Kwa tulioumwa mafua yale ni mashahidi tosha, nahisi ile ilikuwa ni Covid 19

Mwaka huu nimeumwa mafua mabaya kwenye hiatoria ya maisha yangu nimeteseka two weeks nikishindwa kuhema, kifua kunibana Sana joto la mwili kuwa juu Sana plus homa Kali, hafu kifua kikavu sibanji Ila kukosa hewa tu Mara nyingi, mpaka nikawa siwezi kula balaa lingine na ma tonsils yakaanza, kichwa hakiponi hata nitumie Nini aisee Yale mafua kiboko kabisa. Naomba Mungu yasinirudie Tena kukosa pumzi ni kufa huku unajiona ka samaki aliyetolewa majini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu nimepita hizi shuhuda za kuugua mafuta na homa kali na viambatisho vyake. Kifupi wengi waliugua Korona bila kugundua. Kilichosaidia ni Immune System kuwa juu. Africa ikiwemo Tanzania tuna bahati pia ya chakula asili ambavyo siyo GMOs. Genetically Modified Organisms kwa mazao madhara yake ni kwenye afya na tiba. Tanzania unapata ndimu, limao na chungwa la asili kiaina. Ninachoomba kwa Moferators wa PIN huu Uzi ili uwe unasomwa na kutolea shuhuda na wote waliougua Mafua makali na pneumonia iwe mild or intense. Na tiba asili walizotumia. Hii itasaidia wengi mno.

Kifupi nyumbani kuanzia sasa usikose citrus zote kama machungwa, ndimu, limao na spices kama kitunguu maji na swaumu, pilipili manga, karafuu, tangawizi n.k. Na kubwa kuliko ASALI WA NYUKI WAKUBWA NA WADOGO.

KIRUSI CHA KORONA HATOBOI HAPO KABISA.

PIA ENDELEA KUIMARISHA KINGA KWA MBOGA NYINGI NA MATUNDA.
 
Aysee... Kuanzia mwezi watatu mwanzoni niliumwa balaa. Mafua makali, kikohozi kikali, homa Kali. Nilienda hospital nilimaliza vipimo karibu vyote bila mafanikio. Naamini ilikuwa ni hiyo korona
 
anasema haya ni mafua kma mafua mengine ila kuna watu wameamua kueka tension kwenye huu ugonjwa jwa naslahi yao... watakuja kuleta chanjo either waziuze ghali au wafanye chochot watakacho.. huu ugonjwa si mkubwa kama unavyo tangazwa, ni nguvu ya media tu imetumika kuteka tension za watu.. imagine death rate ya ugonjwa ni 3% tu means kwenye watu 100 ni 3 tu ndo hufa.. imagine tangu december last year waliokufa hawafika hata 100K wakati kuna cancer imeshauwa takriban watu Mil 2 ndan ya miez mi3 tuu... sasa kwann corona? ni upuuzi mtupu nothing else zaid kuna watu nyuma ya pazia wana maslahi binafsi
Jamaa kwenye hili alikuwa anazungumzia nini??

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika ilikuwa baba lao. Sijawahi kuugua homa kali, mafua, kikohozi na joto kali namna ile tangu nizaliwe.

Tuliugua familia nzima na dalili zote zinafanana akianzia mtoto wa miaka 2. Tatizo lilianza baada ya kusafiri kutoka Geita kwenda Kahama.

Nilipata tatizo la kupumua hadi nikapoteza fahamu nikiwa kwenye mizunguko yangu ya kutafuta riziki.

Hakika Mungu ni mwema.
 
Na mafua i wiki sasa haya katiki duh

Sent from my SM-A105G using Tapatalk
 
Hiyo ni kweli mkuu hata mimi ilinikuta hiyo khali mwezi February. Nilitoka mkoani nikarejea DSM kufika tu nikahisi kifo maana kichwa kilipiga pande zote mixture mafua makali sana sijawahi kuona.Nikaenda Kinondoni Hospital kupima hamna tatizo sio Malaria wala Ukimwi.Ila nakumbuka nilipima full blood picture FBP ilionesha kupungua kwa Kinga mwilini na uwepo wa virus wakutosha tofaut na mwez mmoja nyuma ilikua optimal.Nilitumia antibiotics za kawaida nikarejea normal after one week

Sent using Jamii Forums mobile app


Watu wanasema wazungu hawatoboi kwa Covid 19, sasa wape ushuhuda kwamba wewe ulitoboa.
 
Kwani ulipimwa vipimo gani hadi useme negative?

Watu wengi hamfahamu kuwa kila kipimo kipo specific kutegemea mtaalamu anataka kuona nini.Huwezi kupima malaria halafu eti wakuambie wameona influenza badala ya plasmodia.
Hapo utaambiwa tu negative ila ni negative ya malaria si kitu kingine
Ni kweli mkuu, wataalamu wengi wanasema ilianza wakati huo.

Mie pia nilibanwa nikahisi ni Influenza lakini vipimo vikawa negative. Nikaishia kupona tu kwa kutuliza homa. Ilikuwa mwezi wa kumi na moja mwaka jana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli tunaweza kuteseka na marufuku nyingi za kutosafiri,kufunga shule na vyuo,kupanda kwa bei za vitu,ila ukweli ni kwamba ni kwa sababu tulikosa vipimo tangu awali.

Na kama kanuni,huwezi kusema ilikuwa covid 19 kwa vile haikupimwa.

Ila swali langu kwa aliyefanya utafiti akaona ni mafua ya kawaida yaani influenza,je walipima sampuli ngapi ku confirm case za influenza?Au ukiwa mtalamu unaruhusiwa kuhisi na ikawa ni sawa tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu
Mwaka jana mwishoni Dar ilikumbwa na ugonjwa wa mafua wa ajabu ambao ulisababisha wizara kutoa tamko kama linavyosomeka hapo chini

Kiukweli mimi nilikua ni mmoja wa watu niliougua mafua hayo, hali ile ilikua haina tofauti hata kidogo na hii corona wanayoisema sasa
Nilitembelea hospitali kama mbili hivi hapa mjini ili kubaini ni kitu gani kilinikuta,, homa ilikua kalo, kupumua kwa shida, joto kali sana lakini unaisikia baridi kali

Nilipimwa hospitali pasipokukutwa na gonjwa, ndipo nikalazimika mpaka kupiwa HIV lakini nayo hakuna!

Yale mafua yalinikondesha ghafla maana hata kula sikuweza

Leo ndio naikumbuka hii barua ya wizara, naicompare na COVID 19

View attachment 1409898
Ile n covid 17 WEWEE
19 ungeshakufaa sasaahizi unachat na jf ya Peponi kama ipo
 
Kwani ulipimwa vipimo gani hadi useme negative?

Watu wengi hamfahamu kuwa kila kipimo kipo specific kutegemea mtaalamu anataka kuona nini.Huwezi kupima malaria halafu eti wakuambie wameona influenza badala ya plasmodia.
Hapo utaambiwa tu negative ila ni negative ya malaria si kitu kingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kipimo ambacho nimezungumzia hapo ni cha influenza. Kutokana na dalili zangu walifikiri nina flu.
 
Back
Top Bottom