Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,576
- 19,457
Taliban wamemechukua madaraka baada ya Marekani kuamua kuondoka. Marekani wasingeondoka, Taliban wangeenedelea kuishi milimani tu.Nisaidie kuelewa inakuaje marekani na jeshi lake yupo Afghanistan halafu anaruhusu serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kura kuondolewa? Wameruhusu ama wamewasusia nchi watajijua wenyewe?
Kinachokatisha tamaa ni kuwa baada ya miaka 20 (yaani mtoto aliyezaliwa wakati vita inaanza, leo hii yuko College), marekani ilifundisha askari 300,000 wa afghanstani na kuwapa silaha za kisasa. Baada ya Marekani kuondoka, hao askari laki tatu wakakimbia kutoka makambini kwao na kuacha silaha zote zichuliwe na talibani bila hata kupigana. Inawezekana kabisa kuwa baadhi ya hao askari waliofundishwa na Marekani walikuwa ni wanachama wa taliban, kwani isingekuwa rahisi Talibani atoke milimani na kuanza kuendesha zile humvee za Marekani mara moja kwa vile yale siyo magari ya kiraia, controls zake ni complex kidogo kwa vile zinaingiliana na weapon systems za gari lenyewe inabidi mtu afundishwe namna ya kulitumia bila kurusha makombora hovyo hovyo.