Kwa nini sasa na si wakati ule?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,982
2,000
Baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kumekuwa na kelele nyingi kidogo za kutaka tuandike katiba mpya. Kelele hizo zinatoka pande mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanachama wa chama tawala.

Tumeanza kufuata tena siasa za mfumo wa vyama vingi miaka 18 iliyopita. Kwa watu wenye akili na wenye kuona mbele ungedhani kuwa wangeona umuhimu wa hayo mageuzi ya mfumo kwenda sambamba na katiba mpya ili kukidhi mahitaji ya mazingiya ya mfumo huo.

Sasa siku za hivi karibuni kusikia watu kama raisi mstaafu Mkapa, jaji mstaafu Kisanga na wengineo ambao kwa namna moja ama nyingine maoni yao yanaweza ku-influence public policy wakizungumzia umuhimu wa kuwa na katiba mpya inashangaza.

Ina maana watu hawa umuhimu huo wanauona leo na hawakuuona wakati ule? Au waliuona hata wakati huo lakini kwa vile katiba iliyopo iliwanufaisha wao wakaamua kula jiwe?

Hitimisho langu ni kuwa sisi kweli ni taifa la vilaza. Tutaingiaje kwenye mfumo mpya bila hata maandalizi ya msingi? Huo ni uendawazimu uliopitiliza.

Watu wenye akili na busara hujiandaa kwa manufaa ya mustakabali wao. Sisi hatukujiandaa. Tunatia aibu na kusikitisha.
 

Kipre tchetche

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
238
0
Walijifanya vipofu sasa wamelazimishwa
kuona .watanzania si wameamka? Wali
fikiri watz watakuwa kwenye usingizi milele
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
7,004
2,000
Mkuu Ambrose, yaliyotokea wakati wa uchaguzi yamei-expose nchi kwa kiasi kikubwa na wote hao unaowataja na wengine wengi ambao huwajui wameona hatari ambayo inaweza kusababisha nchi kusambaratika mara moja iwapo tutaendelea kukumbatia yakliyopo hivi sasa. Wanaoibuka na kudai hivyo wamepata pa kusimamia ndo maana unaona kelele zinaongezeka sasa. Na hii usidhani kwua ni kwa upande mmoja tu, hata wale waliopo jikoni wanalifahamu hilo na wanatafuta pa kuanzia tu kabla nao hajajiunga na kuikubali hoja ya katiba mpya kama kweli wana nia njema na nchi.
 

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
195
NI KWA SABABU YA UCHAKACHUAJI ILIKUWA MAPANGA YATEMBEE SASA BORA KUBADILI MFUMO KULIKO KUUANA KAMA WAKENYA SIO VIZURI-SABABU NI NYINGI LAKINI KUBWA KUTOA AMANI YA KWELI MANAKE HAKUNA AMANI PASIPO HAKI, NA HIZI NYINGINEZOInakandamiza haki ya mgombea binafsi
2. Inatoa fursa ya kuwa na tume ya uchaguzi ya uchakachuaji
3. Inatoa fursa ya watawala kuwanyonya watanzania kwa kuficha mikataba
4. Inatoa fursa kwa rais wa nchi kuwakandamiza watanzania kwa maamuzi yasiyo na mpaka idadi ya wizara, teuzi mabalimbali
5. Inatoa fursa ya matumizi hovyo ya mali ya umma mfano kazi ya naibu waziri na mkuu wa wilaya v. Katibu wa wizara na mkurugenzi wa wilaya
6. Inavunja kanuni ya principle of separation of powers -mbunge anakuwa waziri, watawala wetu wengi wapo juu ya sheria
7. Inatoa fursa ya ufisadi kwa watawala wetu kwa kuzuia hatua yoyote dhidi yao
8. Ilitungwa kwa ajili ya chama kimoja na sasa ni vyama vingi
9. Katiba ya sasa ya tanzania haitambui zanzibar kama nchi
10. Katiba ya sasa inabeba sheria 40 za nyalali alizosema zifutwe
11. Katiba ya sasa inarusu uzandiki mwingi wa kuchakachua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom