Kwa TFDA na idara za afya

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Nimewahi kusikia malalamiko kuhusu uhifadhi wakati wa kusafirisha samaki wabichi kutoka baharini na maziwa mbalimbali kwenda masafa ya mbali yaliko masoko ya bidhaa hizo katika miji mbalimbali. Malalamiko hayo niliyasikia kama fununu kwamba kuna baadhi ya wafanya biashara wasio waadilifu ambao hutumia madawa yasiofaa kwa ajili ya ku preserve hao samaki tayari kwa kusafirisha.

Kwa sasa nashawishika kuamini kwamba kuna mambo yasiyo ya kawaida katika biashara hii kwa uzoefu wangu mwenyewe. Jana nilirudi nyumbani kama kawaida na kukuta kitoweo cha samaki wabichi (fresh) nikaona mambo si ndio haya. Nikala chakula kwa raha zote, cha ajabu ni kwamba vyoo vya nyumbani siku hiyo havikutosha, kwani kila mtu (nyumba nzima) tulikuwa tunaharisha!!

OMBI KWA TFDA NA MA AFISA AFYA WA MIJI/MAJIJI:

Afya za watanzania zinategemea umakini wenu, hivyo malalamiko haya yamekuwepo muda mrefu watu kulalamikia hali hii na madawa feki. Kwa hii biashara ya samaki nayo naamini inahitaji kuangaliwa kwa makini vinginevyo afya zetu tumeweka rehani.
Kwenye kuku (dawa za kurefusha maisha ARV's)
Kwenye samaki (dawa za kuhifadhia maiti)
Madawa ya binadamu (feki na yaliyoisha muda wake)
Kuna usalama hapo?
Tusaidieni kwa hili!!
 
Ni kweli nadhania kila msafirisha samaki anawasafirisha tu kama mzigo mwingine; hakuna udhibiti na sijui ka akuna watu wa hii idara wanaokagua hili eneo; Kuna tetesi kuwa dawa za kuhifadhia maiti zinatumika ama mafuta cjui yann yanatumika.
 
Pole JF-K,ndo nchi yetu hakuna mtu anayemjali mtu mwingine kwa dhamana aliyopewa.
Juzi nilisoma gazeti mwananchi niliishia kutikisa kichwa huko bagamoyo disp./vituo vya afya waliomba wapelekewe dawa na hawa MSD ambazo waliziorodhesha chakushangaza MSD
wakapeleka mabox yote yamejaa kondom!!
 
Hawa ma Afisa Afya ni watu muhimu sana ktk afya zetu sasa sijui shughuli zao wanziendesha kilocal sana yaani shule wameenda (sasa kuna degree yao pale muhimbili) lakini watembelee maofisini kwao bana we
 
Pole JF-K,ndo nchi yetu hakuna mtu anayemjali mtu mwingine kwa dhamana aliyopewa.
Juzi nilisoma gazeti mwananchi niliishia kutikisa kichwa huko bagamoyo disp./vituo vya afya waliomba wapelekewe dawa na hawa MSD ambazo waliziorodhesha chakushangaza MSD
wakapeleka mabox yote yamejaa kondom!!
Hapo ndio wizi wa mchana hufanyika, inawezekanaje sisi tumeagiza kloroquine halafu tunaletewa kondom. Utata mtupu hebu fikiria walitumia maombi gani kuandaa hiyo oda ya kondom. Hivyo utaona idara nzima imeoza kuanzia walinzi wafagizi hadi mtunza stoo husika.

Safari bado ndefu tuombe tufike salama.
 
H/G wako hajui kupika samaki, kama shida ilitokana na madawa matokeo yake mungewashwa sana na kuvimba sio kuharisha.
 
H/G wako hajui kupika samaki, kama shida ilitokana na madawa matokeo yake mungewashwa sana na kuvimba sio kuharisha.

Yaani wewe hata kukuelimisha inakuwa kazi,kwa hiyo wewe unachojua ni allergic reaction ya dawa tuu basi,hakuna madhara mengine ambayo yanaweza kutokea!!!!!!!!!Na umejuaje kwamba jamaa wangewashwa sana na kuvimba na sio kuhalisha au na wewe ni mmojawapo nini!
 
Back
Top Bottom