Kwa Picha: Siku ya Kwanza Ofisini Mhudumu wa Ofisi Afghanistan Mpya

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,301
2,000
"First day in office today for the new Office Assistant in Kabul"!

FB_IMG_16293154692679985.jpg
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,288
2,000
Kwa hiyo marekani baba wa demokrasia kasepa mchana kweupe huku jamaa wakiikanyaga demokrasia live kwa kumkimbiza rais ikulu kwa risasi...waafrika hasa wanaharakati wajifunze marekani sio mtu wa kumshobokea.
Kwa dunia hii US, ni kama maji huwezi ukamkwepa kamwe!!labda akupotezee tu, lakini akuamulie tena kama hizi nchi zetu za kiafrika !!mwaka mmoja tu, ni mrefu mtatafutana!!!
 
Vesuvius

JF-Expert Member
Jun 27, 2021
572
1,000
Naam, tuendelee kushobokea kura za kwenye mabegi.
Nisaidie kuelewa inakuaje marekani na jeshi lake yupo Afghanistan halafu anaruhusu serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kura kuondolewa? Wameruhusu ama wamewasusia nchi watajijua wenyewe?
 
Vesuvius

JF-Expert Member
Jun 27, 2021
572
1,000
Kwa dunia hii US, ni kama maji huwezi ukamkwepa kamwe!!labda akupotezee tu, lakini akuamulie tena kama hizi nchi zetu za kiafrika !!mwaka mmoja tu, ni mrefu mtatafutana!!!
I see..na kwa Afghanistan unaweza nisaidia ni ipi approach ya usa wamewaruhusu taliban ama wameisusa nchi? Ama wana mkakati kiporo wa siku zijazo?
 
Mi Corazon

Member
Oct 16, 2018
38
125
I see..na kwa Afghanistan unaweza nisaidia ni ipi approach ya usa wamewaruhusu taliban ama wameisusa nchi? Ama wana mkakati kiporo wa siku zijazo?

Mkuu ni hivi USA amekaa na jeshi la afghanistan kwa miaka 20. Na wamewatrain vya kutosha so Trump alipoingia akaandaa utaratibu wa kuwatoa majeshi ya USA Afghanistan.

Na ndio hicho kinavhoendelea sasa kwamba waachie nchi wanaweza kuiendesha wenyewe maana majeahi ya Afghanistan ni wengi kuliko Taliban . Ila sasa kilichotokea ni unexpectadly Taliban wamechukua nchi mapema sana
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
5,592
2,000
Mimi siyo Mmarekani, ndugu. Mimi ni Mtanzania. Ndio maana nikaona niongelee mfumo wetu Watanzania (kura za mabegi). Hayo mengine Wamarekani walioko katika JF watakujibu.
Nisaidie kuelewa inakuaje marekani na jeshi lake yupo Afghanistan halafu anaruhusu serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kura kuondolewa? Wameruhusu ama wamewasusia nchi watajijua wenyewe?
 
Dublin

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
1,188
2,000
Nisaidie kuelewa inakuaje marekani na jeshi lake yupo Afghanistan halafu anaruhusu serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kura kuondolewa? Wameruhusu ama wamewasusia nchi watajijua wenyewe?
Nahisi ni mtego! Kwanini US wanasaidia kuwaondoa raia na kuwatafutia hifadhi maelfu kwa ma elfu!!? Kwanini haachi uwanja wa ndege!!? Kwanini ameongeza wanajeshi 1000?

Talibani walikuwa wamejichimbia sana kuwapata ilikuwa ngumu sasa wamejitokeza na wanajiachia! Wakianza kupigwa ni mapigo rahisi sana maana waliookuwa wamejificha pameshaonekana, na sasa wanazagaa mitaa ambayo US anaramani zote!
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,288
2,000
I see..na kwa Afghanistan unaweza nisaidia ni ipi approach ya usa wamewaruhusu taliban ama wameisusa nchi? Ama wana mkakati kiporo wa siku zijazo?
Sasa kwa miaka 20, una wajengea uwezo wenye nchi ili waweze kujirinda, lakini bado hawaeleweki unafanya nini?watalibani hawazidi 70, 000!!nyie mna jeshi la watu 200, 000 vifaa vya kisasa lakini, limejaa mamluki tu, na ndio maana US, ameona hata aendelee kukaa hapo miaka 50!!bado akiondoka kinachotokea sasa kitatokea tu.

Ni bora aonekane ameshindwa tu!!labda iwe nchi ya kuhifadhi magaidi tena ambao wataishambulia US, ndio wanaweza kurudi!!japo hata hao talibani kwa sasa lazima wabadilike tu , kwani miaka 20, nao wameishi kwa tabu sana!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom