Kwa nini usachi simu ya mpenzio? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini usachi simu ya mpenzio?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tall, Mar 4, 2010.

 1. T

  Tall JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mahusiano au mapenzi huleta raha na furaha ya ajabu maishani lakini...........
  kuna watu aidha wanaume au wanawake,wakikutana tu,utasikia 'naomba simu yako'. Ataanza kusachi,atasachi sms zote,misscall zote,dialled call zote,received call zote,majina yote yaliyoseviwa anafanya hivyo huku mimacho imemtoka na presha juu, je? hii inasaidia kweli? kwa nini uwe na mtu asiemwaminifu kama tatizo ndilo hilo?Wengine mpenzi wake akienda kuoga au toilet,utamwona chapchap kwa speed ya maili milioni 1 kwa saa anaingiza mkono kwenye nguo au begi na kuanza u CIA au u FBI,upelelezi wake,mwenzie anatoka bafuni anashangaa kumuona mpenzie kanuna,shida yote hii ya nini?Wengine kama simu zinafanana atafanya juu chini mbadilishane au uisahau simu yako ili ashinde nayo kutwa nzima ili iweje? kwani mkichokana lazima mtafutiane sababu?Unadhani Darling wako ni zoba kiasi cha kusahau kufuta sms zote za hatari? Unadhani mpenzi wake Asha atashindwa kumsevu kwa jina la Alli? Au mpenzi wake John atashindwa kumsevu kama Jane?Nawulizeni wana JF
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Siipendi kabisa simu ya mke wangu.
  Ile ni simu yake ya mkononi, siishiki, pia sitaki aishike yangu.
  Namuamini kuwa ni msafi, binafsi najiamini pia..
  Akitaka kunionyesha kitu, basi atanipa yeye mwenyewe, na sitavuta mipaka.
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Ya kweli hayooooooo..........??? Vipi kila akipigiwa simu anaenda kupokelea mbali na ulipo........hutauliza na kuanza upekuzi ghafra..........???
   
 4. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Mh! mzee naona ur very understanding man.
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Inasaidia. Usidhani hao wanawake nao hawatongozwi. Kuna wanaume ambao wanawapenda hawa wanawake zaidi ya wanavyopendwa na wanaume zao.

  Kuna baadhi ya wanawake wanataka kujua nini kinaendelea kwa wanaume zao ili wajue status zao, na wajue jinsi ya kusawazisha mambo ili maisha yao ya mapenzi katika ndoa au mahusiano yawe na usawa.
   
 6. Sydney

  Sydney Senior Member

  #6
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli simu zina mambo, mi najua ndoa moja ilitaka kuvunjika kwasababu ya simu ya mkononi likichosaidia ni mtoto wao alisema message hiyo ni yake alitumiwa na mpenzie, yaani jamani nyie simu hizi...looh! Lakini cha muhimu ni kuaminiana na kwanza hakuna umuhimu wa kushika simu ya mwenzio labda kuwepo na jambo la dharura sana!
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180

  Sydney cha muhimu si KUAMINIANA ni kuwa MWAMINIFU KWA MWENZI WAKO. utamwanini mwenzio kumbe anamega au megwa wewe unang'ang'ania kumwamini tuuu mwisho wa siku unaingizwa kwenye gridi ya taifa
   
 8. c

  compressor Member

  #8
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaemchunguza haupo tayari kumpenda
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Mar 4, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Pamoja na yote hayo lakini simu ni chanzo cha mifarakano kwenye ndoa.
  Mfano mkeo au mumeo anaweza akatumiwa sms ya mapenzi kimakosa
  (tuseme mtumaji alikosea namba)
  sasa endapo utaisachi simu ya mwenzi wako na ghafla ile sms inakukuta
  hebu fikiria ni hatua gani utaichukua kwa kosa ambalo mwenzi wako hajalifanya?
  Sio vizuri kupekuwa simu ya mwenzi wako.
   
 10. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kusachi simu ya mpz wako ni kuto jiamini kama unajiamini na kujua ww ni mtu mwema vivyo hivyo muamini mwenzio na ujue yy ni mwema,kila jambo linawakati wake na mapenzi hayafichiki ni kikohozi eti so kama kuna baya linalotendeka ipo siku utafunuliwa tu,evytng done on darkeness will be in right one day.
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Amen to that!

  Ni maamuzi magumu sana haya kuchukua na Mungu atupe nguvu kulishinda ni mtihani mzito kwa kweli; kwani wakati mwingine hivi vitu hutokea kwa bahati mbaya sio kusudio lako ama langu kusachi lakini ikitokea ukasachi ukakutana na utata utafanyaje?

  Nitwapeni kisa;

  Jamaa yangu wa karibu alikuwa hana mazoea haya kusachi simu ya masap wake na katu hakuwahi kuwa na wasiwasi naye lakini kuna siku wakiwa mezani wanakula ikapigwa simu ambayo masap hakutaka kuipokea; simu iliita na baadaye jamaa kwa kuona kero kaichukua kuwa iitapo tena aipokee yeye; katika kusubiri; ikatumwa msg "Darling kwa nini una hupokei simu yangu? Nakumbuka sana mchezo ulionipa jana natamani jamaa angekuwa hajarudi leo nije kulala nawe tena! I miss you" (Huyo jamaa yangu ni kweli alikuwa ndo karudi safari) Kuanzia hapo ikawa patashika na mwanamke ang'aka sio sms yake kwa kuwa tu namaba hiyo haiko kwenye phonebook! Jamaa alikosa amani sana na usiku huo huo alinifuata mimi nimshauri; nimejitahidi sana kuwashauri na nimekaa nao wote wawil; na kwa jinsi nilivyoongea nao wote ni kweli shem wangu alimtenda jamaa yangu kwenye matrimonial bed ikiwa ni revenge ya makosa ya ya jamaa naye kuwa na tenda nje miezi sita nyuma!

  Well wamesameheana lakini naamini yule jamaa hatoacha kusachi simu ya mamsap! na sisi wengine tukisikia haya tunaamua kutia maji kabla!
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 674
  Trophy Points: 280
  Kwasababu simu ndio midori ya wakubwa,hivyo yapendeza kuzichezea mara uzionapo,na vile vile zinawekwa hela hivyo ni bora kuzisachi waweza ambulia kitita!!!
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ni dalili ya kutokuaminiana.
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  may be....may be not
   
 15. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  simu yangu iko huru kushikwa na mke wangu, manake hakuna ninachoogopa atakikuta huko siku, Hata mimi nashika simu yake na niko huru kuangalia kilichomo sijawahi kupewa sunction na ukweli ni kuwa kama kuna ka mchezo ka chafu kanaendelea watu wanakuwaga so protective na simu zao! Kama mtu hataki simu yake ishikwe heshimu matakwa yake, Kuna mambo mengi sana nyuma ya pazia huwa hatuyajui kama yangefunuliwa kwa wapenzi wetu bila shaka ndoa nying sana zingevunjika! Binadamu Bwana hachungwi kama ka-mbuzi anaweza soma na ku-delete anaweza clear call history anaweza wasiliana kwa njia nyingine
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  1+1 yes kwanini akukakatalie kuishika?
   
 17. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,827
  Likes Received: 1,980
  Trophy Points: 280
  Ni simu yake na sio ya ofisi wala ya familia
  Ingawa binafsi nataka simu ya tunayependana iwe free zone hata kama nitakuwa siishiki na kusearch
   
 18. y

  yegomwamba Member

  #18
  Mar 5, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kusachi simu ya mpz wako ni kuto jiamini kama unajiamini na kujua ww ni mtu mwema vivyo hivyo muamini mwenzio na ujue yy ni mwema,kila jambo linawakati wake na mapenzi hayafichiki ni kikohozi eti so kama kuna baya linalotendeka ipo siku utafunuliwa tu,evytng done on darkeness will be in right one day.

  Pearl uko juu kama tai ya msabato
   
 19. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Hata mm pia walau hapa kwenye wekundu tunakwenda sawa; sasa shida nikuwa unakutana na reaction tofauti siku ambayo imetokea umeishika; mwenzio anakosa raha au anakimbilia kukunyang'anya! Utaacha kuinyemelea kuisearch?
   
 20. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,827
  Likes Received: 1,980
  Trophy Points: 280
  Na kama amekaa vibaya unaweza kumtwika ndoo ya fasta. Nimekupa thanks kama nilivyokuahidi MJ
   
Loading...