Kwa Shibuda, Hata CHADEMA Hakuna kivuli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Shibuda, Hata CHADEMA Hakuna kivuli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 15, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  MAGAZETI, Redio na Runinga zimeripoti, jana na leo; Freeman Mbowe amemtosa John Shibuda kwenye Baraza Kivuli la Mawaziri.

  Tafsiri yangu, Mzee John Shibuda, Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya CHADEMA ( CCM?) hana wakati mzuri ndani ya CHADEMA. Kule ' kwao' kwa asili CCM alifanyiwa fitna. Jina lake likaenguliwa kwenye kura za maoni.

  Na Mzee wa watu alikuwa juu kwenye kura za maoni. Lakin,i CCM tunawajua, wakafanya ' Vitu vyao!' Wakamnyima kivuli cha kisiasa. Shibuda, Msukuma anayewazidi Wasukuma wote kwa Kiswahili fasaha akaachwa na chama chake aungue juani!

  Masikini Mzee Shibuda, kada mahiri asiyekana wala kuidharau asili yake kiitikadi, alichanganyikiwa. Akakata shauri kuvuka bahari. Akaenda Unguja kuomba ushauri kwa watani zake, Waswahili wa Unguja. Msukuma wa watu akarudi bara.

  Breki ya kwanza ikawa Kinondoni, Makao Makuu ya CHADEMA- Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo. Na jana akaambiwa laivu- Hata CHADEMA hakuna kivuli!

  Mwenyekiti Mbowe amem-freeze Shibuda. Inasemwa magazetini, kuwa Shibuda ameonekana kuwa na mitazamo tofauti dhidi ya chama chake cha sasa. ( Mwananchi, Februari 15, 2011)

  Na ugomvi si ulianzia tangu Bagamoyo, au? Iliandikwa wakati ule, kuwa kulikuwa na kushikana mashati kati ya Kijana Ezekiel Wenje na Mzee John Shibuda. Kijana Wenje alimshutumu Mzee wake kwa uroho wa minofu! Ndio maana, wakati wenzake wamesusa, yeye akavaa shati lake jeupe na kwenda Ikulu ya Chamwino; kula nyama, kunywa na kucheza mduara kwenye sherehe ya Jakaya, Rais wa nchi.

  Waandishi wakamfuata Shibuda kumwuliza kulikoni kushikana mashati na Wenje. Tukamsikia Mzee Shibuda akitamka; Nitakwenda kumshtaki Wenje kwa Wazee wa Mwanza!

  Hata pale kuna tulioingiwa mashaka; hivi CHADEMA hakuna Wazee?

  Na leo imeripotiwa, kuwa vijana wa CHADEMA vyuo vikuu mkoani Dodoma wamepanga leo waende ofisi za Bunge kumzuia Mzee Shibuda asiingie Bungeni, kisa? Msaliti!

  Si Shibuda alitamka juma la jana pale Bungeni, kuwa vijana wa sasa wanahitaji mwongozo mzuri zaidi wa malezi na kwamba yeye atabaki na maadili aliyojifunza ndani ya CCM. Na hakuwa mchoyo, Mzee Shibuda akasema atayapeleka CHADEMA!

  Hapo ndipo alipokosea mtani wangu, Msukuma wa watu Shibuda, Ya CCM kuyapeleka CHADEMA! Vijana wa CHADEMA wamemjia juu kama moshi wa kifuu. Wanasema; " Yeye anataka kuleta malezi aliyoyapata CCM alete CHADEMA, malezi ya CCM ayalete CHADEMA! Hapa hatutaki na sisi tutaandama Jumanne ( leo) kwenda kumzuia Shibuda asiingie Bungeni". Alitamka kijana Toju, Mwenyekiti wa tawi la Miyuji, Dodoma.

  Wabunge Lema na Mdee walikuwapo . Lema akatamka, kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wa viongozi wa chama chao. Mdee akasema hakuna haja ya kumfutilia mbunge huyo ( Shibuda). Kama hukumu atahukumiwa na jamii husika. ( Mwananchi, Februari, 15, 2011).

  Yote haya yanaacha maswali. Moja nalojiuliza, hivi kwanini vyama vyetu vya siasa vinapata tabu sana kumvumilia mwanachama mwenye fikra au mtazamo tofauti na wezake. Kwa nini muono tofauti uwe sawa na usaliti? Tumeyaona ndani ya CCM, na sasa CHADEMA.

  Nini kifanyike kuimarisha Intra- Party Democracy ndani ya vyama vyetu hivi? Nimechokoza mjadala.


  Maggid
  Iringa,
  Februari 15, 2011
   
 2. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  nadhani nikubaliane na maggid kuwa chadema kwa kutomfukuza uanachama wamemvumilia vya kutosha. lakini hili la kumpa uwaziri hapana! why tayari msimamo wake unajulikana kutekeleza maadili ya ccm, msimamo wa chadema ni kuiondoa ccm madarakani, wakati shibuda ni kuendeleza maadili ya ccm ili idumu
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe ni Mnzanzibari nini.Kiswahili hicho,mm..wewe acha tu.All in all, kwa mtizamo wangu mimi, hatua aliyochukuwa Mbowe dhidi ya Shibuda ni sahihi kabisa.Tabia ya Shibuda ya undumi la kuwili haikubaliki kabisa.Huyu bwana ni CCM dam dam.
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Maggid,

  Mawazo tofauti ndani ya chama, hususan CDM, si vibaya!! LAKINI mtu anapaswa kwanza kutafakali ni jambo gani/wazo gani? unalitoa/unayatoa wapi? tena wakati gani? unayatoa kwa namna gani?? na mbele ya nani/au katika muktadha (context) gani? Hapo ndo Mhe. Shibuda na Mhe. mwingine yeyote anapaswa kufikiri sana kabla ya kusema jambo hususan katika chama kama CDM ambacho kinapigania dola katikati ya wachawi wengi!! vinginevyo ni kujibomoa na wanachama hawawezi kukubali kurudishwa nyuma tena! "We have come so far"
   
 5. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mimi sioni tatizo la Shibuda kunyimwa uwaziri kivuli. CDM inao wabunge 20 waliokosa uwaziri kivuli, na wamekosa kwa kuwa lengo ilikuwa ni kumuonyesha Mkwere kuwa baraza dogo la mawaziri 29 linawezekana na sio kupeana tu vyeo kama kuwapa akina Sofia Simba na Hawa Ghasia. Waache mawaziri kivuli wachape kazi na kwa kuanzia Mnyika aliwakilisha vizuri sana leo kwenye Jambo TBC1.
   
 6. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160

  Maggid,
  Naomba kwa kuweka rekodi sawa: Shibuda alishindwa (hakuenguliwa) kwenye kura za maoni na Ndg Robert Kisena ingawa kuna madai kwamba rushwa ilitumika kwa kiwango cha juu sana hasa ukizingatia hakuwa chaguo la Chama Mkoa hata Taifa.

  Tukirudi kwenye mjadala wa Intra-Party Democracy nadhani ni mjadala mpana kwa sababu bado hatujaelewa hata demokrasia yenyewe nini.
  Wapo wanaosema sauti ya wengi ndio democrasia na sio kuwasilikiza wachache.
  Wengine wanaamini democrasia ni uhuru wa kusema chochote tu bila kujali kina madhara gani kwa wengine. Mtu anayeadhibiwa au kukosa uongozi kwenye chama anakihama huku akisema hakuna demokrasia ndani ya chama ila akipandishwa cheo ndani ya chama ndo demokrasia (hapa namkumbuka M/kiti wa BAWACHA).

  Kwa mtazamo wangu mfumo unaotawala siasa zetu ni kitu tofauti kabisa na kinachoitwa demokrasia kama ambavyo nyumbani kwako Majid au kwangu kusivyo na demokrasia - iite Intra-Family Democracy.

  SHIBUDA CITATION
  Kwa mtazamo wangu si sahihi waandishi kusema "Shibuda atoswa" au "Mbowe ammwaga Shibuda".
  Kwa nini waandishi wanataka ionekane kwamba ilikuwa ni lazima Shibuda kuwa waziri kivuli?? Kabla hajahamia Chadema hakupata kuwa waziri hivyo nafasi yake ilikuwa sawa na wabunge wengine wa upinzani.
  Uzoefu wa kuwa Bungeni haumaanishi anakuwa bora kuliko wageni kama Mnyika au Lisu.

  Kwa silka Shibuda ni mwongeaji na ni vema watu wakamkubali kwa namna alivyo bila kuongeza tafsiri kwamba ni mamluki.
  Inawezekana kweli kwamba Chadema wana namna yao ya kuendesha mambo lakini ukisilimu haimanishi kwamba tayari utaijua Quran yote. Kinachotakiwa ni kutambua haiba zetu ili itupe nafasi ya kufanya kazi pamoja au kurekebishana.

  Mimi bado sioni kwa nini watu wadhani Shibuda hana kivuli Chadema kwa vile tu alipishana na Wenje au Toju (M/kiti wa Tawi Vs Mbunge??). Kwa upande mwingine sioni kama kuna tatizo kwenye majibu ya Lema au Mdee (kama hivyo ndivyo walisema).

  Kwa msingi wa hoja hii,
  Je tutumie mabishano ya Shibuda na Wenje kama kigezo cha lack of Intra-Party Democracy?
  Kwa Shibuda kukosa uwaziri-kivuli ni dalili ya kukosekana kwa Intra-Party Democracy??
  Lakini pia Demokrasia ni nini kabla hatujadadavua demokrasia ndani ya Vhama???
   
 7. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Shibuda akili na moyo wake bado uko ccm si mpinzani ila mtu ambaye ana maintain status yake ya Ubunge iliyoharibiwa na ccm anayoipenda sana maisha yake yote. Kwa hiyo ni kumuangalia na kumvumilia tu manake siku nazo zinamtupa mkono
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mjengwa unaweza kutolea mfano kwa uliyoyaona CCM na sasa yanatokea Chadema? Tungeshukuru ungeleta kitu halisi na kutaja wale walivyofanya ccm na uweze kutoa ulinganifu huo. Ni vizuri tukapata evedence. Utakuwa umetusaidia sana kujenga uelewa wetu.
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Hivi mkuu aka si uchochezi ni nini? Kwani mliambiwa anaingia chadema apate uwaziri kivuli? Na je wabunge wa chadema ni wangapi? na je ni waote walipaswa kuwa mawaziri vivuli? Ni kitu gani cha ziada alichonacho ambacho wabunge wengine wa chadema waloachwa hawana?

  Acheni uchochezi na kulifanya jambo hili ni kuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuubwa wakati hakuna kitu. Tatizo la waandishi makanjanja wa bongo ni kutengeneza titles za magazeti ili wauze badala ya kufuata weledi wa uandishi!
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  Mkuu Maggid,

  Mawazo mbadala kwa chama na yanayojenga chama na nchi ni yale yenye maslahi kwa taifa, unapojiunga na chama lazima ujue falsafa yao na misimamo yao ili uone kama ndio kunako kufaa kufikia malengo.

  Kama chama kinachukia ufisadi lakini kiunga mkono mafisadi ukiwa na mawazo mbadala hayo ndio hata wananchi watakuunga mkono. Lakini unajiunga na chama ukijua mlengwa wake ambao hata wananchi weng wanaunga mkono alafu ukafanya maamuzi ambayo yataleta picha mbovu kimshikamano ktk chama na ukijua kabisa hayo maamuzi yatapunguza ari ya wananchi kuzidi kukikataa chama tawala ambacho moja ya ajenda muhimu ni kukitoa madarakani ili kuleta mifumo na mwelekeo mpya wa nchi.

  Huyo ni msaliti wa ajenda za chama na hafai, demokrasia chamani sio kubwabwaja ovyo popote bali ni kufata utaratibu na ukishindwa ondoka. Hiyo demokrasia dunia nzima haipo na mwenye ushaidi atoe hapa jamvini.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ulibhudogo shi?
   
 12. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  CHADEMA washamshutikia Shibuda kuwa ni mercenary aka mamluki kama wewe unavyoji "shibudadua" kwenye masuala, au siyo?
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Umenena.

  Kwa mtaji huohuo JMK amewatosa Wabunge wa majimbo mangapi Tanzanaia.

  Mbona Ja People Mbunge wa Njombe Kaskazini na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa hajapata uWaziri naye Katoswa na Mkwere??

  Ili asiwatose Wabunge wa CCM Mkwere alitakiwa kuwa na Mawaziri sawa na idadi ya Wabunge wa CCM??

  Mbona waandishi NYUGU na FAKE wa Habari Tanzania hawalioni hilo???

   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwani ni lazima Shibuda kuwa waziri kivuli? Hawa waandishi vipi!!
   
 15. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Maana ya Chama cha kisiasa ni mkusanyiko wa watu wanaofuata mtazamo mmoja na wenye fikra zisizokinzana.
  Tatizo la CHADEMA lilikuwa kunyonya kila anaetoka sisiemu bila ya kupimwa itikadi yake, na hilo ndilo linalodumaza upinzani wa Tanzania.

  Kuna watu kama Shibunda wanaenda Bungeni iliwaendelee kujineemesha (kwa mishahara minono na posho lukuki) pasina kujali maisha ya wananchi waliowateua.

  Kwa ufupi Mr. Shibuda ni CCM kwanza na baadae CHADEMA, simulaumu sana yeye binafsi kwani chanzo ni mfumo mzima uliomkuza na kumtunza mpaka aliposasa hivi, na hii ni kansa tuliokuwa nayo wengi wetu waTZ, tunalaumu mlango wa sebuleni na kupuliza mlango wa jikoni.
   
 16. M

  MLEKWA Senior Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwenye siasa kuna michezo na lazima ujue kuicheza kulingana na wakati pia shibuda namsifu kuwa ni mchezaji mzuri kama Raila Odinga kwani anaona zile nyakati za kisiasa.

  Shibuda ni mtaji wa Chadema kwani hawa vijana wanaoleta jeuri hawajui thamani ya shibuda NA Kama wanaijua wawaulize CCM kwani wanamuomba na kumuangukia kwa kura alizowatia hasara huko usukumani na ukingalia mchango wa Shibuda katika uchaguzi uliopita kwa Chadema I feel terrible bad to treat this man who contribute his energy and time to make chadema popular huko Usukumani na kuwaangusha vigogo kama MASHA.

  Tatizo la Chadema ni chama kilichokosa wazee wa Busara na kuwa na ideology ya vijana watupu na hii ni hasara kubwa kwa chama hichi. Wanachadema mukapenda musipende lazima kama munataka ku grow and kuvuna matunda mukubali milima na mabonde hakuna safari ya mteremko tu. Shibuda hayuko Keko kule Gerezani na anajua anachokiongea , ni yale yale yaliomkuta Zitto ndio hao wanaoitwa wasaliti wachache ila Chadema kama inaona kidole cha ncha hata ukikosa huna hasara basi wasubiri hichi kidole cha ncha kipotee watajua umuhimu wa kidole hichi cha ncha.

  Waulize CCM walipomfukuza Hamad kule Zanzibar kidole hichi cha ncha walikiona thamani yake na kujaribu kukirudisha kwa surgery kwan i waliona chawa habanjiki kwa kidole kimoja.

  Ikiwa leo munatanua Usukumani na kuunda mabaraza ya miji kama CUF wanvyotamba Pemba halafu munamtukana mzee wa Watu naona munaelekea mrengo usioeleweka.
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Great thinker!!! makofi, paa paa paa...
   
 18. m

  matawi JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kama mnabeba jiwe la kilo 100 mko watu 6 unajisikiaje moja akiliachia mkabaki 5, unajisikiaje tena akipungua 1 mkabaki 4? ndivyo chadema inavyomwona Shibuda kutotoa ushirikiano katika mapinduzi ya nchi hii kupitia chadema
   
 19. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Upo kwenye safari ya kufika mahali fulani, unapata ufunuo kuwa njia mnayoipitia haiwafikishi huko mapotaka kwenda. lakini upande wa pili unaona kundi jingine linaelekea huko huko ambako kundi uliopo lianaelekea lakini kwa kupitia njia nyingine. Na njia hiyo unaamini ni iko kwenye dira sahihi. Je utafanya nini? Mimi nadhani, ili kuridhisha utashi wa nafsi yako, itakubidi uondoke kwenye kundi hilo na uende ujiunge na kundi la ng'ambo nyingine ambalo unaamini linaloelekea ndiko sahihi. Ukifika huko, itabidi uongozane nao hasa kwa sababu hao wana dira na maono sahihi yanayolingana na yako katika safari hii. Lakini ukifika na kuanza kuleta falsafa na dira ya kundi ulikotoka ambalo ulikataa kuongozana nalo kwa madai kuwa njia wanayotumia haiwafikishi mnakotaka kwenda, ninamini kundi hili litakufukuza haraka sana ili usiwachanganye na kuwachelewesha safari yao. CHADEMA wanamvumilia sana kutomfukuza Shibuda alistahili afukuzwe. Kutokupewa uwaziri kivuli haikuwepo kwenye mapatano wakati anajiunga na Chadema. Mbona kuna wengi wameachwa.
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Shibuda atakuwa kama Lyatonga soon. Kutoka kuwa mwanasiasa mahiri mpaka kufulia na kupauka na kubaki kujikomba-komba kwa watawala.

  ukiyavulia nguo yaoge tu.

  wewe msukuma wa wapi? huna msimamo?

  Chadema ni makini baba. Kama unatangatanga, kivyako!

  Rudi CCM mkuu.

  au unaogopa kuwekwa kitengo cha Tambwe Hiza?
   
Loading...