Kwa nini nimoea mwanamke wa kizungu..

Kwa nini nimoea mwanamke wa kizungu..

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,927
Reaction score
37,773
Mimi ni mwana "uma-jumuhi " wa kiafrika, ninaipenda Afrika, na ninautukuza sana uafrika wangu. Hata hivyo ninasikitika kuwataarifu wananzuoni wenzangu wa kiafrika, kwamba nimeoa mwanamke wa kizungu na sitakaa nioe mwanamke wa kiafrika ( hususani hawa wanao toka katika ukanda huu wa kusini mwa jangwa la sahara/ the saharans )...Kwa nini ? Fuatana nami:

1. Wanawake wa kiafrika hawapatikani tena C Ngoja niiweke kwa kiingereza ili upate kunielewa zaidi )

" African women are no longer existing ". Wanasichana wote wa kiafrika ( hsusuani wale ambao wamekwenda shule ) ni kama wazungu kama sio wazungu kabisa..Tazama nguo wanazo vaa, jinsi wanavyo ongea, namna wanavyo tembea, vyakula wanavyokula, mitindo yao ya nguo, nywele n.k. fikra zao, mawazo yao nakadhalika, vyote kwa pamoja ni akisi ya yale yanayo fanywa na wanawake wa nchi za kimagharibi..Hivyo basi mimi kuoa mwanamke wa kiafrika, haitakuwa na mantiki wala maana yoyote kama mwanamke mwenyewe atakuwa na hulka za kizungu ).

2. Kwa kiwango changu cha elimu, nisingeweza kuoa mwanamke ambaye kiwango chake cha elimu ni chini ya elimu ya chuo kikuu, na tulivyoona hapo juu kwamba wanawake wengi wa kiafrika waliosoma wanajifanya wazungu kabisa, so hoja hii inaunga mkono hoja yangu ya kwanza.

3. NINA PENDA VITU ORIGINAL NA SIO FAKE : Kama ningeoa mwanamke wa kiafrika, ningekuwa nimeoa mwanamke wa kizungu ambaye ni " feki " lakini kwa sababu ninapenda kuwa na vitu original nimeoa mwanamke wa kizungu kabisa ili ijulikane moja kwamba nimeoa mwanamke wa kizungu.

4. Nimepunguza gharama za kulipia MAWIGI. Mke wangu ni mzungu, kwa hiyo haitaji kuvaa mawigi ya kazi gani sasa...

Hizi ni sababu chache tu, but zipo faida nyingi sana kwa kijana wa kitanzania ama wa kiafrika kuoa mwanamke wa kizungu...Utazisoma katika kitabu changu ambacho nitakitoa mwezi Aprili 2013..Katika kitabu hiki nimeelezea experience yangu pamoja na more 20 friends wa kitanzania ambao wameoa wazungu.
 
Mwanazuoni gani hujui kuandika kitu kikaeleweka au kutumia kanuni za uandishi? Pia, mwanazuoni wa kweli hawezi kupita akijinadi kuwa yeye ni mwanazuoni kwa sababu kufanya hivyo ni kupingana na dhana nzima ya uanazuoni

1. Wanawake wa kiafrika hawapatikani tena C Ngoja niiweke kwa kiingereza ili upate kunielewa zaidi )

" African women are no longer existing ". Wanasichana wote wa kiafrika ( hsusuani wale ambao wamekwenda shule ) ni kama wazungu kama sio wazungu kabisa..Tazama nguo wanazo vaa, jinsi wanavyo ongea, namna wanavyo tembea, vyakula wanavyokula, mitindo yao ya nguo, nywele n.k. fikra zao, mawazo yao nakadhalika, vyote kwa pamoja ni akisi ya yale yanayo fanywa na wanawake wa nchi za kimagharibi..Hivyo basi mimi kuoa mwanamke wa kiafrika, haitakuwa na mantiki wala maana yoyote kama mwanamke mwenyewe atakuwa na hulka za kizungu ).

Huwezi ukawa na neno "wote" ikisha ukawa na neno "hususan", kama ni wote basi ni wote kwa jumla hakuna atokae humo, na kama ni hususan wanawake fulani basi sio wote

Fikra na mawazo ya mwanamke wa Kiafrika ni yepi? Mwanamke wa Kiafrika anaongea vipi na wa Kimagharibi anaongea vipi? Na mwondoko jee?
Unataka kutuambia wewe unatembea na kaniki au rubega barabarani au wewe kuvaa mavazi ya kimagharibi ni ruhsa ila akifanya mwanamke ni mwao?

2. Kwa kiwango changu cha elimu, nisingeweza kuoa mwanamke ambaye kiwango chake cha elimu ni chini ya elimu ya chuo kikuu, na tulivyoona hapo juu kwamba wanawake wengi wa kiafrika waliosoma wanajifanya wazungu kabisa, so hoja hii inaunga mkono hoja yangu ya kwanza.

Sio usingeweza, sema usingetaka. Kwa sabababu hakuna chochote kinachoongoa uwezo wako huo, zaidi ya utashi na matakwa yako.

3. NINA PENDA VITU ORIGINAL NA SIO FAKE : Kama ningeoa mwanamke wa kiafrika, ningekuwa nimeoa mwanamke wa kizungu ambaye ni " feki " lakini kwa sababu ninapenda kuwa na vitu original nimeoa mwanamke wa kizungu kabisa ili ijulikane moja kwamba nimeoa mwanamke wa kizungu.

( UFEKI WA WANAWAKE WA KIAFRIKA WANAO JIFANYA WAZUNGU NI PALE LINAPO KUJA SUALA LA BILI/ KATIKA MAMBO MENGINE YOTE WANAJIFANYA WANAWAKE WA KIZUNGU HALAFU LIKIJA SUALA LA KULIOA BILL WANAKUWA WAAFRIKA TENA...KUWENI WAZUNGU KABISA MUWE MNALIPA NA BILL )

Umewafanyia utafiti wanawake wangapi ukajua kuwa hawalipi bills? Kuna wanaume wanatunzwa na wanawake kabisa itakuwa kulipa bill?

4. Nimepunguza gharama za kulipia MAWIGI. Mke wangu ni mzungu, kwa hiyo haitaji kuvaa mawigi ya kazi gani sasa...

Aliyekwambia Wazungu hawavai wigs au kuweka extensions kakudanganya. Wanabandika nywele kwa sababu Wazungu wengi wananywele kidogo kichwani hawapendi.

Hizi ni sababu chache tu, but zipo faida nyingi sana kwa kijana wa kitanzania ama wa kiafrika kuoa mwanamke wa kizungu...Utazisoma katika kitabu changu ambacho nitakitoa mwezi Aprili 2013..Katika kitabu hiki nimeelezea experience yangu pamoja na more 20 friends wa kitanzania ambao wameoa wazungu.

Mtu asiyeweza hata kuunga sentensi mbili bila ya vidoto na asiyeweza hata kuelewa kanuni za uandishi, si mwandishi
 
Nimeiona mantiki ya mtazamo wako na nakubaliana na wewe kuwa wanawake wa kiafrika siku hizi tabu kuwapata(sio kweli hawapo)
"
Lakini umenishangaza pale unaposema huwezi kuoa mwanamke ambae ana elimu chini ya chuo kikuu at the same time unajiita muafrika,hapa unajikinza
"
Unatafuta mwanamke Mwafrika au msomi?Ni kitu gani anacho msomi na mwingine hana?
"
Kwenye masuala ya mke bora hakuna cha msomi wala asiesoma.
"
Kwanza dhana ya usomi ni ya kimagharibi na si uafrika,bibi yako hakusoma na alikua mke bora
"
Pili,ili uonekane msomina usomi uwe na maana ni pale utakapowapima watu kwa ubinadamu wao na sio kitu kingine ndipo usomi utakua na mantiki
"
Kitu ambacho so colled wasomi wanafail ni hiki
"
Watu wanatarajia wasomi wawe mfano wa kuigwa na wawe kioo cha jamii kwa kuonesha kuelimika kwa kutokuonesha ujinga,wao ndo wanaigawa jamii kwa kuwatenga wasiokuwa na elimu na hata kutokuoa wasiosoma utadhani sio binadamu wakati mama yake alikua hata kuandika hajui na alikua mama bora
"
Siku hizi nikisikia msomi naona kama ujinga vile!
 
Pole sana Mtumwa Likud, umepotea njia ndugu yangu, wanawake wa kiafrika bado wapo na bado ni stahiki kuolewa.

Unaposema unaoa mzungu ili kuepuka vitu feki, si kweli kuwa wote wa kiafrika ni feki, je wewe unavaa viatu kazini? Unavaa chupi ya kitambaa au ya magome ya miti? kwanini? Mbona umeacha asili yako?

Kusema ukweli sikuungi mkono kudhania ya kuwa mwanamke akiweka nywele za bandia au akipaka mafuta anageuka mzungu feki, nope!

Kinachokuuma wewe ni kumlipia mkeo bill sio? Pole sana ndugu yangu, tunaoa ili tuwahudumie nao watupende. Mimi ninaona ufahari sana kumlipia mke wangu bill bila roho kuniuma. Kwanini ujiite mumewe alafu roho ikuume kumhudumia?

Jipange mkuu, unatupa mashaka na huo uwana zuoni wako unaojitambia
 
mmh! nashindwa kuelewa ni aina gani ya mwanazuoni ama ni aina gani ya mwandishi aliyeandika hapa.
Gaijin kasema sahihi kabisa, kuhusu aina ya uandishi wako istoshe unaposema wanawake wa kiafrika ni """fake"" ukilinganisha na wazungu nashindwa kuelewa.

ni hiyo rangi unayoangalia ama ni urefu wa nywele ama ni nini?? most of the wazunguzi who are well off the do wear make ups being wigs,nails, foundation etc sasa sijui wewe hilo hapo unaliongeleaje.

pia kuna akina dada wangapi ambao wako very natural, despite being educated?? ama wee unatumia kigezo cha kulipa bills ilihali hakuna mama anayefanya kazi na kisha kumwangushia mumewe zigo lote la maisha??

what i know is kwa experience ya nchi niliowah kutembelea ya ulayaa ni kwamba vinywaji kila mtu ananunua kwa mfuko wake kama mko bar, ila cigarettes huwa anaweza akakupa mwebzio mloko kwenye meza moja. but kinywaji kila mtu anajinunulia is this the bill which you are talking about?? lakini pia sina sexperience sana na nchi za ulaya so siwez kusema sanaa ila hiki kidogo nilicho observe i can say.
 
Last edited by a moderator:
1. Mwanazuoni gani hujui kuandika kitu kikaeleweka au kutumia kanuni za uandishi?

( Kanuni za uandishi sio lazima ziwe zile unazo zifahamu wewe hata hivyo point yangu ilikuwa ni kufikisha

ujumbe ambao naamini umeupata na Kama nilicho andika hakijaeleweka nadhani hata usingeweza ku comment )

2. Pia, mwanazuoni wa kweli hawezi kupita akijinadi kuwa yeye ni mwanazuoni kwa sababu kufanya hivyo ni kupingana na dhana nzima ya uanazuoni

( Mimi nimeweza, na kupingana na dhana ya uanazuoni sio dhambi )

3. Huwezi ukawa na neno "wote" ikisha ukawa na neno "hususan", kama ni wote basi ni wote kwa jumla hakuna atokae humo, na kama ni hususan wanawake fulani basi sio wote

(
Mimi nimeweza kutumia neno " wote " kisha nikaongeza na neno " hususani " na nimeeleweka )

4. Fikra na mawazo ya mwanamke wa Kiafrika ni yepi? ..Ni fikra na mawazo yanayo uthamini na kuutukuza uafrika zaidi kuliko uzungu ama utamaduni mwingine wowote.

Mwanamke wa Kiafrika anaongea vipi na wa Kimagharibi anaongea vipi?..
Mwanamke wa kiafrika anaongea kwa staha na adabu kama ambavyo tamaduni za kiafrika zinamtaka mwanamke awe, huwezi kumkuta mwanamke wa kiafrika anatumia maneno kama " what the f**k is this?, who the hell is u" and all that, wanawake wa kimagharibi hawana staha katika mazungumzo yao

Na mwondoko jee? :
Mwanamke wa kiafrika anatembea kwa madaha na maringo, wanawake wa kizungu wanatembea haraka haraka sana as if wanawahi kitu fulani, mwanamke wa kiafrika akitembea namna hii anachukiza sana.

Unataka kutuambia wewe unatembea na kaniki au rubega barabarani au wewe kuvaa mavazi ya kimagharibi ni ruhsa ila akifanya mwanamke ni mwao?
..Mwanamke wa kiafrika hawezi kuuliza swali kama hili kwa sababu limekaa ki brainwashed kupita maelezo.

Umewafanyia utafiti wanawake wangapi ukajua kuwa hawalipi bills? .....Tusibishane katika hili kwa sababu tutakuwa tunapoteza muda tu

Kuna wanaume wanatunzwa na wanawake kabisa itakuwa kulipa bill?
: Hii mara nyingi hutokea kwenye movie za akina Kanumba na kama kweli inatokea basi lazima kuna mwanaume anaye umia hapo kwa sababu mwanamke wa kibongo hawezi kumuhonga mwanaume pesa bila ya yeye kwanza kuhongwa.
 
maisha ni kuchagua hakuna wa kukupangia...,

Different Strokes for Different Folks.. wote tungependa vitu sawa mbona ingekuwa shughuli, by the way wanawake wa Kiafrika unaowatafuta wanaanzia karne gani ? ile ya kuvaa majani matiti nje au ile ya wanawake kazi yao ni kuzaa na kulea watoto? (kumbuka change is inevitable) hata hao wazungu enzi za victorian era ni tofauti na wa enzi za "The Sixties"
 
Mangemaniac
wewe sema njaa yako,ubahili wako ndo vilikuponza ukaoe tasha ha ha mbaya zaidi tasha mwenyewe na yeye njaa.
Umebuuug meeen !!!!
 
pole kwakulishwa kitimoto kila siku ilhali kwako ni kharam umebug meeeeeeeeeeeeeeeeeeen no point of view here kwanza huna hata hadhi yakuoa mzungu wewe
 
Kiongozi LIKUD Unaweza kuwa umesoma saana!na usielemike!! Wewe ni mmoja wao! Unadai uafrica unaupenda sana!! Dada zetu wengi ni 'feki',unapenda vitu orijinal!!, ukijuchunguza vizuri kaka wewe ndie FEKI,
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Sal
Back
Top Bottom