Mimi ni mwana "uma-jumuhi " wa kiafrika, ninaipenda Afrika, na ninautukuza sana uafrika wangu. Hata hivyo ninasikitika kuwataarifu wananzuoni wenzangu wa kiafrika, kwamba nimeoa mwanamke wa kizungu na sitakaa nioe mwanamke wa kiafrika ( hususani hawa wanao toka katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara/ the saharans )...Kwa nini ? Fuatana nami:
1. Wanawake wa kiafrika hawapatikani tena C Ngoja niiweke kwa kiingereza ili upate kunielewa zaidi )
" African women are no longer existing ". Wanasichana wote wa kiafrika ( hsusuani wale ambao wamekwenda shule ) ni kama wazungu kama sio wazungu kabisa..Tazama nguo wanazo vaa, jinsi wanavyo ongea, namna wanavyo tembea, vyakula wanavyokula, mitindo yao ya nguo, nywele n.k. fikra zao, mawazo yao nakadhalika, vyote kwa pamoja ni akisi ya yale yanayo fanywa na wanawake wa nchi za kimagharibi..Hivyo basi mimi kuoa mwanamke wa kiafrika, haitakuwa na mantiki wala maana yoyote kama mwanamke mwenyewe atakuwa na hulka za kizungu ).
2. Kwa kiwango changu cha elimu, nisingeweza kuoa mwanamke ambaye kiwango chake cha elimu ni chini ya elimu ya chuo kikuu, na tulivyoona hapo juu kwamba wanawake wengi wa kiafrika waliosoma wanajifanya wazungu kabisa, so hoja hii inaunga mkono hoja yangu ya kwanza.
3. NINA PENDA VITU ORIGINAL NA SIO FAKE : Kama ningeoa mwanamke wa kiafrika, ningekuwa nimeoa mwanamke wa kizungu ambaye ni " feki " lakini kwa sababu ninapenda kuwa na vitu original nimeoa mwanamke wa kizungu kabisa ili ijulikane moja kwamba nimeoa mwanamke wa kizungu.
( UFEKI WA WANAWAKE WA KIAFRIKA WANAO JIFANYA WAZUNGU NI PALE LINAPO KUJA SUALA LA BILI/ KATIKA MAMBO MENGINE YOTE WANAJIFANYA WANAWAKE WA KIZUNGU HALAFU LIKIJA SUALA LA KULIOA BILL WANAKUWA WAAFRIKA TENA...KUWENI WAZUNGU KABISA MUWE MNALIPA NA BILL )
4. Nimepunguza gharama za kulipia MAWIGI. Mke wangu ni mzungu, kwa hiyo haitaji kuvaa mawigi ya kazi gani sasa...
Hizi ni sababu chache tu, but zipo faida nyingi sana kwa kijana wa kitanzania ama wa kiafrika kuoa mwanamke wa kizungu...Utazisoma katika kitabu changu ambacho nitakitoa mwezi Aprili 2013..Katika kitabu hiki nimeelezea experience yangu pamoja na more 20 friends wa kitanzania ambao wameoa wazungu.