Kwa nini usachi simu ya mpenzio?

Inasaidia. Usidhani hao wanawake nao hawatongozwi. Kuna wanaume ambao wanawapenda hawa wanawake zaidi ya wanavyopendwa na wanaume zao.

Kuna baadhi ya wanawake wanataka kujua nini kinaendelea kwa wanaume zao ili wajue status zao, na wajue jinsi ya kusawazisha mambo ili maisha yao ya mapenzi katika ndoa au mahusiano yawe na usawa.

Big up mkuu, nakubaliana na wewe mia kwa mia lazima kujua status ya mwenzako. na lakini kwa nini mfichane?
 
Big up mkuu, nakubaliana na wewe mia kwa mia lazima kujua status ya mwenzako. na lakini kwa nini mfichane?

Remmy, unaijua status ya mpenzi wako/mumeo/mkeo kwa kuchunguza simu yake?
 
Siipendi kabisa simu ya mke wangu.
Ile ni simu yake ya mkononi, siishiki, pia sitaki aishike yangu.
Namuamini kuwa ni msafi, binafsi najiamini pia..
Akitaka kunionyesha kitu, basi atanipa yeye mwenyewe, na sitavuta mipaka.

kama mnapenda na mliambana mtakuwa pamoja kwenye shida na raha
nini simu kitu gani???mwache achungulie kama msafi wa ndoa/uhusiano wako akuna atakacho kumbana nacho zaidi ataishia kucheka na ku smile ,..n hiyo kumwakikishia usalama wake zaidi....
 
kusachi simu ya mpz wako ni kuto jiamini kama unajiamini na kujua ww ni mtu mwema vivyo hivyo muamini mwenzio na ujue yy ni mwema,kila jambo linawakati wake na mapenzi hayafichiki ni kikohozi eti so kama kuna baya linalotendeka ipo siku utafunuliwa tu,evytng done on darkeness will be in right one day.

Pearl uko juu kama tai ya msabato

si kweli acha tusiwadanganye watu....mi nikiwa na mpenzi wa aina hiyo kwanza nafurahi ukiona mwenzio anashika simu yako anakupenda
anakutakia mema,...si wote wenye nia ya ubaya wengine wanajua simu vishawishi so wanakusaidia ahata wakikufuma na masg zako za sweetbaby,hny darling,mnaitana mnarekebishana unakuwa umemwokoa na umeokoa uhai wa watoto zako...kwa nini uzae mtoto anaumwa wakati kuna uwezekano wa ku avoid???matapeli wa mapenzi wengi waoga kushikwa simu zao...ukiona mkeo ama mumeo anashika simu yako mwongezee na dollar kabisa...
 
Mahusiano au mapenzi huleta raha na furaha ya ajabu maishani lakini...........
kuna watu aidha wanaume au wanawake,wakikutana tu,utasikia 'naomba simu yako'. Ataanza kusachi,atasachi sms zote,misscall zote,dialled call zote,received call zote,majina yote yaliyoseviwa anafanya hivyo huku mimacho imemtoka na presha juu, je? hii inasaidia kweli? kwa nini uwe na mtu asiemwaminifu kama tatizo ndilo hilo?Wengine mpenzi wake akienda kuoga au toilet,utamwona chapchap kwa speed ya maili milioni 1 kwa saa anaingiza mkono kwenye nguo au begi na kuanza u CIA au u FBI,upelelezi wake,mwenzie anatoka bafuni anashangaa kumuona mpenzie kanuna,shida yote hii ya nini?Wengine kama simu zinafanana atafanya juu chini mbadilishane au uisahau simu yako ili ashinde nayo kutwa nzima ili iweje? kwani mkichokana lazima mtafutiane sababu?Unadhani Darling wako ni zoba kiasi cha kusahau kufuta sms zote za hatari? Unadhani mpenzi wake Asha atashindwa kumsevu kwa jina la Alli? Au mpenzi wake John atashindwa kumsevu kama Jane?Nawulizeni wana JF

pole sana mzee, yamekukuta nn?
mbona unaogopa sana mpenzi wako asione kilichoko katika simu yako?.....kuna nini cha siri wakati ukiugua ndiye atayekutawaza? Wanaojilisha upepo kumbe wako wengi! masha yamekuwa mafupi sana siku hizi, na asilimia 20 ya wanaume waliooa wanalea watoto wasio wao!!!!! angalia usije kuwa mmoja wao.
 
Siipendi kabisa simu ya mke wangu.
Ile ni simu yake ya mkononi, siishiki, pia sitaki aishike yangu.
Namuamini kuwa ni msafi, binafsi najiamini pia..
Akitaka kunionyesha kitu, basi atanipa yeye mwenyewe, na sitavuta mipaka.

Katika hali kama hii inaonyesha kuwa hata wanandoa wanaopata ukimwi shurti wawe wamelia kwenye wali au juice kwenye cafe fulani manake huku kuaminiana inaonekana ni kukubwa saaaana.
Labda zaidi ya 75% ya wanandoa wanaishi kwa imani tu lakini siyo bayana ya uhalisia wa mambo. Kwamba wanaamini/kufahamu kuwa nyendo kinyume na misingi ipo, lakini wasingetaka kufahamu. Watu wanadanganyana, eti sijui upendo, sijui kuchokana n.k. Hizi simu na mtandao ya internet zimeleta maendeleo makubwa lakini pia zimechangia sana kuharibu ndoa nyingi. Zimeongeza sana tija kwa mafataki.
 
I wouldn't like if my partner start to search my phone in my absence... thats called insecurity... I dont search my partner's phone for one main reason...
I would rather not know if he is having affair, I really dont wanna find out at least not at this moment
 
Kwasababu simu ndio midori ya wakubwa,hivyo yapendeza kuzichezea mara uzionapo,na vile vile zinawekwa hela hivyo ni bora kuzisachi waweza ambulia kitita!!!
sasa wewe unatafuta mkong'oto,akigundua salio lake limehamia kwako?vurugu unaziweza?
 
Kuna wengine huenda mabali zaidi wanapopata nafasi kama hiyo huweka simu kadi zao za ziada na kukopi number kutoka katika simu za wapenzi wao kwa hiyo wanakuwa na wakati mzuri wa kuzifanyia utafiti wakiwa mabali na wapenzi wao .kuna siku Ndugu yangu alitumiwa Text na mtu asie mjuwa na kumuliza wewe fulani ni nani kwako?pale pale nikajuwa kuwa jamaa ni Very sad na ni luza.
 
Kusachi simu ya mwenzio tayari umemvunjia Heshima kwa kumuona kuwa sio Mwaminifu.
Wanawake na Wanaume wapo wenye tabia kama hizo.
Kwa mchezo huo mtaishi maisha ya mashaka na ugomvi hadi mwisho wa maisha yenu.
 
Uchunguzi uliofanyika,katika nchi za kiafrika hivi karibuni, umegundua kuwa, kwa kutahiriwa,mwanamme anapunguza uwezekano wa kuambukizwa ukimwi kwa asilimia hamsini.UJUMBE ; kama una jamaa/ndugu yako bado ana ile sijui wanaita nini? mshauri atoe/akatahiriwe. .
 
Kama kweli watu mi wasafi wa miili na mioyo kuna ubaya gani wa mme au mke kushika simu ya mwenza wake?
 
Back
Top Bottom