Ukuzwaji wa uchumi jumuishi mkuu...kuwa na matajiri kama kina Lugumi, kuna paralyze uwezo wa ujumla, ukiangalia wengi wanaosumbua huko mitaani ni mtindo wa kina Lugumi...huu ni mfano, sina kijicho na mtu wenu.
Tuliwahi sikia watu wanaficha fedha nje, tumesikia jinsi gani watu wananunua majumba Dubai, tumesikia jinsi gani wanasiasa na watumishi wa umma wanavyoweka fedha zao kwenye ardhi, majumba na hizi bonds za serikali kuficha wizi wao, sasa tuchukulie mfano mmoja tu;
- Inasemekana mtumishi mmoja wa serikali miaka ile ya Msoga, alikutwa na trilioni 3 shilingi kazihifadhi Bondeni.
- By that time, budget ya nchi haikuwahi kufika trilioni 20 kwa mwaka na bado haikuwa inakamilishwa kwa mwaka.
- Huyu ni mtumishi wa umma, mwenye mshahara wa chini ya sh 5m kwa mwezi, anayetumikia ajira 9hrs a day, 23day a month, anawezaje kuzalisha kiwango hicho cha pesa?
- Na kama ni kiwango anachoweza kuzalisha kwa shughuli za pembeni, kwanini aendelee na ajira isiyompa hata tzs 100m tu kwa mwaka kihalali?
Sasa, kama angewekeza hizo trilioni 3 nchini, tena nadhani dolari ilikuwa chini ya 2000; unadhani angesisimua uchumi kiasi gani?
- Taasisi ya moyo imejengwa na kukamilishwa kwa chini ya bilioni 60 tzs, tena kwa bei ya kiserikali, unadhani angejenga ngapi za kibiashara?
- Benjamin Mkapa, iligharimu tzs 51b, angejenga ngapi na kutoa ajira?
- Kama ni shule au vyuo, angekuwa navyo vingapi?
- Mitandao mitatu mikubwa ya simu TZ kwa miaka ile ilikuwa inapata turnover ya tzs 585bn kwa pamoja kwa mwaka, hii ni ⅙ ya fedha yake.
- Dangote, unadhani amewekeza ngapi kwenye kiwanda cha cement, tzs 1.8t na kutoa ajira lukuki.
- Bajeti za wizara nyingi kwa mwaka zilikuwa chini ya 1trilion, ya ulinzi pekee ndo ilikiwa 1.2t, Zanzibar ikiwa na bajeti ya chini ya 600b by then.
Sasa, unaona hizo fedha ni za umma, zimepigwa na fala mmoja na hazitumii sasa, kaziweka Bondeni ambapo benki ile, inazikopesha kwa watu wao ili kusisimu uchumi wa huko huku yeye akikatwa service charge ya kuhifadhi mzigo huo.
Wamelo wa namna hii wako wengi sana, tunaona na hatuna la kufanya, ila jua ndo wanadhulumu haki na nguvu za hao wanaoonekana wajinga na wasio na juhudi za kujishughulisha....
Kama serikali ikipata wazalendo na wenye maadili, kila kitu kitakuwa bora, kwa nchi masikini kama hii, maendeleo ya mtu mmoja mmoja hayana impact yeyeto hata mtu mhusika...ila maendeleo ya vitu yana impact kwa watu wengi.
Serikali zalendo;
- Itajenga shule bora kwaajili ya wengi, sio wachache kama ilivyo sasa, mtoto wa Nchemba anasoma Fedha, ila anasisitiza watoto wa wengine kusoma bure kule kusiko hata na madawati.
- Itajenga hospitals
- Itaboresha miundombinu, hakuna wa kulala njiani kwenda Kigoma au Mwanza, lakini hakuna sababu ya kutembea na private vehicle kama kuna SGR-300kph, Dar - Kigoma ni 6hrs tu.
- Umeme hautakuwa issue, mbwinde ndani mdani huko wanaangaza, wanasaga, wanahifadhi samaki n.k
- Inapambana na magonjwa kwa kuwa na research centers, hospitals etc
- Teknolojia inakuzwa kuendana na wakati
Mambo ambayo mtu binafsi hawezi fanya kwaajili ya wengi.
Uchumi jumuishi unajenga na serikali adilifu na zalendo...sasa kama WASIOJULIKANA tu wameshindikana, hao wenye matrilioni itakuaje?