Kwa nini wasichana hawakupenda?

Kwa nini wasichana hawakupenda?

karv

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
1,801
Reaction score
3,272
Una umri wa kutosha wa kuwa na rafiki wa karibu wa jinsia tofauti. Ungependa kumpata mtu anayevutia na aliye na imani kama zako za kidini.

Hata hivyo kila mara unapojaribu kuanzisha uhusiano ulihisi kana kwamba uligonga mwamba.

Kipi unachopaswa kufanya

1)Jifunze kuwa na adabu
~"Mwenye upendo hakosi adabu." Sasa wewe endeleza dharau kwa watu halafu uone kama utapendwa na yeyote.

Ukiwa na adabu unaonyesha unawaheshimu wengine na unasitawisha utu. Kumbuka wasichana wengine kuangalia na kuchunguza jinsi unavyowatendea watu wengine na familia yako ili akufahamu vizuri.q

2)Tunza usafi wako
~Ukipunguza usafi wako utapoteza nafasi ya kumvutia msichana.

3)Jifunze jinsi ya kuendeleza mazungumzo
~Msingi wa uhusiano wa kudumu ni mawasiliano mazuri.

4)Heshimu uamuzi wa msichana.
~Kama hataki usimbembeleze. Kuwa na kipimo cha kubembeleza hawachelewi kukutangazia ubaya hawa.

Mengine mtaongezea wenyewe ukiona hujaelewa jua ndio unakaribia kuelewa hapo.
 
hudumia kulingana na urefu wa kamba yako
 
Back
Top Bottom