Kwa Tanzania hii ya sasa na hasa wale waliopo huko / humo ( Eagle Wing House ) hili la Uingereza linawezekana?

Mwanamama Mmoja huko nchini Uingereza amempongeza sana Marehemu Mumewe hadi kumuita ' Shujaa ' hasa kwa Kitendo chake cha ' Kumficha ' kwa miaka 64 kuwa Yeye ( Mumewe ) alikuwa ni Mwana Usalama wa Taifa wa nchini Uingereza.

" Japo leo namzika Mume wangu na nilikuwa sijui muda wote kuwa ni mwana Usalama wa Taifa mpaka pale Wakubwa zake walipokuja hapa Msibani na Kunifahamisha hilo. Hata Wao wenyewe ( Mabosi zake ) walijua labda Mume wangu aliniambia kwakuwa nilikuwa Mkewe ila haikuwa hivyo na kiukweli japo Mume wangu amefariki ila kwa Kitendo chake cha Kunificha katika hili tena kwa miaka yake yote 64 aliyokuwa huko ( Usalama wa Taifa ) namuita ni Shujaa na kwakweli Idara ya Usalama wa Taifa ya Uingereza ilimpata Mtu mahiri, muhimu na Shujaa aliyeitendea vyema Kazi yake hiyo "

Je kwa Tanzania hili linawezekana? Je wana Usalama wa Taifa ( Eagle Wing House ) hasa hawa wa sasa achilia mbali wale ' Wastaafu ' wana uwezo na ' Ushujaa ' huu kama aliokuwa nao huyu Mwenzao kutoka nchini Uingereza kiasi kwamba wanaweza ' Kujificha ' si tu kwa Watu baki bali hata kwa Ndugu zao, Wake zao, Marafiki zao na Jamaa zao?

Nawasilisha.
Mkuu huku ngumu . huku marakibao tumekutana na vitisho vya hawa jamaa hasa wakilewa au wakikasirishwa kwenye ugonvi. Kuna mmoja aligonga gari nyingine pale manzese acha apige mikwara ooh "mnajua Mie ni nani " watu wakabaki wanamshangaa.
 
Kila Mtu akifanya majukumu kwa Mahadili sehemu ya kazi yake tutafika mbali sana.

Naamanisha kujua wajibu wa Kazi yako na Wajibu wako kama mfanya kazi, iwe kwa sehemu yoyote ile Mahadili ni kitu muhimu.
 
duh.... Mchungaji Modestus Kipilimba ni mpaka pale alipoteuliwa kuwa mkurugenzi ndipo watu wakashangaa..... Kuna yule mwingine Magufuli alimtaja mbele ya kadamnasi hadi IGP akashtuka .... wapo watu wanatunza siri sana.
 
Hata yule big ambaye ni PSU wa Ngosha, miaka ile anasoma MALIMBE kitivo cha sheria hakuwahi kujisifu kabisa wala hatukumjua kabisaaa mpaka alipomaliza ndio tukaanza kumuona kwenye misafara ya wakubwa.
Nimewahi sana kujiuliza ile sura niliiona wapi, jamaa alikua anahudhuria sana kwenye kile kibanda umiza cha nyamalango na alikua mbishi sana kwenye mechi ila kiujumla he's good people..
 
Nilipoteana na rafiki yangu tangu 1998. Siku nakutana nae by appearance tu ya kimavazi nikajua jamaa ni TISS. Nilipomuhoji anapofanyia kazi licha ya kunidanganya kwa ulimi lakini macho yake yalimsaliti. At the end he accented to the truth kuwa ni kitengo attached ktk ofisi fulani hivi. Mi nashauri TISS Mpotezee hizo suti zenu. Jichanganyeni na kila aina ya vazi. Plus msiwe serious mkiwa kitaa kiasi mnapoteza hata ile social interaction.
Kama mimi ukinikuta huwezi kunijua yani kwanza najichanganya na masela kinyama yani halafu nina udevu ka Osama! Sina makuu ila ukinzingua ntakuuliza "unan'jua mi ni nani?!!"
 
Afu possibly nilikutana nawe Mkuu :-D, maana si kwa udevu ule. Hata James Harden kasingiziwa
Kama mimi ukinikuta huwezi kunijua yani kwanza najichanganya na masela kinyama yani halafu nina udevu ka Osama! Sina makuu ila ukinzingua ntakuuliza "unan'jua mi ni nani?!!"
 
Uingereza wana idara kuu mbili maarufu. Idara ya Ujasusi wa kimataifa a.k.a Military Intelligence 6 (MI6) ama Secret Intelligence Service (SIS) kama inavyojulikana kileo. Pia wana idara ya Ujasusi wa ndani iitwayo MI5. Hio ni kama ilivyo FBI kwa Marekani na SHINIBET kwa Israeli. Na pia ni sawa na ilivyokuwepo Second Chief Directorate ya zamani za KGB. Huku MOSSAD ya Ujasusi wa nje ya Israeli ilivyo CIA kwa Marekani. Ntashukuru nikisahihishwa.
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Huko Eagle Wing house; kuna watu wa aina mbili tu ambao ni "COVERT NA OVERT" hawa overt ndio wenye shida hiyo unayoizungumzia sasa mana nao wamegawanyika kuna "Suveilensi na ripota" shida kubwa hasa ipo kwa hao ripota na lau kidogo suveilensi ambao wamo na transpota huwa ni ngumu kuwajua na wanaheshimu sana kazi zao kuliko maripota lakini pia maripota nao wamefanikiwa kujizuia japo si wote!!

Covert huwezi kumjua hata kama ni baba yako na hapa ndo unakutana na madeep spy nk...

Lakini watu walioharibu jina la Usalama wa Taifa ni hawa walioko chini ya kitengo cha CID(criminal investigation department) au hupenda kuitwa "IO" yani Intelligence officer. Hawa ndo mademu zao wanatamba mtaani kuwa mabwana zao ni usalama wa taifa, na hawa ndo wakilewa wanajitapa mtaani kuwa "unajua mi ni nani" hawa ndo mnaowaona wengi huko mtaani mkidhani ni usalama wa taifa.

Key rule ya usalama wa taifa ni kutoatract tension, na hapo ni somo pana sana kwao so ni ngumu sana aisee!!!
Hapo kama sijakuelewa mkuu! Unapozungumzia CID hao ni kitengo kipo ndani ya Polis ambao wanadeal na criminal investigation achana na hao pia kuna IO Hawa pia wapo ndani ya polis na ndani ya jwtz intelligence officers...

Mara nyingi hawa cid wao wanajulikana na wala hawajifichi maana hata wanapomhoji mtuhumiwa lazma wajitambulishe ...

Hawa Tiss Wa sasa wengi wao wameiharibu hii idara kutokana na kuingizwa kwenye kazi hyo pasipokufuata taratibu Bali wanaingizwa kwa utafiki na udugu, nilishawahi kukutana nao baadhi japo wao ni undercover lakn wako hovyo sana wanajionesha ovyo misifa mingi
 
Mwanamama Mmoja huko nchini Uingereza amempongeza sana Marehemu Mumewe hadi kumuita ' Shujaa ' hasa kwa Kitendo chake cha ' Kumficha ' kwa miaka 64 kuwa Yeye ( Mumewe ) alikuwa ni Mwana Usalama wa Taifa wa nchini Uingereza.
" Japo leo namzika Mume wangu na nilikuwa sijui muda wote kuwa ni mwana Usalama wa Taifa mpaka pale Wakubwa zake walipokuja hapa Msibani na Kunifahamisha hilo. Hata Wao wenyewe ( Mabosi zake ) walijua labda Mume wangu aliniambia kwakuwa nilikuwa Mkewe ila haikuwa hivyo na kiukweli japo Mume wangu amefariki ila kwa Kitendo chake cha Kunificha katika hili tena kwa miaka yake yote 64 aliyokuwa huko ( Usalama wa Taifa ) namuita ni Shujaa na kwakweli Idara ya Usalama wa Taifa ya Uingereza ilimpata Mtu mahiri, muhimu na Shujaa aliyeitendea vyema Kazi yake hiyo "
Je kwa Tanzania hili linawezekana? Je wana Usalama wa Taifa ( Eagle Wing House ) hasa hawa wa sasa achilia mbali wale ' Wastaafu ' wana uwezo na ' Ushujaa ' huu kama aliokuwa nao huyu Mwenzao kutoka nchini Uingereza kiasi kwamba wanaweza ' Kujificha ' si tu kwa Watu baki bali hata kwa Ndugu zao, Wake zao, Marafiki zao na Jamaa zao?
Nawasilisha.
Na wewe je, umeweza kumficha mkeo? Au wazazi wako?
 
Usalama Wa taifa Wa wingeleza ndio akina nani hao

Hivi huwa unaandika nini

Pumbavu na narudia tena Pumbavu kabisa. Najua ninalolifanya na nimewasilisha hii Mada kwa kutumia neno hilo la ' Usalama wa Taifa wa Uingereza ' ili kuleta ' dhania ' pana ya Kimjadala kwakuwa najaribu Kuhusianisha hili tukio lillofanywa na Mwana Usalama wa Uingereza nikijua ya kwamba hata hapa Tanzania pia wapo. Siku zingine ukijijua huna ' Akili ' halafu pia ni ' Mpumbavu Mwandamizi ' kama ulivyo Wewe na huyo aliyekupa ' Like ' hapo tracebongo usiwe unafungua ' threads ' zangu sawa? Pumbavu.
 
Back
Top Bottom