Kwa nini Mijadala ya CHADEMA hapa huwa haikisaidii CHADEMA?

Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
5,565
Likes
24
Points
135
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
5,565 24 135
Nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa JF inachokihusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), lakini mijadala hii mara nyingi imekuwa ikiishia kwenye Malumbano, watu kuitana Majina ya Ajabu ambayo naamini kabisa kama tungekuwa tunatumia majina yetu halisi basi ni wazi wakati mwingine huwa tunawatukana hata Baba zetu.
Nimejaribu kuwa mfwatiliaji (Kuliko Mchangiaji) katika hizi mada na nimefanikiwa kugundua ni kwa nini basi hii mijadala haina Manufaa kwa CHADEMA wala kwa Taifa

1: Mijadala mingi ya JF Imejenga makundi makuu mawili na sasa hata hiyo mijadala imekuwa na Mabishano na Matukanano kati ya hayo makundi Mawili ( Mimi nawaita Watu wazima Hovyo)

2: Kuweko kwa makundi hayo Mawili kumesababisha baadhi ya Member Makini wa JF kutochangia hiyo Mijadala kwa kuogopa kuwekwa katika moja ya hayo makundi na kwa sababu watu wengi wamekuwa wakichangia kimajungu na kivisa.

3: Makundi hayo ni

1: Zitto Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Zitto ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa hata Mwanachama wa CHADEMA. Kundi hili limekosa support ya Member wa JF ambao kwa michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM ( Chama ambacho kwao ustawi wa CHADEMA ni tishio la Maisha na Ulaji wao)

2: Mbowe Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Mbowe ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Kundi hili ( Sijui ni Bahati Mbaya au Nzuri) linaungwa mkono na Member wengi kama si wote ambao kutokana na Michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM damu (Chama ambacho Maslahi na Ustawi wake unategemea zaidi na namna gani uongozi wa CHADEMA uko, eidha weak au strong)mfano Dar Es Salaam, Malaria Sugu, JayKey na wengine wengi tu.Lengo la kuweka hii topic ni kuwafanya Wana CHADEMA wote makini ( Namaanisha wale wanaoamini kwamba Chama hakijengwi na Mtu Mmoja) kupima na kuangalia juu ya ama kuchangia ama kuipuuza mijadala yeyote inayolenga kuvunja umoja na Mshikamano ulioko ndani ya Chama

Asanteni
 
omarilyas

omarilyas

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2007
Messages
2,127
Likes
6
Points
0
omarilyas

omarilyas

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2007
2,127 6 0
Jibu ni kuwa kwa sababu imelenga kushambulia watu ama kumwaga chuki na fitina dhidi ya watu na wakitegemea kuwa kwa kuwa wengine ni waungwana basi hawatajibiwa na hivyo propaganda zao zitafanikiwa.

Ukweli ni kuwa hivi sasa katika Chadema kuna makundi mawili ambayo yanawakilishwa na personalities mbalimbali. Lakini makundi hayo yamegawanyika kifikira, kimikakati na kiitikadi. Tatizo ni kuwa wengi wanaoleta mijadala inayohusu Chadema ni wale ambao wanaamini katika siasa za chuki na fitina ili kufanikisha maslahi yao kisiasa. Na wengi wao bahati mbaya ni maadui wa ukweli na siasa za hoja hivyo ili kutuwaacha wakahodhi ushawishi wa umma kama ambavyo wamekuwa wakifanikiwa hapo kabla, ni wajibu wetu wengine kuingilia na kupambana nao katika platform wanayoielewa.

Hayumkini ni juzi tu hawa watu wanakutanishwa kutafuta suluhu kwa maslahi ya chama leo linatokea gazeti lao linaendeleza siasa majitaka halafu utegemee watu wengine waendeleze ustaarabu wa kuwanyamazia......

Ukweli ni kuwa maadui wa Chadema ni wao wenyewe ama kwa kukosa upeo wa kisiasa miongoni mwa viongozi wao ama kwa wale wengine washabiki ni kuamini katika siasa za chuki kiasi cha kukosa UTU kama walivyonyesha hivi karibuni.

Na mbaya zaidi haya yanayoandikwa sio kuwa yanatoka kwa Kubenea Mwenyewe isipokuwa anatumika na viongozi wa Chadema na ni hao ndio wanaongoza katika kuleta haya humu na kuyashabikia.......
 
T

tufikiri

Senior Member
Joined
Nov 26, 2010
Messages
156
Likes
0
Points
0
T

tufikiri

Senior Member
Joined Nov 26, 2010
156 0 0
Nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa JF inachokihusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), lakini mijadala hii mara nyingi imekuwa ikiishia kwenye Malumbano, watu kuitana Majina ya Ajabu ambayo naamini kabisa kama tungekuwa tunatumia majina yetu halisi basi ni wazi wakati mwingine huwa tunawatukana hata Baba zetu.
Nimejaribu kuwa mfwatiliaji (Kuliko Mchangiaji) katika hizi mada na nimefanikiwa kugundua ni kwa nini basi hii mijadala haina Manufaa kwa CHADEMA wala kwa Taifa

1: Mijadala mingi ya JF Imejenga makundi makuu mawili na sasa hata hiyo mijadala imekuwa na Mabishano na Matukanano kati ya hayo makundi Mawili ( Mimi nawaita Watu wazima Hovyo)

2: Kuweko kwa makundi hayo Mawili kumesababisha baadhi ya Member Makini wa JF kutochangia hiyo Mijadala kwa kuogopa kuwekwa katika moja ya hayo makundi na kwa sababu watu wengi wamekuwa wakichangia kimajungu na kivisa.

3: Makundi hayo ni

1: Zitto Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Zitto ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa hata Mwanachama wa CHADEMA. Kundi hili limekosa support ya Member wa JF ambao kwa michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM ( Chama ambacho kwao ustawi wa CHADEMA ni tishio la Maisha na Ulaji wao)

2: Mbowe Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Mbowe ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Kundi hili ( Sijui ni Bahati Mbaya au Nzuri) linaungwa mkono na Member wengi kama si wote ambao kutokana na Michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM damu (Chama ambacho Maslahi na Ustawi wake unategemea zaidi na namna gani uongozi wa CHADEMA uko, eidha weak au strong)mfano Dar Es Salaam, Malaria Sugu, JayKey na wengine wengi tu.Lengo la kuweka hii topic ni kuwafanya Wana CHADEMA wote makini ( Namaanisha wale wanaoamini kwamba Chama hakijengwi na Mtu Mmoja) kupima na kuangalia juu ya ama kuchangia ama kuipuuza mijadala yeyote inayolenga kuvunja umoja na Mshikamano ulioko ndani ya Chama

Asanteni
Safi sana wewe ni miongoni mwa watu wenye upeo wa kufikiri katika hili jamvi. Achana na hao wanaocomment hata yale ambayo hawana upeo nayo. Sisi kama kweli tunataka kujadili mambo kwa ajili ya kuleta maendeleo na mabadiliko katika maisha, tunatakiwa tuondokane na SIASA ZA MHEMKO ambazo hutokana na kuangalia NANI ANAONGEA na sio NINI ANAONGEA.
 
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Messages
5,565
Likes
24
Points
135
Albedo

Albedo

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2008
5,565 24 135
Ni uamuzi wao ( Zitto Haters au Mbowe Haters) waendelee na Siasa zao za Maji taka, hizi ni Siasa za Majungu ambazo cha kusikitisha sana zimekuwa zikiwekewa Gasoline na CCM
 
Mohamedi Mtoi

Mohamedi Mtoi

R I P
Joined
Dec 11, 2010
Messages
3,325
Likes
51
Points
0
Mohamedi Mtoi

Mohamedi Mtoi

R I P
Joined Dec 11, 2010
3,325 51 0
Nimeaona mantiki nzuri sana kwa aliyeleta hoja hii! Hongera sana kaka kwa kuliona hilo. Binafsi huwa sipendi kuchangania mijadala inayoonyesha utume wa mtu mmoja kuwa yeye ndio kila kitu kama jinsi ulicvyo eleza hapo juu! Kuna jamaa mmoja alishawahi kusema kama huna la kusema heri kunyamaza kimya kuliko kuliko kuongea shudu zisizo na mashiko hata kwa watoto wa chekechea.

Naomba kuwasilisha.
 
P

Paul S.S

Verified Member
Joined
Aug 27, 2009
Messages
5,935
Likes
303
Points
180
P

Paul S.S

Verified Member
Joined Aug 27, 2009
5,935 303 180
Mkuu tatizo lingine ni kuwa hao wenyewe mbowe na zitto hawaivi chungu kimoja
 
Brooklyn

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
1,461
Likes
55
Points
145
Brooklyn

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
1,461 55 145
JF ni jamvi huru na lisilofungamana na chama chochote ingawa ukifuatilia mijadala mingi ya kisiasa inayojadiliwa hapa JF inaonyesha majority of members ni wafuasi wa Chadema. Hii inadhihirishwa na jazba ambazo mara nyingi members hao wanazionyesha especially kwa watu ambao wanamuelekeo wa kusupport vyama kama vile CCM, CUF na NCCR Mageuzi.

Yeyote anayepinga ama kuonekana akitoa hoja zinazokinzana na members hao (wafuasi wa chadema) wamekuwa wakiporomoshewa maneno ya kejeli na wengine kwenda mbali zaidi na kutoa maneno ya matusi na kashfa.

.........fuatilia response ya huu mchango wangu utaamini nikisemacho..!!
 
Narubongo

Narubongo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
1,953
Likes
85
Points
145
Narubongo

Narubongo

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2010
1,953 85 145
Mimi nipo chadema sina kundi na ni muelewa wa mambo huwa sitoi maamuzi kwa kushawishiwa na mtu, huwa naangalia nakupima mwenyewe na kutoa maamuzi yangu kuhusu zitto(si hapa JF) nilijikuta tu nikipigwa butwaa baada ya kuingia tume ya madini... ninaukubali uongozi wa mbowe chadema 100% mtanzania si mtu wa kufanya nae kazi kwa kumkenulia meno..
na hayo makundi ya haters unayozungumzia hayapo chadema Zitto akifanya mazuri huwa anapongezwa sana tena sana hapa JF na kila mtu ukiondoa wanaccm na akienda sipo huwa tunampa ukweli na si kueneza chuki bado sijaona kauli tata za mbowe
 
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Messages
7,283
Likes
16
Points
135
Kachanchabuseta

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2010
7,283 16 135
Nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa JF inachokihusu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), lakini mijadala hii mara nyingi imekuwa ikiishia kwenye Malumbano, watu kuitana Majina ya Ajabu ambayo naamini kabisa kama tungekuwa tunatumia majina yetu halisi basi ni wazi wakati mwingine huwa tunawatukana hata Baba zetu.
Nimejaribu kuwa mfwatiliaji (Kuliko Mchangiaji) katika hizi mada na nimefanikiwa kugundua ni kwa nini basi hii mijadala haina Manufaa kwa CHADEMA wala kwa Taifa

Mijadala mingi ya JF Imejenga makundi makuu mawili na sasa hata hiyo mijadala imekuwa na Mabishano na Matukanano kati ya hayo makundi Mawili ( Mimi nawaita Watu wazima Hovyo)

2: Kuweko kwa makundi hayo Mawili kumesababisha baadhi ya Member Makini wa JF kutochangia hiyo Mijadala kwa kuogopa kuwekwa katika moja ya hayo makundi na kwa sababu watu wengi wamekuwa wakichangia kimajungu na kivisa.

3: Makundi hayo ni

1: Zitto Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Zitto ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa hata Mwanachama wa CHADEMA. Kundi hili limekosa support ya Member wa JF ambao kwa michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM ( Chama ambacho kwao ustawi wa CHADEMA ni tishio la Maisha na Ulaji wao)

2: Mbowe Haters: Hawa ni wale ambao wanaona au wanadhani kwamba Mbowe ndiye hasa Tatizo kubwa lililopo katika chama na ni Mtu ambaye hafai kabisa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Kundi hili ( Sijui ni Bahati Mbaya au Nzuri) linaungwa mkono na Member wengi kama si wote ambao kutokana na Michango yao wanafahamika kabisa kwamba wao ni CCM damu (Chama ambacho Maslahi na Ustawi wake unategemea zaidi na namna gani uongozi wa CHADEMA uko, eidha weak au strong)mfano Dar Es Salaam, Malaria Sugu, JayKey na wengine wengi tu.Lengo la kuweka hii topic ni kuwafanya Wana CHADEMA wote makini ( Namaanisha wale wanaoamini kwamba Chama hakijengwi na Mtu Mmoja) kupima na kuangalia juu ya ama kuchangia ama kuipuuza mijadala yeyote inayolenga kuvunja umoja na Mshikamano ulioko ndani ya Chama

Asanteni
Ni uamuzi wao ( Zitto Haters au Mbowe Haters) waendelee na Siasa zao za Maji taka, hizi ni Siasa za Majungu ambazo cha kusikitisha sana zimekuwa zikiwekewa Gasoline na CCM

Personal attact
PERSONAL ATTACK
PERSONAL ATTACK
 
Forum statistics

Threads 1,238,322
Members 475,877
Posts 29,316,122