Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,255
- 113,669
Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kumekuwa na kelele nyingi kidogo za kutaka tuandike katiba mpya. Kelele hizo zinatoka pande mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanachama wa chama tawala.
Tumeanza kufuata tena siasa za mfumo wa vyama vingi miaka 18 iliyopita. Kwa watu wenye akili na wenye kuona mbele ungedhani kuwa wangeona umuhimu wa hayo mageuzi ya mfumo kwenda sambamba na katiba mpya ili kukidhi mahitaji ya mazingiya ya mfumo huo.
Sasa siku za hivi karibuni kusikia watu kama raisi mstaafu Mkapa, jaji mstaafu Kisanga na wengineo ambao kwa namna moja ama nyingine maoni yao yanaweza ku-influence public policy wakizungumzia umuhimu wa kuwa na katiba mpya inashangaza.
Ina maana watu hawa umuhimu huo wanauona leo na hawakuuona wakati ule? Au waliuona hata wakati huo lakini kwa vile katiba iliyopo iliwanufaisha wao wakaamua kula jiwe?
Hitimisho langu ni kuwa sisi kweli ni taifa la vilaza. Tutaingiaje kwenye mfumo mpya bila hata maandalizi ya msingi? Huo ni uendawazimu uliopitiliza.
Watu wenye akili na busara hujiandaa kwa manufaa ya mustakabali wao. Sisi hatukujiandaa. Tunatia aibu na kusikitisha.