Ndugu zangu waislam, tuitunze hii amani tuliyonayo, msirithishwe chuki

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,311
4,019
Hakika nawaambia adui yenu sio Mkristo au Muyahudi, adui yenu ni huyo anaewajaza chuki dhidi yetu.

Adui yenu ni hayo mataifa ya itikadi kali yanayowapa maagizo ya kufanya jihad dhidi ya jamii ya kikristu na kiyahudi.

Tunategemeana, uchumi wenu ni uchumi wetu, msidhani mnaweza bila sisi, msidhani mnaweza kututupa chini na mkawa juu yetu, kitachofata ni vifo vya vizazi na vizazi.

Hizi dini walituletea wakati hatujui chochote kuhusu mkuchukia mtu kwa sababu haamini kama wewe, sasa tumezichukua hizi dini na zinatupelekesha vile makuhani wa dini wanavyotaka.

Kumbuka, Islam inaamini asili yake ni Ibrahim, muyahudi anaamini asili yake ni Ibrahim na mkristo nae anaamini asili yake ni Ibrahim. Basi kama ni hivyo, Ibrahim huyo tunayemuenzi alikuwa na Mungu mmoja, ndio huyo tunayemuabudu, kwanini tena tutengane, ina maana tunakuwa wanafiki kwa babu yetu ibrahim na Mungu wake mmoja.

Kumbukeni, pengine dini hizi ni mchongo wa kutenganisha watu na sisi tumo tu kupokea yale tunayorithishwa.

Vita ni mbaya nawaambia, wala hakuna mahala eti utaenda kupumzika kwa amani peponi eti kisa uliuua asie amini kama wewe, hizo ni stori walianzisha ili muendeleze chuki walizozianzisha juu ya imani nyingine.

SHALOM, BWANA YESU ASIFIWE, ASALAAM ALAYKUM.
 
085730ff9a0c72859f2ae26b02152068.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom