Kwa Tanzania hii ya sasa na hasa wale waliopo huko / humo ( Eagle Wing House ) hili la Uingereza linawezekana?

Kila Mtu akifanya majukumu kwa Mahadili sehemu ya kazi yake tutafika mbali sana.

Naamanisha kujua wajibu wa Kazi yako na Wajibu wako kama mfanya kazi, iwe kwa sehemu yoyote ile Mahadili ni kitu muhimu.

Mkuu ni Maadili na siyo Mahadili kama ulivyoandika Wewe tafadhali. Tukipende sana Kiswahili chetu na tukienzi mno pia.
 
Nimewahi sana kujiuliza ile sura niliiona wapi, jamaa alikua anahudhuria sana kwenye kile kibanda umiza cha nyamalango na alikua mbishi sana kwenye mechi ila kiujumla he's good people..

Ulivyotaja tu hilo eneo la Nyamalango umenifanya nikumbuke jinsi Mademu wengi wa hilo eneo hasa wale ' Wanazengo ' walivyo na Gono na Kaswende sana.
 
Uingereza wana idara kuu mbili maarufu. Idara ya Ujasusi wa kimataifa a.k.a Military Intelligence 6 (MI6) ama Secret Intelligence Service (SIS) kama inavyojulikana kileo. Pia wana idara ya Ujasusi wa ndani iitwayo MI5. Hio ni kama ilivyo FBI kwa Marekani na SHINIBET kwa Israeli. Na pia ni sawa na ilivyokuwepo Second Chief Directorate ya zamani za KGB. Huku MOSSAD ya Ujasusi wa nje ya Israeli ilivyo CIA kwa Marekani. Ntashukuru nikisahihishwa.

Ulichokiandika hapa kinahusiana vipi na ' Hoja ' iliyoko mezani? Waswahili bhana!!!!!! Kwahiyo umeambiwa kuwa Sisi wengine wote hatuyajui haya ' uliyoyatapika ' hapa wakati hata uki ' Google ' tu unayapata yote na kama haitoshi wengine hadi tuna Vitabu vyao vingi vya hayo mambo kutoka Idara / Taasisi mbalimbali za duniani? Siku zingine jitahidi uwe unajikita hasa kata Mada husika na epuka kuwa ' Out of Context ' sawa?
 
Hapo kama sijakuelewa mkuu! Unapozungumzia CID hao ni kitengo kipo ndani ya Polis ambao wanadeal na criminal investigation achana na hao pia kuna IO Hawa pia wapo ndani ya polis na ndani ya jwtz intelligence officers...

Mara nyingi hawa cid wao wanajulikana na wala hawajifichi maana hata wanapomhoji mtuhumiwa lazma wajitambulishe ...

Hawa Tiss Wa sasa wengi wao wameiharibu hii idara kutokana na kuingizwa kwenye kazi hyo pasipokufuata taratibu Bali wanaingizwa kwa utafiki na udugu, nilishawahi kukutana nao baadhi japo wao ni undercover lakn wako hovyo sana wanajionesha ovyo misifa mingi
Hapo sijazungumzia IO walioko chini ya MI. Nimezungumzia IO walioko chini ya kitengo cha CID; achana na wale wanaopelekewa kesi wakiwa wamekaa. Nazungmzia wale askari kanzu ambao wapo kama ma infomer kwa OC CID na pia vitu deep mtaani huhusika navyo moja kwa moja kisha huripoti kwa OCD, OCS, RPC au mhusika katika hilo jambo!!

Ni ngumu kufahamika mana wanaact kama UT!! Na wana kazi kama UT ila wao wana dili ndani ya nchi.

Labda sijui kuelewesha ila kama umenilewa basi inabidi tuangalie upya lawama zetu kwa UT
 
Kuna open na closed.. hao unaowaona wewe ni open..!!..closed utaishia kuwahisi tuu... ku'unlock cover yake mpaka uwe sehemu yao..
Nilipoteana na rafiki yangu tangu 1998. Siku nakutana nae by appearance tu ya kimavazi nikajua jamaa ni TISS. Nilipomuhoji anapofanyia kazi licha ya kunidanganya kwa ulimi lakini macho yake yalimsaliti. At the end he accented to the truth kuwa ni kitengo attached ktk ofisi fulani hivi. Mi nashauri TISS Mpotezee hizo suti zenu. Jichanganyeni na kila aina ya vazi. Plus msiwe serious mkiwa kitaa kiasi mnapoteza hata ile social interaction.
 
Na siku ile mjomba jiwe alivyomtambulisha spymaster mbele ya kadamnasi.. dhamira ilikuwa ni nini..??..maana hii sijawahi kuonaga duniani spymaster kuanikwa..
Haijatosha akamu'unlock na boss wa pccb mchana kweupe........inakuwaje ????
 
Na siku ile mjomba jiwe alivyomtambulisha spymaster mbele ya kadamnasi.. dhamira ilikuwa ni nini..??..maana hii sijawahi kuonaga duniani spymaster kuanikwa..
Haijatosha akamu'unlock na boss wa pccb mchana kweupe........inakuwaje ????

Bahati mbaya Idara / Taasisi haina Msemaji wake / wao hivyo sijui hili Swali lako unataka lijibiwe na nani hapa Mkuu.
 
Back
Top Bottom