Kwa nini hii ni zaidi kwa wanawake ?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini hii ni zaidi kwa wanawake ?!

Discussion in 'JF Doctor' started by DAWA YA SIKIO, Jan 21, 2012.

 1. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hili eneo ninaloishi liko mbele sana kwa ku 'export' vijana wasichana kwa wavulana kwenda kufanyakazi za ndani,mara nyingi Dar,Arusha na Moshi.
  Kinachonishangaza baada ya muda fulani vijana hao wanaporudi pengine likizo au kuacha kazi,wasichana wengi huonekana kubadili lafudhi kufuata ya kule walikokuwa. Lakini mara chache kwa wavulana kuchenji lafudhi yao ya asili.
  HIVYO NAOMBA KUJUZWA HILO LA KUBADILIKA LAFUDHI KWA NINI NI RAHISI KWA KINA DADA ?!
   
 2. m

  mhondo JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Wakına dada ndıyo wanaweza kujıbu.
   
 3. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Ahsante Mkuu kwa mawazo yako.
  Ngoja tusubiri na ya wengine.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  swagga tu hizo ili waonekane wajanja kwa wwenzao wa bush
   
 5. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Duuuh!
  Ya kweli hayo mkuu!
   
 6. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wahehe nn hao mkuu? Maana weng ndo zao.
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehehehehe. . . huu ni ugonjwa?

  Nwy ngoja nijaribu kuilezea kwa mtazamo wa kisaikolojia ili jibu liendane na jukwaa husika.

  Kwenye saikolojia kuna kitu kinaita Conformity. Hicho ni kitendo cha mtu kubadilika kifikra, kimuonekano, kitabia n.k ili aendane na mazingira yanayomkabili au wakati mwingine anafanya hivyo ili tu atimize hitaji lake la kuwa KUNDINI badala ya nje ya kundi. Yani nae afanane na wenzake, asionekane tofauti/mshamba/asiyejua kitu.

  Mf. Mzuri ni asilimia kubwa ya vijana wanapoanza kuvuta sigara/kunywa pombe. Wengi hua wanaanza kufanya hayo kwasababu marafiki zao wanafanya hayo. Kukwepa kuitwa mshamba ama kuonekana mjuaji/wa ajabu kwa kutofanya kitu ambacho ni cha kijinga ila kinachokubaliwa na kundi.

  Nikirudi kwa wadada na lafudhi vs wakaka na lafudhi.
  Kwa wadada kujionyesha nae ni wa mjini ni muhimu kuliko kwa wakaka. Hao mabinti wanapokuja mjini wanaona hitaji la wao kufanana na waliowakuta ili nao wafanane na waliowakuta pia wasiitwe/wasionekane ni washamba, kitu ambacho hakiwasumbua sana vijana wa kiume.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Wadada ni wepesi wa kulearn mambo mapya na kuyapractice.
   
 9. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ahsante sana mkuu!
  Kwa ufafanuzi wa kitaalamu zaidi! NIMEIPENDA HII!!
  But sorry sikumaanisha ugonjwa! Ila nilikuwa nahisi labda ni tatizo la kisaikolojia (kwa maelezo yako najihisi kuwa sahihi). Hivyo sikuona jukwaa lifaalo zaidi ya hili.

   
 10. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35


  Teh teh teh!
  Hapana Mkuu. Msafara wa mamba tu...
  Gogo tribe.
   
 11. DAWA YA SIKIO

  DAWA YA SIKIO JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  LOL !... Sikulijua hilo.
  Thanx Mkuu!
  Sasa naanza kupata mwanga!
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Usijali nlikua nazingua tu. .
   
Loading...