Kwa nini tupoteze amani tuliyonayo kwa visingizio vya muungano? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tupoteze amani tuliyonayo kwa visingizio vya muungano?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ruttashobolwa, May 28, 2012.

 1. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Amani tuliyo nayo watanzania, inawafanya hata majirani zetu kila kukicha kukimbilia tanzania, waki amini hakuna kitu bora katika maisha kama amani. Watanzania tumekuwa tukiishi kwa upendo na amani pamota na kuwepo kwa dini tofauti na makabila. Lakini kila iitwayo leo amani hii ina onekana si kitu cha muhimu tena, kwani vitendo vinavyo onesha kuleta hisia za udini vina anza kuoneka huku tatizo la muungano likiwa kisingizio. Nina amini hakuna kitabu chochote cha dini kinacho hamasisha kujenga chuki kwa dini zingine, leo hii nigeria,sudan wanavuna walicho panda, dini ni chanzo cha amani ikitumika vizuri, lakini watu wachache utumia dini vibaya kwa maslai yao binafsi. Hakuna hisia mbaya ambazo ukisumbua kichwa cha mwanadamu kama hisia za udini. Kinacho tokea sasa zanzibar kinabeba hisia za udini kabla hata ya kufikiri kuna mkono wa siasa, kitendo cha kanisa kuchomwa moto,kina ondoa dhana nzima ya swala la muungano. Naamini waislam walio wengi hawa kubaliani na vitendo vinavyofanywa na watu wachache hili kuuchafua uislam,na jua dini zetu hazikosi watu ambao wapo kwaajili ya kuzichafua dini zao,pengine hao ndio wanakuwa wakipandikiza hisia na chuki kwenye dini zetu watu kama ( njiwa na abu) wanaonekana dhahiri kuwa wachochezi ili kuigeuza nchi yetu kama sudan kwa maneno yao ya uchochezi ili waonekane wana utetea uislam kitu ambacho si kweli. Kwa kuwa na watu kama hawa kwenye mtandao watatusababishia kuiweka jf rehani,maana inaweza kuonekana ni sehemu ya kuchochea maovu badala ya kuyapinga. Najua muislam aliyeshika din kweli hawezi kumchukia mkristo.watanzani tusikubari mtu au kikundi chochote kutokomeza amani na mshikamano tulio nao kwa kutumia vivuri vya dini zetu.
   
Loading...