pettymarcel
JF-Expert Member
- Jun 17, 2012
- 2,161
- 880
mbona kimya miss.chaga lete maujanja
wakuu Sijaelewa
hiZo bidhaa wanatengeneza wao wenyewe Alibaba au Hapo ni uwanja Wa kukutana na kufanya biashara Na Makampuni mbalimbali?
Mkuu kujiunga ni mpaka uwe na kampuni ... Halafu ukitaka kununua vitu huwezi nunua kimoja kimoja mpaka kwa ujumla ...
Naomba ufafanuzi wako tafadhali .
Kama unataka business na Huna pesa ya mtaji mwingi ingieni Alibaba tafuta small business partners .
Alibaba is no 1 Hamna matapeli mke wewe .Imeizidi google na eBay .its safe
KARIBU
- Ni kama unavyosema sokoni KARIAKOO, kuna wauzajia wa rejareja na jumla jumla.
- Nyongeza ni kuwa waweza kupata Business Partner - kama alivyo eleza mleta mada
- Pia pitia hii link | AliExpress.com - Online Shopping for Electronics, Fashion, Home & Garden, Toys & Sports, Automobiles from China. | Ni sehemu ya alibaba.com
umeuliza au umeeleza?
Mkuu hilo ulisemalo sio kweli kabisa.
Usije ukawaponza waTz hapa.
ALIBABA.COM Hawatoi Guarantee yyt kwa Washiriki waliomo humo na makampuni mengi yaliomo humo ALIBABA.COM hayakubali PAYPAL as a source of payments.
Kwa sababu PAYPAL inakuhakikishua Usalama wa Pesa zako.
Wengi wao wanataka utume pesa kwa Moneygram au Western Union.
Na njia hizi zote HAKUNA USALAMA WAPESA ZAKO.
Ukiwaambia utume kwa (LOC) kupitia benki yako ASILIMIA 90% ya makampuni hayo WANAKATAA.
WIZI WENGI MNO kupita WAAMINIFU.
Mwenye kutaka bidhaa CHINA ni bora mara milioni upoteze hio NAULI uende mwenyewe.
Siyo kweli Mkuu! Alibaba nao mbona wana kitu wanaita Escrow ambayo ni sawa na hiyo PayPal??!!
Wizi wakubwa hawa wachina.
Msiwashauri watz wenye mitaji ya kubangaiza.
Mtawaliza watu machozi ya Damu.
Hebu mkuu jaribu kutumia hio Escrow hata kwa bidhaa ya dola 20 tu oune moto wake.
Mimi nakwambia kitu kilichonikuta LIVE!
Sio kuhadithiwa.
Mkuu hebu mwaga story yote jinsi ilivyokuwa!
Haya ndo matatizo ya wa-TZ! Hata asiyekuwa na uzoefu anajidai kuwa na huo uzoefu! Kukatishana tamaa mwanzo mwisho! Wenye uzoefu nao wanatoa infos nusu nusu tu sijui tutabadilika lini?
Huwa nawakubali Money Stunna na Konzogwe jamaa huwa wanamwaga uzoefu mpaka unatamani ufanye hiyo biashara, hawa wengine magumashi tu! Konzogwe hebu njoo huku usikie huu mjadala kuhusu Alibaba.com! Money Stunna njoo huku utoe uzoefu wako kuhusu online businesses, watu wanazingua huku!!
Sishauri mtu ajiunge au anunue vitu alibaba wengi ni wezi matapeli (scammers) unagiza simu unaletewa mdoli wa kichina,
Stori ni ndefu mno.
Kwa kifupi nimekuja washtukia kwenye malipo.
Tumeshakubaliana bei na kila kitu mwisho kwenye kutuma malipo mimi nilihimiza aidha kutumia Paypal au (Lc) letter of Credit kipitia benki yangu, jamaa wanahimiza Western Union yaani utafikiri namtumia shangazi hela ya Sikukuu!
Kuwauliza sababu ya Kukataa hizi njia Ambazo zinakubalika Ulimwenguni kote eti wanasema Pesa inachelewa!
Pumbaff kabisa.
Wizi hawa mi nakwambia.
Na km ukipata muaminifu basi ni mmoja kati ya milioni.
Alibaba is no 1 Hamna matapeli mke wewe .Imeizidi google na eBay .its safe
acha upotoshaji bana wewe, ukiona mmoja haumwelewi unaachana naye unaenda kwa muuzaji mwingine. kwanza siku hizi alibaba wana escrow, tafuta gold supplier nunua kwa escrow, siyo unaponda tu ONE IN A MILLION, unafikiri kampuni ingekuwepo mpaka sasa?!!! watu tunanunua kule kila siku, cha kuhofia sanasana ni ubora tu, na kwa hilo kama ni mteja unataka vingi wanakutumia sample BURE!!