Jayfour_King
JF-Expert Member
- Nov 15, 2009
- 1,135
- 128
Nimewahi kusikia malalamiko kuhusu uhifadhi wakati wa kusafirisha samaki wabichi kutoka baharini na maziwa mbalimbali kwenda masafa ya mbali yaliko masoko ya bidhaa hizo katika miji mbalimbali. Malalamiko hayo niliyasikia kama fununu kwamba kuna baadhi ya wafanya biashara wasio waadilifu ambao hutumia madawa yasiofaa kwa ajili ya ku preserve hao samaki tayari kwa kusafirisha.
Kwa sasa nashawishika kuamini kwamba kuna mambo yasiyo ya kawaida katika biashara hii kwa uzoefu wangu mwenyewe. Jana nilirudi nyumbani kama kawaida na kukuta kitoweo cha samaki wabichi (fresh) nikaona mambo si ndio haya. Nikala chakula kwa raha zote, cha ajabu ni kwamba vyoo vya nyumbani siku hiyo havikutosha, kwani kila mtu (nyumba nzima) tulikuwa tunaharisha!!
OMBI KWA TFDA NA MA AFISA AFYA WA MIJI/MAJIJI:
Afya za watanzania zinategemea umakini wenu, hivyo malalamiko haya yamekuwepo muda mrefu watu kulalamikia hali hii na madawa feki. Kwa hii biashara ya samaki nayo naamini inahitaji kuangaliwa kwa makini vinginevyo afya zetu tumeweka rehani.
Kwenye kuku (dawa za kurefusha maisha ARV's)
Kwenye samaki (dawa za kuhifadhia maiti)
Madawa ya binadamu (feki na yaliyoisha muda wake)
Kuna usalama hapo?
Tusaidieni kwa hili!!