demokrasia
Member
- Apr 6, 2011
- 52
- 5
Mimi ni mwanaume nina mpenzi wangu ambaye anapenda sana kutishia kuniacha kila inapotokea ugomvi kidogo tu. Mara nyingi nimekuwa nikijitahidi sana kuomba msamaha hata kama kosa ni la kwake, ili tu mambo yaishe tusonge mbele. Wiki moja iliyopita kama kawaida yake amenitishia kuniacha na akaniambia kuwa niache kumpigia simu ili nimsahau. Lakini safari hii sijataka tena kuomba msamaha, badala yake nimemwambia kuwa ok waweza kwenda, nitapata mpenzi mwingine. Zikapita siku nne sijamtafuta, ghafla yeye kaanza kunitafuta na kuniomba nimsamehe kwa maneno aliyoniambia. Wana JF naombeni mawazo yenu, hii maana yake ni nini?