STEIN
JF-Expert Member
- Aug 29, 2010
- 1,772
- 555
WanaJF ni kweli kabisa kama kiongozi unatakiwa kufahamu mijadala mbali mbali yanayohusu nchi yako na kwa TZ JF ndiyo mtandao ambao unaruhusu watu kutoa michango yao mbali mbali yanayohusu siasa, jamii na maisha yao kwa ujumla kwa hiyo Dr. Slaa kama viongozi wengine wanapaswa kuingia jamii forum na kufahamu wanaJF na waTZ tunajadili mada zipi.
Ila ninachokipenda kwa DR. Slaa yuko mwazi, amekuwa anatumia jina lake halisi na hii ni kutokana na ujasiri wake kwa sababu si mtu wa majungu, kama kuna issue tata anatoa ufafanuzi na watu tunamwelewa na kusonga mbele yote ikiwa ni kujenga taifa letu.
Katika hili ndio sababu waTZ wengi tunampenda ukiacha yale matawi ya mafisadi, kwani Dr. Slaa atakwambia ukweli hata kama hupendi.
Kingine ambacho naweza kusema kwa Dr. Slaa ni mtu wa kupenda kusoma kila kitu na kuielewa mimi nafikiri katika hili hata nikimfagilia hakuna wa kupinga kwani amekuwa akikosoa doc. mbali mbali za serikali hata sheria kama utakumbuka amekuwa akitoa kasoro mbali mbali kwenye bajeti, vifungu vya sheria vilivyopelekwa bungeni kwa miaka kumi na tano ya kuwa bungeni haya tumekuwa tukiyaona.
Mwisho mimi ningewashauri wamiliki wa JF wangetupa taarifa ya lini na kwa muda gani Dr. Slaa atatoa ufafanuzi wa maswala yanayohusu taifa letu in advace ili watu tuwe standby kumsubiri.
Mwisho nampongeza Dr, Slaa kwa kuwa muwazi na kwa kutupa sisi waTZ moyo na aendelee na moyo huo sisi tupo pamoja naye.
Najua Viongozi wengi lazima wapo humu JF lakini hawataki wajulikane wamo humu sijui kwa sababu gani au kwa kutojiamini kwa mambo wanyofanya.
Thanks Peoples power Katiba mpya lazima viraka vimetosha.