Nimefanya utafiti wa kina nikagundua kuwa ile mikoa ambayo watu wake ni maskini ndio wapenzi na washabiki wa ccm. Kwa mfano Pwani, Morogoro, Dodoma, Tanga, Mtwara, singida na zingine kama hizo. Lakini angalia Mikoa inayoisapoti Upinzani kama Arusha, Mbeya, Mwanza, Dar es salam na Kigoma watu wake walivyokuwa vizuri kielimu na kiuchumi. Sasa hebu tujiulize ni kwa nini hawa watu wa mikoa iliyoko chini kiuchumi wanaishabikia ccm wakati majimbo yao ndio yako mwisho kwa maendeleo?. Na hawa watu ni juhudi gani itumike kuwakomboa kutoka kwa makoloni ccm?.