Kwa nini MANDELA na sio NYERERE ???

Kwa nini MANDELA na sio NYERERE ???

Free ideas

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
3,508
Reaction score
2,060
Mwaka 1999 Oktober 14,wakati BABA mwasisi wa Taifa hili (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere)anafariki,nikiwa na umri wa miaka 12,tena mwanafunzi wa Primary niliona ni tukio ambalo ni kubwa lililowagusa watu wengi sana Duniani kote.,vilevile mazishi yake yalikusanya viongozi wengi kutoka Afrika na kila pande ya Dunia.


Kwa kuwa pia mwalimu wangu wa Primary enzi hizo Pale Nyarigamba primary school, alitusimulia hadithi nyingi kuhusu baba wa taifa niliona alistahili heshima ile wakati ule.Niliamini kabisa baba wa taifa alikuwa na mchango mkubwa sana katika kuiletea nchi hii Uhuru lakini pia alishiriki vyema sana katika Kuzikomboa nchi nyingi za afrika baadhi zikiwa,Msumbiji,Angola,Zimbabwe,Afrika kusini,Namibia,Malawi na n.k.alijitoa kusafiri kila kona na Hata kwenda UNO ya enzi hizo kuwaambia wazipe uhuru nchi za Afrika.Hakika alikuwa shujaaaa aliyediriki na akaweza,

Wakati vugu vugu hilo la uhuru likiendelea katika nchi mbalimbali,viongozi wengine walipitia wakati mgumu ikiwa ni pamoja na kufungwa jela kwa miaka kadhaa ama kuuwawa kabisa.Hapa ndipo tunapompata shujaa mwingime wa Afrika NELSON MANDELA,(RIP)aliyefungwa miaka 26 na miez 9~27 jela na kutolewa na kuendelea na shughuli za ukomboz wa SOUTH AFRICA.,

Lakini hawa ni akina nani??...
J.k Nyerere,...,

Rais wa kwanza wa tanzania Huru,aliyepata elimu ya kikoloni na kufanikiwa kupambana na kuiletea ardhi yetu uhuru bila kumwaga damu.
Kiitikadi Nyerere alikuwa msocialist/mkommunist aliyeamini katika ujamaa na kujitegemea,Baada ya uhuru aliwafukuza wazungu na kuwaita wanyonyaji(mabeberu),hakika walikuwa wanyonyaji ambao hawakutakiwa kwa wakati ule.Alifariki jumatano tarehe,1 Oktober 1999 japo ilitangazwa rasmi tarehe 14,

Mandela....,,
Mpigania uhuru katika taifa la kusin kabisa mwa Afrika lakini pia ndiye rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo.katika harakati kupinga utawala wa wadachi bahat mbaya anafungwa jela muda mrefu.
Kiitikadi ni msocialist aliyebadili msimamo baada ya kutoka jela.amefariki mwaka huu 2013,na kuzikwa na viongozi wa kila pande duniani na kutangazwa SHUJAA WA AFRIKA!!!,,bendera za nchi mbali mbali kubwa zikipepea nusu mlingoti na vyombo vya habar dunia nzima vikiripoti kifo chake!!,

Haya tuendeleee hapa chini...,


Lakini kwa nn Mandela na sio Nyerere??....

Kosa la Nyerere kwa wazungu..,kitendo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa bega kwa bega na nchi za kisocialist kama ,RUSIA,CHINA,CUBA,INDIA,VIETINAM n.k katika harakat za ukombozi niliwakera na zilimfanya asikubalike kwa maana kama mtakumbuka kipindi hiki kulikuwa pia na vuguvugu la vita baridi kati ya RUSIA na USA.pili kitendo chake cha kukataa Capitalism system of Govment ilimuongezea maadui hasa magharibi kwa kuwa lengo la kutoa uhuru ilikuwa ni kufanya Neo-colonialism.
Pamoja na mengine mengi mwalimu nyerere alionekana kikwazo katika matakwa ya wamagharibi na hivyo kutopewa umuhim sana katika historia yao.



Kwa nn mandela,..
Mwanzo wakati Nelson hajaenda jela alikuwa na simamo sawa na wa Mwalimu Julius Kambarage.Lakini alipotoka jela alikuwa na ,mtazamo tofauti.Baada ya kutoka jela mzee madiba alieneza siasa ya kutokubaguana,.lakini je,sera hii alijifunza jela??,nn kilimsukuma kubadili msimamo?.ni maswali ambayo kama ningejaaliwa kukutana nae baada ya salam ningemuuliza.Kwa haraka hataka tunaweza sema kwamba inawezekana aliona wingi wa wazungu kule bondeni pamoja na Investment zao akaona ngoja niwaache...,lakini kwa nn awaache adui zake waliomfunga jela kirahisi hivo.,

Ninacho amini mimi,..
Mzee madiba alipewa misingi na jinsi ya kutawala atakapotoka jela.Aliambiwa asithubutu kuwafukuza wazungu na aliambiwa atangaze siasa ya kutokubagua.Na kama angekwenda kinyume na hapo asingeeleweka kwao.kwa hiyo binafsi naamini kwamba mzee madiba alipangiwa nn cha kufanya na kamwe sio kwa matakwa yake. Jela za enzi hizo zilikuwa sio mchezo,ukiambiwa tunakutoa jela pia tunakuandaa kula raisi lakini lazima ufanye moja..,mbili..,tatu utakataaa??,,una miaka hujaona familia!!,,nisiende mbali sana ila nadhan mmenielewa....

Kwa nn Nyerere ni zaidi..,

Mwalimu julius kamabarage Nyerere alisimamia msimamo wake mpaka anakufa!!,hakusalim amri kamwe kwa mabeberu hata hali ilipokuwa mbaya japo alienda kuomba msaada wakampa masharti manne,1.kupunguza idada ya mawazir
2.kukubal capitalism 3.kushusha thamni ya fedha(shilingi) mbele ya dollar
4.kukubali privatision(uwekezaji).
Hata marekani na uingereza walipoitumia Uganda kuanzisha vita dhidi ya tz ili uchumi uyumbe waje kuwekeza bado baba wa taifa alidinda.
Kwa sifa hiz pamoja na nyingine nyingi Mwalimu kambarage ni bora kuliko Nelson Mandela,lakini madiba anakuja kuwa bora zaidi machoni pa mabeberu kwa kuwa Hajakwamisha interest zao.Ndo mana leo tunaona dunia nzima inaomboleza hadi kushusha bendela nusu wakimwita mzee NELSON MANDELA SHUJAAA!!! wa AFRIKA!!,huku nyerere akibaki kuitwa raisi wa kwanza wa tanzania!!,TAFAKARI!!ila usichukue hatua!!,


Asanteni kwa kusoma,kumbuka n mawazo yangu tu ,sijakopi na kupesti,waweza kukosoa ama kusapoti,,
From Free ideaz
 
Back
Top Bottom