bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,667
Ni documentary moja ya RAIA Wa Kiingereza anafanya utalii kwa nchi zenye risk kubwa, nazipenda hizi documentary kwani zinanisaidia kufahamu wenzetu wanaishi vipi.
Baada ya kuangalia mwanzo mpaka mwisho wa safari ya mwamba Afghanistan nami nimewiwa kwenda kutalii kule siku moja, kumbuka jamaa ameenda kipindi hiki Taliban wakiwa wameshika nchi.
Kikubwa nlichokiona Taliban wanaogopeka sana Afghanistan ila jamaa walimpa Uhuru wa kupiga picha maeneo mbalimbali Ila alipewa warning na Dreva Tax asipige picha kwenye maeneo ya kimkakati kama vile kambi za jeshi, vituo vya polisi...nk
Ilifika mahali mpaka jamaa anawauliza wewe ni Taliban, Wanajeshi wa Kitaliban wanamjibu Yes, kuna sehemu wanakula msosi pamoja na askari wa kitaliban ila jamaa wanatisha anzia mavazi yao mpaka userious wao.
Kuna vivutio vingi vya utalii, nyanda mbalimbali za milima, chui wa kwenye barafu, mito, majengo ya kale pamoja na tamaduni zao.
Pia RAIA wengi wa Afghanistan ni maskini kwani kila sehemu alipokua anapita watu wengi wanamfwata na kumwomba hela kuna sehemu iliwapa hela aisee waligombania mnoo hata ukiangalia nyuso zao hazina matumaini kabisa.
Ukitua tu pale Kabul international Airport na shirika la ndege la Kam airways unapatana na kibao I love Afghanistan.
Kuna mji unaitwa Jalalabad watu wanauza silaha kama bamia zinavyouzwa soko la usiku Mbagala tena ni mashine haswa na kuna fundi wa kurepair vinu kabisa silaha nyingi ni made in China na Urusi.
Hapo ndipo nliposhangaa silaha kuuzwa kweupe, Wamarekani wameacha vifaa vyao Vingi sana Afghanistan sijui ni mtego au maji yalizidi unga asilimia kubwa ya wanamgambo wa Talibani wameachana na AK 47 za mrusi na sasa wanamiliki vinu vya kimarekani, magari ya Humvee ni mengi sana mengine yakiwa mazima yanatumika na Taliban mengine ni Mikweche.
Next time nikizichanga I hope miezi kama hii ntambeba my Valentine tukale Bata mitaa ya Kabul Pale.