Kwa Shibuda, Hata CHADEMA Hakuna kivuli!

ndugu MAGGID,

Swala la msingi hapa ni tujiulize, je unapojiunga na CDM si maana yake umekubaliana na mtazamo na mwelekeo wa CDM na wanachama wake? sasa inapofika baada ya kuchaguliwa unaleta chokochoko za kwenda kinyume na maadili ya CDM maana ya ni kuwa na mtazamo tofauti?

Mimi nafikiri hata wewe kuna kitu hapa unatuchanganya, unapofanya vitu ambavyo vinaifever CCM au CUF maana yake si kuwa na mtazamo tofauti bali ni wazi wewe ni kipandikizi na msaliti mkubwa.

Nasema hivi kutokana na mambo ambayo yamekuwa yakifanyika mfano swala Shibuda kuisifia CCM ile hali ndio imetufikisha kwenye hii hali ya umasikini mkubwa, mgawo wa umeme, kuwapa wazungu madini bure, hali ya maisha kuwa ngumu na unasema utayaendeleza hayo mpaka mwisho maana yake nini? Huu ni usaliti mkubwa kwa watanzania.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom