Kwa nini ngeleja nae asisimamishwe?

Najijua

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
1,039
180
Wadau nimefarijika sana na habari kuwa bwana JK amemsimamisha kazi rafiki yake Jairo kwanini na Ngeleja asimfuate?kitendo cha yeye kwenda kumpokea na kumkumbatia ni kulidhalilisha bunge, waziri mkuu na kuonekana kushangilia kosa lilofanyika.

Kwa nini Ngeleja asimamishwe kwa kushindwa kuleta unafaa na maendeleo katika wizara anayo iongoza kwa miaka 4 na zaidi sasa?
 
Kama ni kufukuzwa kwa kumkumbatia, vipi wale wengine walioshangilia?
Na kama ni hivyo basi hakuna atakayepona...
 
Jk sijui anamwogopa nini huyu ngeleja..Jana ametuonyesha live kuwa ameshiriki kwenye hiyo rushwa kwa kumkumbatia fisadi mwenzake jairo..jk akitaka heshima irudi atimue wote hawa.
 
girfriend wangu alikuepo kati ya wanaoshangilia nimemit nae jion tu nkapiga kibuti ka wasemavyo
 
Kwa ngeleja, yeye asubiri maamuzi ya tume iliyoundwa, isipokuwa anaetakiwa kusimamishwa kazi pamoja na Jairo kupisha uchunguzi, ni katibu mkuu kiongozi.
Huyu nae anatakiwa kuchunguzwa.
 
Wadau nimefarijika sana na habari kuwa bwana JK amemsimamisha kazi rafiki yake Jairo kwanini na Ngeleja asimfuate?kitendo cha yeye kwenda kumpokea na kumkumbatia ni kulidhalilisha bunge, waziri mkuu na kuonekana kushangilia kosa lilofanyika.

Kwa nini Ngeleja asimamishwe kwa kushindwa kuleta unafaa na maendeleo katika wizara anayo iongoza kwa miaka 4 na zaidi sasa?
Si ngeleja pekee na hawa wafuatao ni wakutimua kazi
1.mh. Ludovick Utoh-kwa kumsafisha Jairo.
2.Luhanjop kwa kumsafisha Jairo.
3.Wafanyakazi wote Wizara ya Ngeleja--kwa kusukum gari la mwizi
NB. Huku kwetu mwizi anauwawa, hapewi hata sekunde ya kujitetea, wao wana mshangilia mwizi.
 
Bishop Hiluka usiodandie hoja soma hoja yote na uelewe hoja sio kumkumbatia wewe
 
ngeleja nae si lolote Bunge limwajibishe
Huyu anafanya mambo anayotumwa na wakuu wake
 
Jairo mwenyewe hajasimamishwa, bali amepewa likizo terms zingine za ajira zipo palepale. ccm wanatuchezea sinema za kihindi
 
Kwa nini Ngeleja asimamishwe kwa kushindwa kuleta unafaa na maendeleo katika wizara anayo iongoza kwa miaka 4 na zaidi sasa?[/QUOTE]

Kwa sababu huo sio utaratibu wetu. Mtu akipewa uwaziri hapimwi utendaji wake. Anaachwa tu hata kama hakuna analofanya, alimradi hajakorofisha wakubwa atakaa miaka yote mitano raha mustarehe!
 
Nilibahatika kumuona Waziri mmoja zezeta wa serikali legelege akimkumbatia Jairo, katika kutafakari sana nikagundua alikuwa anafurahiya jinsi alivyojipatia milioni 4 kiulaini bila bughuza yoyote. Kisha nikawaona mazezeta wenzake wa wizara ya unyang'anyi wakilisukuma gari alilopanda yule mwizi nikajua tu tayari uchakachuaji wa ripoti umefanyika kwani zile milioni kazaa ambazo hazionekani watakuwa wamezigawana. Kisha nikajiuliza hivi JAIRO na LUHANJO ni mtu na mdogo wake????? Jibu likawa jepesi " Ndiyo wote wezi". Tusubiri tuone sarakasi inayokuja kwani tunasikia wameficha ushahidi ili Kamati ya Bunge isipate vielelezo muhimu.
 
Tuache unafiki, Luhanjo anafanya kazi ofisi ipi na kikwete naye ofisi ipi. lao moja! Tumeliwa Mpaka 2015 na twiga wote uarabuni kwenye tanzania mpya.
 
Ngeleja anatakiwa kujiuzulu! Amedanganya watanzania kwa umeme wa wiki 2 ili bajeti ipitishwe baada ya kupata alichotaka mgao umerudi full swing! Hapa tulipo vichwa vinauma sababu ya kelele za generator maana kila nyumba inaungurumisha lake!
 
Ndani ya GAMBA hakuna wakuachwa kuanzia JK hadi Cabinet yake wote waachie ngazi nani anasema JAIRO kafukuzwa hata kama kamati itamfukunza JAIRO anaweza akapewa ubalozi. Ule ufisadi ni ngazi ndefu ya wakubwa na hayupo peke yake sasa ndio hao wengine wananitokeza. majibu Luhanjo ndio ya Raisi baada ya kutoka AFRIKA YA KUSINI hawa wote ni wasanii.
 
Wadau nimefarijika sana na habari kuwa bwana JK amemsimamisha kazi rafiki yake Jairo kwanini na Ngeleja asimfuate?kitendo cha yeye kwenda kumpokea na kumkumbatia ni kulidhalilisha bunge, waziri mkuu na kuonekana kushangilia kosa lilofanyika.

Kwa nini Ngeleja asimamishwe kwa kushindwa kuleta unafaa na maendeleo katika wizara anayo iongoza kwa miaka 4 na zaidi sasa?
kwa taratibu za kiutawala: ngeleja na jairo wote ni uteuzi wa raisi hivyo kila mmoja hapa atahukumiwa kwa dhambi yake. jairo angelikuwa ameteuliwa na ngeleja wote wangepaswa kusimamishwa kazi. vyenginevyo ngeleja asimamishwe kwa kosa la kwake binafsi na si la jairo ambaye ndiye mtendaji mkuu wa wizara. ngeleja ni mtendaji mkuu wa wizara kisiasa na si utendaji..... ie why mwenye mamlaka ya kumsimamisha kazi jairo amekuwa raisi na si waziri wake...
 
Back
Top Bottom