Kwa nini TBC haionekani Mkoani Kilimanjaro?

Asamwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
3,805
Reaction score
2,581
Ni muda mrefu sasa tangu matangazo ya Televisheni ya Taifa (TBC) yaache kuonekana Mkoani Kilimanjaro.

Mwanzoni tulidhani ni tatizo la kiufundi ambalo lingerekebishwa, lakini hakuna dalili za hali kubadilika.

Tatizo hili linawakumba waliokuwa wanaona TBC kupitia madishi na pia wanaotumia vifumbuzi vya Star Times.

TBC kama chombo cha habari cha taifa inaendeshwa kwa kodi zetu, hivyo wananchi wote wanapaswa kupata matangazo yake bila ubaguzi.

Naomba kama kuna anayefahamau undani wa hili, atufahamishe.
 
huko ni kambi ya chadema. Tumeamua kusitisha matangazo kwa sababu mtufagilii kabisa nyie
 
TBC inapatikana japo signal zake ni chache mpaka umpate mtalaam wa kufunga dish ndo itashika!
 
Ni muda mrefu sasa tangu matangazo ya Televisheni ya Taifa (TBC) yaache kuonekana Mkoani Kilimanjaro.

Mwanzoni tulidhani ni tatizo la kiufundi ambalo lingerekebishwa, lakini hakuna dalili za hali kubadilika.

Tatizo hili linawakumba waliokuwa wanaona TBC kupitia madishi na pia wanaotumia vifumbuzi vya Star Times.

TBC kama chombo cha habari cha taifa inaendeshwa kwa kodi zetu, hivyo wananchi wote wanapaswa kupata matangazo yake bila ubaguzi.

Naomba kama kuna anayefahamau undani wa hili, atufahamishe.

Moshi ni mojawapo ya maeneo ambayo sumu za TBCCM zimeshindwa kupenya. So kuliko kupoteza resources zao kurusha matangazo yao huko ambako hawatazamwi, bora wazime tu.
 
TBC inapatikana japo signal zake ni chache mpaka umpate mtalaam wa kufunga dish ndo itashika!

Asante kwa ushauri mkuu. Nitajaribu kuwasiliana na wataalam.

Ila hata kama wamebadilisha frequency zao si wangefahamisha watazamaji wao?!
 
Back
Top Bottom