Kwa Tanzania hii ya sasa na hasa wale waliopo huko / humo ( Eagle Wing House ) hili la Uingereza linawezekana?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,528
Mwanamama Mmoja huko nchini Uingereza amempongeza sana Marehemu Mumewe hadi kumuita ' Shujaa ' hasa kwa Kitendo chake cha ' Kumficha ' kwa miaka 64 kuwa Yeye ( Mumewe ) alikuwa ni Mwana Usalama wa Taifa wa nchini Uingereza.

" Japo leo namzika Mume wangu na nilikuwa sijui muda wote kuwa ni mwana Usalama wa Taifa mpaka pale Wakubwa zake walipokuja hapa Msibani na Kunifahamisha hilo. Hata Wao wenyewe ( Mabosi zake ) walijua labda Mume wangu aliniambia kwakuwa nilikuwa Mkewe ila haikuwa hivyo na kiukweli japo Mume wangu amefariki ila kwa Kitendo chake cha Kunificha katika hili tena kwa miaka yake yote 64 aliyokuwa huko ( Usalama wa Taifa ) namuita ni Shujaa na kwakweli Idara ya Usalama wa Taifa ya Uingereza ilimpata Mtu mahiri, muhimu na Shujaa aliyeitendea vyema Kazi yake hiyo "

Je kwa Tanzania hili linawezekana? Je wana Usalama wa Taifa ( Eagle Wing House ) hasa hawa wa sasa achilia mbali wale ' Wastaafu ' wana uwezo na ' Ushujaa ' huu kama aliokuwa nao huyu Mwenzao kutoka nchini Uingereza kiasi kwamba wanaweza ' Kujificha ' si tu kwa Watu baki bali hata kwa Ndugu zao, Wake zao, Marafiki zao na Jamaa zao?

Nawasilisha.
 
Huko Eagle Wing house; kuna watu wa aina mbili tu ambao ni "COVERT NA OVERT" hawa overt ndio wenye shida hiyo unayoizungumzia sasa mana nao wamegawanyika kuna "Suveilensi na ripota" shida kubwa hasa ipo kwa hao ripota na lau kidogo suveilensi ambao wamo na transpota huwa ni ngumu kuwajua na wanaheshimu sana kazi zao kuliko maripota lakini pia maripota nao wamefanikiwa kujizuia japo si wote!!

Covert huwezi kumjua hata kama ni baba yako na hapa ndo unakutana na madeep spy nk...

Lakini watu walioharibu jina la Usalama wa Taifa ni hawa walioko chini ya kitengo cha CID(criminal investigation department) au hupenda kuitwa "IO" yani Intelligence officer. Hawa ndo mademu zao wanatamba mtaani kuwa mabwana zao ni usalama wa taifa, na hawa ndo wakilewa wanajitapa mtaani kuwa "unajua mi ni nani" hawa ndo mnaowaona wengi huko mtaani mkidhani ni usalama wa taifa.

Key rule ya usalama wa taifa ni kutoatract tension, na hapo ni somo pana sana kwao so ni ngumu sana aisee!!!
 
Nilipoteana na rafiki yangu tangu 1998. Siku nakutana nae by appearance tu ya kimavazi nikajua jamaa ni TISS. Nilipomuhoji anapofanyia kazi licha ya kunidanganya kwa ulimi lakini macho yake yalimsaliti. At the end he accented to the truth kuwa ni kitengo attached ktk ofisi fulani hivi. Mi nashauri TISS Mpotezee hizo suti zenu. Jichanganyeni na kila aina ya vazi. Plus msiwe serious mkiwa kitaa kiasi mnapoteza hata ile social interaction.
 
Huku kuwa huko ni sifa hivyo lazima watu mitaani wajue wewe ni nani.. Kwa wenzetu hiyo ni kazi nyeti yenye miiko yake kama kazi nyingine hivyo miiko ya kazi lazima izingatiwe.

Huku yanazingatiwa sana maslahi ya CCM hivyo lazima watoke hadharani kuitetea CCM, kwa wenzetu maslahi ya nchi kwanza hivyo wako serious kulinda maslahi ya nchi na si mtu, watu au kikundi cha watu.
 
Huko Eagle Wing house; kuna watu wa aina mbili tu ambao ni "COVERT NA OVERT" hawa overt ndio wenye shida hiyo unayoizungumzia sasa mana nao wamegawanyika kuna "Suveilensi na ripota" shida kubwa hasa ipo kwa hao ripota na lau kidogo suveilensi ambao wamo na transpota huwa ni ngumu kuwajua na wanaheshimu sana kazi zao kuliko maripota lakini pia maripota nao wamefanikiwa kujizuia japo si wote!!

Covert huwezi kumjua hata kama ni baba yako na hapa ndo unakutana na madeep spy nk...

Lakini watu walioharibu jina la Usalama wa Taifa ni hawa walioko chini ya kitengo cha CID(criminal investigation department) au hupenda kuitwa "IO" yani Intelligence officer. Hawa ndo mademu zao wanatamba mtaani kuwa mabwana zao ni usalama wa taifa, na hawa ndo wakilewa wanajitapa mtaani kuwa "unajua mi ni nani" hawa ndo mnaowaona wengi huko mtaani mkidhani ni usalama wa taifa.

Key rule ya usalama wa taifa ni kutoatract tension, na hapo ni somo pana sana kwao so ni ngumu sana aisee!!!
CID si polisi hao
 
Usalama jinsia ya kike ndo wanaweza, nlikua na swahiba wangu wakike, nmesoma nae chuo miaka mitatu, sijawahi kugundua ni usalama, mpaka tumemakiza chuo......mara tulipomaliza nashangaa anamlinda mke wa......
Noma sana
Hata yule big ambaye ni PSU wa Ngosha, miaka ile anasoma MALIMBE kitivo cha sheria hakuwahi kujisifu kabisa wala hatukumjua kabisaaa mpaka alipomaliza ndio tukaanza kumuona kwenye misafara ya wakubwa.
 
Bongo wachache ndio wanaweza ila wanaoingia kwasababu kufahamiana hao ndio unawakuta wakivimba kabisa mimi usalama .kuna bwana mmoja kaoa sister wakitaa baadae tukasikia yule bwana ni usalama huyo sister aliwachana rafiki zake nasisi wana tukajua .wapo ila wachache wanaweza tunza siri
 
Huku kuwa huko ni sifa hivyo lazima watu mitaani wajue wewe ni nani.. Kwa wenzetu hiyo ni kazi nyeti yenye miiko yake kama kazi nyingine hivyo miiko ya kazi lazima izingatiwe.

Huku yanazingatiwa sana maslahi ya CCM hivyo lazima watoke hadharani kuitetea CCM, kwa wenzetu maslahi ya nchi kwanza hivyo wako serious kulinda maslahi ya nchi na si mtu, watu au kikundi cha watu.

Mimi nina Kumbukumbu moja mpaka leo ninayo na sitoisahau ambapo katika ' harakati ' zangu za ' Ujana ' hasa wa Kupenda ' Ngono ' kuna Siku moja nilimbahatisha Mrembo Mmoja na kama kawaida Yetu Wanaume wengi ( hasa Sisi Apeche Alolo / Tusio na Hela ) huwa ni Mabingwa wa Kudanganya na Uwongo ambapo nilimuahidi Mrembo Vitu vikubwa wakati mfukoni mwangu tu nilikuwa hata Tsh 5,000/ sina na kama kawaida yao Wanawake zetu wa Kitanzania wakidanganywa ndiyo huamini nikaenda nae Ghettoni ' Kumchapa ' nao.

Nakumbuka wakati nikiwa nae huko Chumbani kama kawaida yangu ya kupenda ' Kuchokonoa / Kudadisi ' mambo nikaanza Kuzungumza na yule Mrembo ila alipoja kunishanganza kuna mahala tena akiwa mkavu kabisa wala hakuwa na Uwoga katika mazungumzo yetu akanisema kuwa Mumewe yupo Usalama na kuonyesha kuwa alikuwa anamaanisha na yupo ' serious ' kabisa akasema kuwa Mumewe huyo alishawahi hadi Kumtolea Vitambulisho vyao na kwamba hata Silaha yake huwa anaiona na anajua anapoiweka akiwa nae Kwao.

Baada ya kuniambia huo ' Upopoma ' wake hapo hapo hata hamu ya Kuendelea ' Kutifuana ' nae ' Kibaiolojia ' ikaniishia kwani nikajiona kabisa kwamba Kwanza GENTAMYCINE nimetua mahala pabaya na ' Hatarishi ' ambapo muda wowote ujao Jina langu lingebadilika kutoka Kuitwa Ndugu na lingekuwa Marehemu na kubwa zaidi nilishtuka na kuogopa mno huku nikijiuliza ni kwanini Mumewe alifikia hatua hadi ya ' Kufunguka ' kiasi kile Kwake huyu Mrembo niliyekuwa nae?

Kazi ipo!
 
CID si polisi hao
Ndio ni polisi ila ndo wale tunaowaita askari kanzu, yani nao huwa hawafahamiki kwa kuwa wanavaa kiraia sana na mara nyingi tupo nao kitaa, sasa aina yao ya kazi ndio imefanya watu wengi tushindwe kuelewa usalama wanafanyaje kazi na ni nini miiko yao. Hawa IO wanaact tabia za UT hivyo si ajabu ukutane na mtu akwambie yule ni UT kumbe ni IO.

Tuwaheshimu UT, hawajawa wajinga kiasi hicho
 
Hata yule big ambaye ni PSU wa Ngosha, miaka ile anasoma MALIMBE kitivo cha sheria hakuwahi kujisifu kabisa wala hatukumjua kabisaaa mpaka alipomaliza ndio tukaanza kumuona kwenye misafara ya wakubwa.

Basi ilikuwa ni bahati Kwako ila kwa Sisi tunaozunguka zunguka Mitaani huku na kule tunakutana na makubwa Mkuu kwani hata kabla hujauliza wengine wanakuambia tu wenyewe. Na ukitaka uwachokoze ili wajitambulishe wenyewe gombea nao Mademu au Mdhulumu tu hata Mmoja wao ndipo utashangaa kama si kustaajabu kabisa.
 
Hahaha pole sana

Ukiona hadi Watoto wako au Wanafamilia wako wanakujua kabisa kuwa Wewe ni mwana ' Eagle Wing House ' wa Tanzania basi ujue kuwa hapo hakuna Kitu na ni ' hatari ' tupu si tu Kwake bali hadi katika Idara. Nimeileta hapa hii taarifa ya huyu Mama wa huko Uingereza ili kama kuna cha Kujifunza basi Wahusika na wengineo pia tuweze kujua ' Miiko ' ya Kutukuka na Mitakatifu ya hiyo Tasnia muhimu na nyeti katika nchi yoyote ile hapa Ulimwenguni.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom