Kwa tulioumwa mafua yale ni mashahidi tosha, nahisi ile ilikuwa ni Covid 19

Habari wakuu
Mwaka jana mwishoni Dar ilikumbwa na ugonjwa wa mafua wa ajabu ambao ulisababisha wizara kutoa tamko kama linavyosomeka hapo chini

Kiukweli mimi nilikua ni mmoja wa watu niliougua mafua hayo, hali ile ilikua haina tofauti hata kidogo na hii corona wanayoisema sasa
Nilitembelea hospitali kama mbili hivi hapa mjini ili kubaini ni kitu gani kilinikuta,, homa ilikua kalo, kupumua kwa shida, joto kali sana lakini unaisikia baridi kali

Nilipimwa hospitali pasipokukutwa na gonjwa, ndipo nikalazimika mpaka kupiwa HIV lakini nayo hakuna!

Yale mafua yalinikondesha ghafla maana hata kula sikuweza

Leo ndio naikumbuka hii barua ya wizara, naicompare na COVID 19

View attachment 1409898
Sawa dawa uliyotumia kukuweka hai hadi sasa ipi na je una family kama unayo wanahali gani maana hili janga linaambukiza au ulijifungia peke yako hadi ukapaona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mie nliugua mafua makali mno, mwez wa kwanza,, nlienda hosptal nikaambiwa hayo ni mafua ya virus,,

Nakumbuka mwezi mzima nliugua,, kikohozi, mafua, vidonda kooni, kichwa kuuma, homa mwili kuchemka,

Ilifikia hatua nikasema labda HIV +

Nikachek niko -



Sent using Jamii Forums mobile app
 
#NAKUBALIANA
niliumwa sana pia nov 2019 hadi 20 dec 2019 nilipimwa maabara magonjwa mengi tu lakini haikusaidia dr aliniandikia dawa nyingi tu,ilibidi nirudi kwa dr tena nikapimwa maabara tena na dawa zingine na uku home nanywa asali na tangawizi.nilikuaja pona kabla ya christmas sikuamini!!sijawai umwa vile tokea najitambua..kubanwa pumzi ukilala adi uamke unapumulia mdomo,kikohozi,homa kali na joto,kolomeo,kuchoka viungo sana
 
Mimi nmeugua week kadhaa zilizopita jaman afu ilinianzia alhamisi usiku ndani niko pekeangu yaan nliumwa jamani kulukua hakulaliki ndani hospital amna kitu...mafua makali, kichwa, mwili kuchoka, joto kama moto wa mkaa ndio upo mwilini, kifua mapafu kushindwa kupumua aise sio kwa kuumwa kulem...nashukuru Mungu nliombewa hapohapo nikapona ...maana nlikua nashindwa hadi kuka aptite ilikua less, yaan kile kifua kilikua sio cha nchi nlikua siwez kupumua pumzi ilikua inabana koo lilikua kavu acha kabisa .. maombi ndio yaliniponya na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wangapi hapa wamesema walivyoenda hopitali hawakupatikana na kitu? Na bado walikuwa na dalili zilezile?
Kwa hiyo huwezi kwenda kupima kitu ambacho hakipo!! Ila the fact kwamba wamesurvive makes reality kwamba huu ugonjwa unapona, mengine siyo ya nchi zetu, tuwaachie wao wapambane na mafua, wacha sisi tutaabike na vipindupindu.
Kujikinga ni sawa Dennis, lakini bado Corona sio tishio.
Kwan nimesema wapi watu hawaponi, nimesema mafua yapo ya aina nyingi, na covid-19 ni aina mojawapo ya mafua, huwezi sema ilikuwepo bila kuwa na scientific prove, tujaribu kuwa waelewa
 
Kwan nimesema wapi watu hawaponi, nimesema mafua zipo za aina nyingi, na covid-19 ni aina mojawapo ya mafua, huwezi sema ilikuwepo bila kuwa na scientific prove, tujaribu kuwa waelewa
Dennis ulitegemea scientific prove ipatikane wapi kama sio Hospitali? Na watu wameenda, baada ya kupata dalili hizo hizo japo jina la Corona halikuwepo!!! Na waliambiwa kitu kingine,
Baadaye dalili zilezile zimepewa jina la Corona, kwanini unazikataa dalili kwa sababu ya Jina?
Unatishwa na jina?Lakini dalili ni zile zile na kuugua ni kulekule, kwa hiyo hutaki? Kwa sababu jina limekuja baadaye kwa dalili zile zile?
 
Mimi pia. Hapa Arusha nilikamatwa na Homa Kali Sana.. bia haikupita ulimini.. ikabidi niende St. Elizabeth kitengo Cha HIV.. nikawa Sina Ngwengwe.. nakumbuka niliandika Humu
 
Barua hiyo inaonesha hatuna aidha wataalam au vyombo/ mitambo ya kisasa kubaini virusi/ bacteria na magonjwa mapya.
Unaingia chuma cha Daktari. Unamweleza shida yako kuhusiana na unavyojisikia anakujibu kwa haraka kwamba tatizo lako ni mafua na kwamba mafua hayana dawa. Hivyo anakushauri urudi nyumbani, pumzika na kunywa maji mengi. Laiti wangejiongeza kidogo na kustukia idadi kubwa ya watu waliougua wakati ule tungeweza kuiokoa dunia na janga hili. Lakini kizingiti kikubwa ni ukosefu wa vifaa vya kutambua ugonjwa huu. Hospitali zetu hazikuwa na vifaa hivyo na hadi sasa sampuli zinapelekwa maabara kuu ya Serikali kwa uchunguzi.
 
Hapa Tanzania madaktari wangekuwa na Jarida la Medical Journal Tanzania na kufuatilia kisayansi ushuhuda wenu kuhusu haya mafua ya ajabu kwa kwenda kuchunguza vipimo, damu, makohozi na taarifa za waliolazwa au kufika hospitali kupata ushauri wa madaktari, Tanzania ingekuwa mbele kitabibu kwa angalau kutoa angalizo ya namna gani ya kujikinga, kujilinda na kujifungia ndani.

Yote kwa yote wanaJamiiForums mmeonesha njia ya jamii kubwa ku- share taarifa juu ya mlipuko wa gonjwa lolote la ajabu na labda Wizara ya Afya, Madaktari Watafiti, Vyuo Vikuu vya Udaktari wataanzisha utamaduni wa kupita hapa JamiiForums na kuanzisha uchunguzi kwa kila taarifa nyingi za afya ya jamii (pubilic Health) na kuzihifadhi ktk Medical Journal Tanzania.

Dhima ikiwa ni kufanya utafiti kugundua dawa au njia ya kuzuia maambukizi ktk jamii na kujikinga mapema, bila kusubiri kuiga au kutegemea kusikilizia taarifa za watabibu 'mabeberu' wanasema nini huko China, Ulaya na Marekani ya Kaskazini.
www.mcdgc.go.tz › index.php › view
Mahali pasipo na daktari… - mcdgc

Full Title : Mahali pasipo na daktari...: kitabu cha mafunzo ya afya vijijini, David Werner Dar Es Salaam, Rotary International, Tanzania: ..

Ushuhuda wa Chris Cuomo mwandishi nguli aliyebainika kuwa na Covid-19 na kuhusu gonjwa hili linalokutesa kila usiku wa manane kwa homa kali, kubanwa pumzi / kifua , debe la jasho , kukonda ghafla (kupoteza uzito wa mwili) .....

2 Apr 2020
During a COVID-19 update on Thursday, New York Governor Andrew Cuomo remotely interviewed his brother and CNN anchor Chris Cuomo who tested positive for the virus and is in self-isolation at his home.



Chris said that he is feeling better, but that the illness is “very tough" and he understands why it has such an impact on infected individuals.
Source : Global News
 
Hapa Tanzania madaktari wangekuwa na Jarida la Medical Journal Tanzania na kufuatilia kisayansi ushuhuda wenu kuhusu haya mafua ya ajabu kwa kwenda kuchunguza vipimo, damu, makohozi na taarifa za waliolazwa au kufika hospitali kupata ushauri wa madaktari, Tanzania ingekuwa mbele kitabibu kwa angalau kutoa angalizo ya namna gani ya kujikinga, kujilinda na kujifungia ndani.

Yote ya yote wanaJamiiForums mmeonesha njia ya jamii kubwa ku- share taarifa juu ya mlipuko wa gonjwa lolote la ajabu na labda Wizara ya Afya, Madaktari Watafiti, Vyuo Vikuu vya Udaktari wataanzisha utamaduni wa kupita hapa JamiiForums na kuanzisha uchunguzi kwa kila taarifa nyingi za afya ya jamii (pubilic Health) na kuzihifadhi ktk Medical Journal Tanzania.

Dhima ikiwa ni kufanya utafiti kugundua dawa au njia ya kuzuia maambukizi ktk jamii na kujikinga mapema, bila kusubiri kuiga au kutegemea kusikilizia taarifa za watabibu 'mabeberu' wanasema nini huko China, Ulaya na Marekani ya Kaskazini.
Asante kwa ulichokiandika hapo juu. Scientific Journal la Madaktari wa Tanzania ni muhimu katika kubadirishana mawazo kuhusiana na maradhi ambayo yanaweza kujitokeza hapa nchini. Hizi taarifa zingetolewa katika jarida hilo, madaktari wangeweza kushtukia hali hii na pengine kutoa ushauri kuhusu hatua ya kuchukua. Lakini historia inaonesha hata wao pengine walihisi kitu fulani lakini wanabanwa na sheria au agizo lisemalo hawana mamlaka ya kutangaza uwepo wa ugonjwa katika nchi hii. Bado tunakumbuka jinsi Mkurugenzi wa NIMRI alivyondolewa madarakani.
 
Tatizo kubwa la nchi zetu sidhani kama kuna ushirikiano wa utabibu na dunia nyingine
Wenzetu kama tatizo linatokea wanauliza kwa wataalamu wakubwa duniani kwa mfano Canada amekwama mahali atauliza USA na kutuma sample kujua huo ni ugonjwa gani
Hakuna aibu katika magonjwa bali magonjwa yanatofautiana sana
Sisi waafrika tumejifungia sana na ndio maana tunakuwa nyuma kwa kila jambo

Inawezekana maradhi yetu mengi yanapona kwa dawa kadhaa ambayo huenda Venezuela wana tiba yake
Medical journal inatoa mengi sana ila ni madokta wachache sana wanasoma
Tujifungue na dunia kama ni sample au utafiti utumwe hata Cuba


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Asante kwa ulichokiandika hapo juu. Scientific Journal la Madaktari wa Tanzania ni muhimu katika kubadirishana mawazo kuhusiana na maradhi ambayo yanaweza kujitokeza hapa nchini. Hizi taarifa zingetolewa katika jaribu hilo, madaktari wangeweza kushtukia hali hii na pengine kutoa ushauri kuhusu hatua ya kuchukua. Lakini historia inaonesha hata wao pengine walihisi kitu fulani lakini wanabanwa na sheria au agizo lisemalo hawana mamlaka ya kutangaza uwepo wa ugonjwa katika nchi hii. Bado tunakumbuka jinsi Mkurugenzi wa NIMRI alivyondolewa madarakani.

Jarida hilo liwe linaandikwa kwa Kiingereza na Kiswahili na kutolewa machapisho mengi kila mwezi kuelezea "hali ya afya ya jamii" Tanzania huku likibainisha ni magonjwa gani yanaisumbua jamii yawe mapya au yaliyopo pia kinga, matibabu na dawa zake na ushauri kwa jamii. Kinga ni Bora kuliko Tiba.

Nchi masikini kama Cuba zenye bajeti finyu ya serikali na wananchi 'wanyonge' kiuchumi, mfumo wao wa kukabiliana na magonjwa ni Kinga ni Bora kuliko Tiba na wanafanikiwa kwa kuwahusisha wananchi kupitia kampeni za elimu ya afya na kuitaarifu jamii kuhusu kinschoendelea kiafya na tishio la magonjwa.
 
Hata mimi yalinipata hayo mafua, joto kali lakini nikiwasha feni nasikia baridicla kufa kufa kabisa, nadhani ilikuwa ni Corona ile..
 
Mimi sikushikwa na kikozi ila mafua, sijawahi ktk maisha yangu nikabanwa na mafua kiasi cha kumka usiku wa manene.

Nilimeza dawa mbalimbali kabla ya usiku huo ila zilidunda, nilipozidiwa nikalamba asali, hapo ndipo pona pona ilitokea ile siku, baada ya hapo nikaoga kama dakika 20 hivi, nikazidi kujisikia nafuu.

Nikachukua asali kidogo nikaweka puani, nikapiga chafya nikatoa mafua mengi, hii siku na mimi siwezi kuisahau.

Niliamka usiku wa maneno maana niliona nina shida ktk upumiaji, hamuwez kuamini wakuu ila kupumua ilikuwa ni shida, nilikuwa nahemea mdomo, sikuwahi kuumwa mafua kiasi hiki na mwili wote una joto kali mno.

Isingekuwa asali huenda ningejisikia vibaya zaidi, naunga mkono hoja ya mleta mada.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiku wa manene na usiku wa maneno pole sana mkuu mi mpaka leo napiga chafua toka februari
 
Barua hiyo inaonesha hatuna aidha wataalam au vyombo/ mitambo ya kisasa kubaini virusi/ bacteria na magonjwa mapya.
Tuna wataalamu na madaktari mabingwa na wabobezi, tatizo ni vifaa, na hata vichache vilivyopo ni obsolete, na wagonjwa kukamuliwa hela nyingi sana. Hela zinaliwa na wanasiasa na siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom