Kwa style hii kila mtu ale urefu wa kamba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa style hii kila mtu ale urefu wa kamba yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hittler, Aug 23, 2011.

 1. h

  hittler Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mfumo wa uongozi wa Tanzania kwa sasa nashauri kila mtu ale urefu wa kamba yake, kwasababu wote wanaotuhumiwa kwa rushwa wanasafishwa na serikal. Ni bora serikali ikahalalisha rushwa katika sehemu za kazi ili tujue moja, tumechoka kusubiri uchunguzi wa CAG ambao haujawahi kutoa ukweli
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Zama hizi mtumishi wa umma anajengewa nyumba ya kuishi ya thamani ya mabilioni ya shilingi na
  akikaribia kustaafu anakopeshwa kwa vimilioni vichache, pia ni zama ambazo kufikishwa mahakamani
  kwa ubadhirifu inategemea umekwapua kiasi gani, kama ni kikubwa, dola yenyewe inatamka kuwa hukamatiki!

  Ni zama ambazo ukiwa mtumishi wa umma mwenye cheo kikubwa unaweza kusomesha mwanao nchi yoyote
  uitakayo bila mawazo ya karo, si hivyo tu kutibiwa nje si kwa magonjwa ya moyo tu bali hata mafua,
  muhimu cheo kizuri cha kuhudumia umma.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwani kuna uongozi tena tanzania hii
  si wapo watu tuu walioshikilia nafasi wanajiita viongozi
  Kwani tungekuwa na uongozi haya madudu yangekuwa yanaonekana
  Ahhhh inatia hasira sana
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  ukipata chance iba,usibakishe hata shilingi mpaka akili itukae sawa kama libya,tunisia,yemen(rais alipigwa bomu..duh!!),misri na kwingineko
   
 5. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mkuu, naomba nifute kauli yangu, tuna watawala na si viongozi
  ndiyo maana nchini kuna tume ya Utawala Bora na si Uongozi Bora...
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Ushauri mzuri sana!
   
 7. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Mh, vizazi vyetu watakuja kujitafutia wenyewe siyo?
  Ama kweli ukistaajabu ya Mussa...
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  kabisa mkuu
  ni watawala na sio viongozi
  na wako pale kwa ajili ya maslahi yao binafsi na kujijenga sio maslahi ya watawaliwa
  tumefikia mahali watu hawana imani na watawala hawa maana kila wakiamka asubuhi ndo madudu wanayoyafanya yanazidi ya jana yake
   
 9. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Watoto na wajukuu wetu watajuta kuzaliwa Tanzania...
   
 10. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sasa tena kama haya ya mnadhimu wa jeshi ni ya kweli basi kila mtu atakula kwa urefu wa kamab yake! Huyu Bregadia Abrahamani Shimbo kuna tetesi amekamatwa na interpol kwa kuwa na akaunt huku South Africa yenye tshs Trilioni 3!!!!! Jamani yan kama ni kweli zichukuliwe zijenge miundombinu ya umeme hapa nchini. Yani anamiliki robo ya budget ya taifa la Tanzania. Duu! Kweli hata ukipata chance iba bwana
   
 11. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Aibu kubwa sana kwa taasisi za serikali kama CAG office, TAKUKURU, POLICE, TISS zote zipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya wezi. Jibu ni moja tu nao ni MAJIZI wakubwa laana wanatoka nayo
   
 12. W

  We know next JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tutakuja laumiwa na vizazi vijavyo kuwa tulikuwa wapi kufanya maamuzi magumu ya kubadilisha hali hii ya utawala wa Kifisadi?
   
 13. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi hata mashirika manne yaliyotoe hizo fedha cag alivyosema,je huyo ndio utaratibu?na bajeti ya hizo fedha ilikuwepo?waliopelekea ili kupitisha au kuandaa bajeji ofsini kwao hakuchukua fedha za kujikimu na posho?tumekwisha huku tunajiona jamani.
   
 14. s

  samkyjoseph New Member

  #14
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TZ bila ufisadi haiwezekani! Nijambo la ajabu kumsikia katibu mkuu akise Jayro anatakiwa arudi kazin eti kwasababu tu kiasi alicho iba nikidodogo tafauti nailivyo daiwa hivyo haitoshi kumtia hatiani.......? je vipi kuhusu usemiwetu kuwa aliye kamatwa na ngozi ndiye mwiz wa mbuzi?
   
 15. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
   
Loading...