Kwa nini jamii inayokuzunguka wewe ni masikini?

Umasikini ni (man made) unasababishwa na binadamu.

Haya maisha ilibidi watu wawe stressful kuvumbua mambo mbalimbali yatakayoipaisha dunia

Na sio watu kuhangaika kutafuta Chakula End meet , n.k

Kwa kutumia rasimali Kama Ardhi , Bahari , maziwa , misitu kila mtu angeweza kula , kunywa na kubakisha ziada.

Ila kinachotokea kunakuwa limitations of resources , kwamba watu wachache wanamiliki vitu vingi na wengi wanakosa.

Mfano mdogo tazama MTU Kama Job Ndugai amekuwa Mbunge over 20 years amekuwa Speaker n.k Ila bado hachoki anataka na mwaka huu arudi bungeni .

Au mtazame Mwampossa pesa alzonanzo na umri wake means anaweza kula mpaka anakufa Ila bado anawakamua watu sadaka.

Njoo katika jamii zetu unakuta MTU ana kila kitu Ila bado anamtapeli MTU ambaye hana chochote .

Je hii utaisemaje au utahiitaje?.

Means accumulation and distribution haipo sawa .

Mambo Kama uvivu , ni nadharia ambazo zimetengenezwa kuhalalisha kuiweka dunia kukosa usawa.
kanda ya ziwa wakikuona una maisha mazuri wastani na unakula vizuri , jiandae kuitwa majina yote mara taperi, jambazi au freemason...... tena wakiona huyumbi kiuchumi na kila siku unazidi kupaa jiandae kuwa na maadui kila kona
 
Hao wanahitaji plan Bs.Kazi za ziada kuwaongezea vipato vyao.Changamoto yao walio wengi ni kukata tamaa na kuzidisha matumizi yasiyo ya lazima kwenye "kuoa wake wengi",kamari,kutoweka malengo/akiba hata kama ni kidogo,kuwa na familia kubwa,kutojibidiisha kuongeza elimu na kuyaona maisha nfiyo kama yalivyo tu kwa mazoea.
Mkuu, kinadharia ndivyo inavyoelezeka, uhalisia ni mpaka uwe umepitia magumu hayo kisha uchomoke ndo unaweza sema lolote.

Unapata kipato cha sh 7,000 kwa siku, kabla ya chakula, nauli etc. Hapo, ni saa 1 asbh mpaka saa 12 jioni; anajiongeza vipi huyu na yuko mjini Dar, ana mke na mtoto mmoja, amepanga!
  • Hana muda wa kujaribu ila kulisha na kuilinda familia kila siku
  • Umri ulishaenda, huwezi sema kwanini ana familia
  • Tsh 7000 kwa siku, unaweka akiba ngapi?

Assume, kima cha chini ni tsh 500k, wastani wa sh 16,000 kwa siku, hawa bila viposho posho na wizi wa hapa na pale, nanga haipai...sasa wa 7k kwa siku anatoboaje?
  • Mkuu, kumbuka, kadiri ujira unavyokuwa mdogo ndivyo masaa ya kazi yanavyobana kwa kazi za shuruti.
  • Huyu mtu, hawezi kupewa mkopo wa 15m na taasisi za kifedha
  • Nchi yetu tunategemea zaidi cash tofauti na nchi nyingi...unakopa cash, ndo ulipe gari kisha wanakukata monthly, hakuna hata grace period kwa vimikopo hivi.
  • Elimu unaongeza wakati gani? Walioko serikalini tu wa kiwango hicho cha mshahara ndo wanayo nafasi ya kuongeza elimu na hapo ni kwa tabu sana akifikiria masuhuli yanakata. Zaidi, qualification za wao kuajiriwa, ni kwasababu wamekosa vigezo vya kuendelea na elimu ya juu, wafanyaje sasa, waende veta?
  • Angalia uaskari, wanachukua kuanzia pointi 28 kuendelea kwa hawa wasiokuwa na majukumu ya kufikiri...na vyuo hamtaki hizo pointi, afanyaje?

Kwa hali ya umasikini wa nchi, huwezi kuwa Mfanyakazi, Mfanyabiashara na Mkulima kwa pamoja, haiwezekani asilani ISIPOKUWA tu kama una nafasi ya wizi, ufisadi n.k
  • Wengi wafanyakazi wanadanganya kufanya biashara kwakuwa wana-inject pesa zisizowekeka benki kutoka kwenye ajira zao, siku wakipigwa chini, unaona na biashara zinayumba na nyingine kufa kabisa.
  • Wafanyabiashara 100% wanaofanikiwa pakubwa ni wale wakwepa kodi pakubwa na biashara za nyuma ya pazia...
 
Nini kifanyike katika kumsaidia mtu kama huyu?
 
Nilimsaidia mama jirani yangu, akiwa mgonjwa nikamchukua na kumuuguza.
Mama asimuite kijana wake aje anidange 😹😹
Ila wazaramo wanapenda kitonga balaa.
Nikawatimua wote mama na mtoto..!!

Huyo mkaka sasa anaongea km chiriku, ujuaji, alikua anajituma mpk mbwa anaogesha 😹😹
Nikasema wewe mimi sio Vick wa Prof Jay hakuna ZALI LA MENTALI HAPA katafute kazi..!!
 
Wewe ulimpa samaki, badala ya kumfundisha kuvua samaki.
 
Mi nilitoa msaada wao ndo wakazingua, wangeacha upuuzi ningemtafutia hata connection ya kazi kijana wake.

Ajabu akataka kunimiliki kisa wameona niko single, sasa mkinga na mzaramo wapi na wapi? 😹😹🤣
Kama uko singo ngoja nipambane nije nikumiliki, una roho nzuri sana.
 
Tatizo kubwa haswa kwa nini jamii fulani ipo nyuma kimaendeleo na wengine wana maendeleo mazuri, tunaweza kusema ni mgawanyo wa hali ya kimaisha, ubinafsi, ujinga na umaskini wa ujumla katika taifa.
 
Ni nini kifanyike ili na wao wawe na maisha mazuri?
 
Back
Top Bottom