Kwa nini wakwe hawaelewani

babuwaloliondo

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
378
174
Jamani naomba kuuliza
Nikwanini kunakuwa na kutokuelewana kwa wazazi wa mwanaume na wakwe zao?
esp mama mzazi wa mwanaume na mke wa mtoto wake, maana kila ndoa nyingi zina malalamiko haya!.
Kisa hasa ni nini hasa?, je kwa ambao hawajao wanawezaje kuepusha hili!.
 
aaaaahhhh!!! mie natarajia wangu tupendane kama mama yangu mzazi lol!!

lbd tusubiri tuone wengine wanasemaje!!! sina uzoefu zaidi!!!
 
Ni swala la uelewa, kujitambua, na kuyakubali mabadiliko.

Nitafafanua kidogo: kijana kabla hajao mara nyingi anakuwa karibu na familia yake (baba, mama) hata kama amepanga haoni shida kutoa matumizi kwa familia yake (japo si wote) lakini anapooa automatically akili yake anailekeza kwa mamsapu wake coz atakuwa ametengeneza familia yake.

Hali kama hiyo inapotokea yale matumizi aliyokuwa anayapeleka nyumbani (kwa baba na mama) yanapungua au yasiwepo kabisa! Hapo mama mzazi anaona kama ametupwa, amedharaulika au kusahaulika na lawama zinaenda kwa mkwe kwamba ndiye anayebana matumizi; sasa katika hali ya ubinadamu mama mzazi naye anasahau hata wakati anaolewa yeye hayo yalitokea kwa namna moja ama nyingine, hivyo chuki inajengeka kwa yule mkwe (mke wa mtoto), kumbe ni swala la mabadiliko na mzunguko wa maisha. .....

Yatakiwa akili mukichwa kuyakabili haya mambo

:loco::loco::loco::loco::loco::loco::loco::loco:
 
The following user say thanks to mama mia for this usefull post
susy (Today)
 
Well said.
 
Mama mkwe kwa kawaida huwa anaona kila kitu anachofanyiwa mwanawe sicho. Mfano, chakula anachopikiwa siyo kizuri, vile anavyohudumiwa sivyo na kadhalika na kadhalika. Bado anataka kuwa na control na mwanawe na anataka mkwe awe mirror image yake, kitu ambacho hakiwezekani. Akiona mkwe amenunuliwa kitenge au viatu na yeye analazimisha. Alimradi inakuwa vurugu tu.

Wakiingia na mawifi ndiyo inakuwa balaa kabisa.

Lakini ukipata mama mkwe mwenye imani kwa kweli unastarehe sana, maana huwa anakusaidia kwa mawazo na katika shughuli za ujenzi wa familia.
 
Back
Top Bottom