camberlizer
New Member
- Jan 10, 2018
- 4
- 4
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa watumishi ngazi ya serikali za Mitaa hasa kada ya Watendaji wa Vijiji (VEO) na Mitaa (MEO). Malalamiko yanayotokana na Mishahara midogo isiyokidhi gharama za maisha. Ukilinganisha na majukumu yao na Mazingira yao ya kazi.
Malalamiko na vilio vyao vinaishia kupotelea hewani kama machozi ya samaki kwenye maji, bila kutafutiwa ufumbuzi. Na bado wanaendelea kuitumikia serikali kwa hali zao zote bila kuleta mgomo wala kufanya maandamano ya aina yoyote.
Hivyo naishauri Serikali iwakumbuke hawa watumishi wao walio wapeleka vijijini mbali na miji yao ya asili, kwajili ya kutekeleza majukumu yao. Kwa nyongeza za mishahara na hata ofa mbalimbali.
TUPAZE SAUTI KWA PAMOJA