Kwa nini JF inaandamwa hivyo?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,119
2,000
Wakuu, tumesikia kesi aliyofunguliwa mwasisi wa JF. ukiitafakari kwa kina makosa aliyoshtakiwa utabaini kuwa serikali inahofu kubwa hasa kwa vijana kuungana kuyapinga yale wanayoyafanya. baadhi ya mambo ambayo nahisi yanawachanganya ni
1. usitishaji wa ajira za walimu wa sanaa. hawa wako wengi mtaani hivyo wakiamua kuungana na kutoa kilio chao hadharani, serikali ya JPM itaingia doa. moja ya mtandao unaoweza kuwakutanisha kwa haraka ni JF.

2. Kupotea kwa Ben Saanane. hili nalo nadhani ni miongoni mwa sababu za kutaka kuifungia JF. wanaopost humu ndani wengi hutumia nicknames so huwezi kuwatambua. Inamaana miongoni mwa wanaoshiriki uovu wana Id zao humu so hata wakiamua kumwaga mboga hakuna anayeweza kuwatambua. (rejea issue ya madawa ya kulevya iliyomkumba mtoto wa ..... huko China). watu wasiporidhika watamwaga mboga na serikali itaingia doa. kukwepa hilo inabidi JF ifungwe. tumeona mpaka matokeo ya mtoto wa sizonje yakipakuliwa humu humu JF pamoja na kudisco kwake. watawala hawaitaki hii aibu.

3. kuminywa kwa demokrasia. vyama vya siasa tayari vimebanwa koo kwa stairi Fulani ilhali wenye serikali wanapeta na kijani yao. Wanaharakati wote kimyaa pamoja na asasi zisizo za kiserikali. ukifungua mdomo yakukuta ya Lema (pole sana kamanda) na Ben. Sehemu pekee iliyokuwa imebaki ikiwa huru kwa watu kumwaga yanayowasibu mioyoni ilikuwa JF. sasa watawala hataki hii kitu iwepo hivyo lazima wapambane kuuzima huu mtandao wa JF.

Pole sana Max kwa Yale unayoyapitia sasa Mungu akutie nguvu na awadhoofishe watesi wako. Jamiiforums ikifungwa hatutakuwa na haya majukwaa ambayo wengi wetu tumeshayazoea kupata taarifa mbalimbali za yanayojiri nchini, ajira, matokeo, nk

ACHA TUISOME NAMBA - huu wimbo inatakiwa uwe wimbo bora wa mwaka
 

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
50,946
2,000
Tatizo la kila kitu ni hii laana tuliyoipata hapo ikulu.
Yani yeye akili fupi anadhani wanaomzunguka ndio nchi nzima.
 

Kibo255

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
4,408
2,000
Ukweli hawataki watu wajue ukweli
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom