya kuisambaratisha ccm yalianza kitambo lakini hata moja linalofanikiwa
 
usishabikie SMS sana, mtapata spam messages hadi ukasirike. Kenya walitumia majina na nambari za watu kutoka kwa madaftari ya mpesa agents kiholela, kisha wanaanza kukutumia message za campaign, inaudhi sana.
 
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikishangazwa na vyama vya siasa kutokutumia ipasavyo fursa za mawasiliano zilizopo kutokana na maendelea ya ki-tekinolojia !. Sote tumekuwa tukipokea matangazo mbali mbali yakija kwa njia ya SMS kwenye simu zetu za mikononi na nimeshindwa kuelewa kwa nini vyama vya siasa havitumii utaratibu huu...

Kwa mfano, kama ambavyo mtu unaweza kupokea msg ambayo source yake ni CRDB, M-PESA etc, imagine uwezekano wa watu kupata msg ambayo inaonyesha kwamba inatoka CHADEMA na ambayo inahimiza watu wakajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura na mambo mengine kama hayo !. Ni njia ambayo itawawezesha chama kuwafikia mamilioni ya watu in a matter of minutes na kufikisha ujumbe unaokusudiwa !. Pamoja na kuwaza huku, bado nilikuwa na wasiwasi kama CCM itakubali kirahisi wapinzani wawe na uwezo wa kuwafikia wananchi kwa njia hii na kwa urahisi hivi.....most likely wangeweza kuwatumia TCRA, kujaribu kuibua sababu mbali mbali za kuzuia kitu kama hiki......

Mimi naamini kwamba ubunifu wa Chadema kwa kuanzisha program zao tatu, utawezesha hiki nilichokiongelea hapo juu, kufanyika kwa ufanisi mkubwa !

Program hizo tatu ni :

E-membership --- kama inavyojieleza kwa jina lake itawawezesha wale wanaotaka kuwa member wa chama kuweza kufanya hivyo kwa njia ya mtandao....

E-media ---- itawawezesha wanachama na wananchi kwa ujumla kuweza kupata taarifa mbali mbali za chama baada ya kujiunga na hiyo huduma

E-movement ---- baadhi yetu tayari tumeitumia hii huduma siku ya uzinduzi. Kwa kutumia njia hii watu mbali mbali wanaweza kuchangia harakati za chama kirahisi tu kwa njia ya mtandao.

Nitatoa maeleozo ya ziada kidogo kwa huduma mbili (e-movement na e-media) :

E-MOVEMENT
Kilichoanzishwa na CDM kupitia hii huduma ni kitu kikubwa sana !. Sio tu kwamba tarehe 31 October 2014, kulifanyika fundraising kwa kupita hii huduma, bali kikubwa zaidi kulianzishwa utaratibu wa kuchangisha fedha endelevu ambao watu wanaweza kuhamisishwa kuchangia kwenye kila mkutano wa hadhara na hata mitaani kwenye interactions za kila siku !. Imagine katika kila mkutano wa CDM watu wawe wanahimizwa kuchangia (wale wanaoweza) angalau alfu moja kwa njia ya mtandao hapo hapo mkutanoni !. Wengine watachangia hata zaidi ya hiyo 1000 na wanaweza hata kuendelea kuchangia baada ya mkutano. Kwa mfano mimi nilichangia hela nzuri tu kwenye uzinduzi na nitaendelea kuchangia kiwango kama hicho kila mwezi. Vile vile nikiwa katika maongezi ya kikazi na mtu mmoja, nikatumia muda huo kumshawishi na yeye achangie na akakubali kuchangia hela kubwa tu ! Ninaamini uhamasishaji ukiwa mzuri, tutakuwa na hela za kutosha sana kupitia utaratibu huu ambazo zitatusaidia katika harakati zetu kama CDM kwa kushirikiana na UKAWA kuitoa CCM madarakani....

E-MEDIA
Kwa mawazo yangu hii program ndio funga kazi !.

Kama watu wataweza kusubscribe bure kwenye hii huduma na kuweza kupata bure, taarifa za CDM na hata UKAWA kupitia SMS, then ninaamini tutapata mafanikio makubwa sana !. Kazi ambayo inabidi ifanywe kwa nguvu mara baada ya huduma hii kuwa hewani, ni kuwashawishi watu wote wanaohudhuria mikutano mbali mbali ya chama kusubscribe/kujiunga na huduma hii. Ikiwezekana katika kila mkutano au mkusanyiko wa kisiasa, dakika kama tano zinaweza kutumika kwa wale wote ambao hawajajiunga waweze kujiunga hapo hapo kama watapenda kufanya hivyo.

Watu vile vile wawe encouraged kuwashiwishi ndugu, jamaa na marafiki zao wajiunge na huduma hiyo !. Tukifanya hivi katika miezi michache ijayo tunaweza tukawa na mamilioni ya watu ambao wamejiunga na huduma hii !. Imagine kabla ya uchaguzi mkuu, tuwe na watu wanaofikia million kumi waliojiunga !.....Uzuri wa hii huduma ni kwamba watu wanajiunga wenyewe na wengi wa hao watakuwa na interest na hivyo kwa kujua idadi yao tayari tutakuwa na indication ya watu ambao most likely watatusupport katika uchaguzi.

Faida ya hii huduma, mimi ninavyoiona, si kwa taarifa mbali mbali kutoka kwenye uongozi, bali zaidi faida ninaiona katika kutoa maelekezo au instructions kwa wale waliojiunga !. Itakuwa rahisi kwa mfano, kuhamasisha watu kuchangia shughuli za chama kupitia huduma ya e-movement !

Hebu fikiria hizi possibilities..........

  • Imagine siku mbili au tatu kabla ya muda wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu kwisha, ujumbe wa SMS unaingia kwenye simu za watu wapatao million kumi ukihimiza watu kwenda kujiandikisha na wakati huo huo ukihimiza watu hao wote wausambaze ujumbe huo kwa ndugu jamaa na marafiki zao !.

  • Imagine siku moja kabla ya uchaguzi, ujumbe wa SMS unaingia kwenye simu za watu wapatao million kumi ukikumbusha kupiga kura siku inayofuata bila kujali hali ya hewa ya siku hiyo kwani kila kura ina thamani na kuwahimiza vile vile wawahimize ndugu, jamaa na marafiki kuhakikisha nao wanapiga kura !

  • Imagine wakati fulani katikati ya campaign kukatokea uhitaji wa hela kwa ajili ya kuwasaidia wagombea mbali mbali wa UKAWA na hapo kukatumwa ujumbe kwa watu wote waliojiunga ukiwahimiza kwamba siku hiyo hiyo kwa wale wanaoweza wachange angalau 500 kila mtu ili kufanikisha harakati za campaign !. In just one day unaweza ukapata billions !

Kwa ubunifu huu, kinachotakiwa ni kuhakikisha tu kwamba watu wengi sana wanajiunga na huduma hii na baada ya hapo, the possibilities are endless !. Ninaamini IKAWA unaungwa mkono na mamilioni ya watanzania na uwezekano wa kupata watanzania wanaofikia million kumi kuweza kujiunga na huduma hii ni jambo ambalo linawezekana kabisa.

Tukiwa na idadi kama hii itarahisisha sana kuiondoa CCM madarakani kwani :

  • Hawa ndio watakaoshawishiwa waipigie kura UKAWA hasa kwa jumbe zilizosukwa kitaalamu kwa kuvishirikisha vyama vingine vya UKAWA na kufikia wote waliojiunga kwa njia ya SMS,

  • Hawa watasaidia kusambaza jumbe hizo kwa ndugu, jamaa na marafiki wao, wajiandikishe na kuipigia kura UKAWA

  • Na hawa hawa ndio ambao hata kama wakitakiwa kuchangia miatano kila mmoja (pale inapobidi) , kwa wingi wao watawezesha kupatikana kwa billions of money in a matter of days

The possibilities are endless !

Asante kwa uchambuzi na maelezo ya kina yanayojitosheleza vizuri sana, usijali kwa wale watakaokuja kuponda, wanafanya hivyo kwakuwa hawana kingine cha kufanya
 
Back
Top Bottom