Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,604
- 5,581
MKUU wa kundi la waangalizi wa Umoja wa Ulaya, David Martin, jana ametoa taarifa yake ya awali kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu ulivyokwenda visiwani Zanzibar. Wakati huo huo Kamati ya waangalizi wa uchaguzi Tanzania TEMCO, nayo pia imetoa ripoti juu ya uchaguzi huo.
Katika taarifa yake kuhusu uchaguzi, mkuu wa waangalizi wa Umioja wa Ulaya David Martin, alisema kwa ujumla uchaguzi ulifanyika katika hali ya amani na utulivu, lakini akataja dosari zilizotokeza na ambazo zinatia wasiwasi katika mchakato mzima.
Alisema kuharibika kwa zaidi ya kura 10,000 (kama ni kweli hapo)ni moja wapo ya shaka hizo ambapo inaonesha kwamba elimu ya uraia ilikosekana na ndio sababu kubwa ya wananchi wengi kuharibu kura zao bila ya kujua.
Hali kadhalika alitaja juu ya kasoro zilizojitokeza katika upande wa utoaji nafasi katika vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali kwa kuwa vimejiegemeza na kukibeba chama tawala cha CCM ambapo kimepewa nafasi kubwa mno na vile vya upinzani kuekewa vikwazo katika kutolewa taarifa zao.
Aidha kuhusu Tume alieleza kwamba, kulikuweko na uwazi lakini anasikitika na kukataliwa kwa wawakilishi wa vyama vya kisiasa na waangalizi wa ndani na wa kimataifa kuingia katika ukumbi wa kujumuisha matokeo ya kura na hivyo zoezi hilo kufanywa bila ya kushuhudiwa na waangalizi ambapo ni kinyume na makubaliano waliokubaliana. Mkuu huyo wa waangalizi alisema serikali na Tume ilishindwa kutekeleza ahadi nyingi zilizotolewa kabla ya waangalizi hao kufika nchini na akasisitiza kwamba litakua jambo la busara kuhakikisha mambo kama hayo yanarekebishwa katika uchaguzi wa siku zijazo. Na kupendekeza kuruhusiwa kuwepo kwa wagombea wakujitegemea, akiitaja kuwa ni haki ya kila raia.
Kutolewa kwa ripoti ya Umoja wa Ulaya hii leo ni hatua ya kwanza na ya awali kabla ya kutolewa ripoti kamili baadae mwezi huu. Wakati huo huo Kamati ya waangalizi wa uchaguzi Tanzania (TEMCO) nayo imetoa ripoti yake Zanzibar kuhusu uchaguzi huo na ikipongeza utulivu na amani ulioshuhudiwa wakati wa kampeni na siku ya uchaguzi, pamoja na hayo ilitaja juu ya dosari kadhaa upande wa mawakala wa tume na pia kunyimwa kwa chama cha upinzani nafasi ya kufanya mkutano katika jimbo la Donge.
Mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha dare s salaam, Bashiru Ali aliwaambia waandishi wa habari katika ukumbi wa Eacrotanal kwamba ameshangazwa kuwa Tume ilishindwa kuchukua hatua yoyote wakati chama cha CUF kuilipokataliwa kufanya mkutano wake katika jimbo la Donge na akawasifu viongozi wa CUF kwa kuwashawishi wanachama wao na kuepusha shari.
"Nilikuwepo katika mkutano uliofanyiak Jangombe Maalim Seif na Jussa walitumia nusu saa nzima kuwashawishi wanachama wao waachane na mkutano wa Donge, hata hivyo vyombo vya ulinzi na usalama vilikwenda kule Donge kuweka ulinzi vikidhani CUF watakwenda kwa nguvu…kwa kweli kuna tatizo kubwa katika utoaji wa viwanja vya kufanyia kampeni hata kama hili halijalalmikiwa lakini tatizo hilo lipo…" alisema Mratibu huyo wa TEMCO.
Nadhani picha imepatikana hapo
Nimeanza kumpa ushahidi yule ndugu yangu anaesema WACHAKACHUAJI HAWACHAKACHUI:sad: