Kwa suala hili BAKWATA hamjatenda haki

Kwa suala hili BAKWATA hamjatenda haki

Ertugrul Bey

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
13,191
Reaction score
26,339
Utangulizi:

Uislamu unasema hivi "ukiona uovu basi kwanza uondoe kwa mikono yako,ukishindwa kwa kauli na ukishindwa kabisa basi kwa kuchukia moyoni mwako,na huu ndio udhaifu wa imani" kwa maana yule anayechukia jambo moyoni mwake ni mdhaifu wa imani,kwasababu option ya kwanza na ya pili ndio best zaidi

Lakini hata huyu anayechukia moyoni ni bora kuliko yule ambaye anaona uovu unatendeka kisha hata asichukie moyoni mwake

Twende kazi....

Kwanza niseme wazi mimi nitakuwa kwenye haki siku zote,hata dini yangu inasisitiza juu ya haki hata kwa asie muislamu,ndio maana hata kwenye kutoa ushahidi unatakiwa useme haki,hata kama ndugu yako ana kesi na asiye muislamu basi toa ushahidi wa haki hata kama utakuwa ushahidi huo unakuwa dhidi ya ndugu yangu,kwani huo ndio uadilifu mbele ya Allah

Kwa yale yaliyo tokea 29 Oct 2025 ilikuwa ni uovu dhidi ya uhai wa binadamu,nieleweke vizur hapa,sibadilishi msimamo wangu kwamba yale hayakuwa maandamano ni fujo na vurugu,ni kweli hayakuwa maandamano bali ni fujo na vurugu

Lakini haikuwa sawa kwa Serikali kutumia nguvu kubwa kutuliza fujo na vurugu zile na kupelekea watu wengi kupoteza maisha yao,ile nguvu haikuwa sahihi kutumika kwa watu ambao hawakuwa na silaha za moto

Sasa Bakwata kama taasisi ya kidini ilipaswa kukemea Vikali kile kilichotokea 29 Oct 2025,kwanza kwakuwa ni jambo la dini ya kiislamu linavyoelekeza pindi uonapo uovu basi uondoe kwa namna tatu,mosi uondoe kwa mikono yako,au uondoe kwa kauli yako au ukishindwa kabisa basi uchukie moyoni mwako

Najua njia ya kwanza Bakwata hamkuwa nayo,lakini njia ya pili mlikuwa nayo,hapa mlipaswa kukemea vikali mauaji yale kwa nguvu kubwa kwakuwa hilo ni jambo muhimu la kufanya kwanza kijamii,lakini pili ni kidini kama Uislamu unavyoelekeza.

Kwa hapa Bakwata hamna la kujitetea,mimi ni muislamu kwahiyo natenda haki kwa kusema ukweli kwamba hapa mmekosea,wasomaji wangu mnaweza sema mbona hujalisema hili zamani,mjue kwamba kila jambo lina wakati wake, nikiwa kama ERTUGRUL BEY basi ni wakati wangu wa kulizungumzia hili.

Lakini muongozo wa kiislamu unasema kwamba akikujieni mzushi yoyote na habari yoyote basi muichunguzeni kwanza na kujua ukweli wake ili msije kuwadhuru watu bure, kwa kutambua hili kuna habari nimeisoma humu mtandaoni kwamba Waislamu waliahidiwa kwamba kero zao ambazo zimekuwa hazijatatuliwa miaka nenda rudi basi zingepatikana katika awamu hii.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa huenda ndio ilikuwa sababu ya Waislamu kumuunga mkono Mama Samia na huenda ikapelekea kutokemea hayo yaliyo tokea,mtoa taarifa ni mtu ambaye siwezi kumuweka kwenye hadhi ya mzushi kwakuwa amejijengea heshima kubwa humu kwa kuleta hoja mbali mbali ambazo zina mashiko,lakini pamoja na hayo bado itabakia ni taarifa ambayo haijathibitishwa kwa asilimia Mia moja.

Mimi ERTUGRUL BEY nasema hivi endapo hii taarifa ni ya kweli basi hapa Bakwata mtakuwa mmepuyanga vibaya sana,kwasababu mtakuwa hamjatenda haki kwa mujibu wa miongozo ya dini yetu. Naomba hii taarifa isiwe ni kweli.

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
 
Back
Top Bottom