Kwa nini Dk. Idris Rashidi bado yuko kazini hadi leo?

Ukishindwa Ku-deliver kujiuzulu its Fine...Kuna wabongo wetu ambao hawajapewa nafasi ili tuone Vipaji vyao...!!!

Mambo ya kufikishwa Mahakamani any person anaweza..Ikiwa Mtikila anaweza sembuse wengine washindwe....Kupelekwa mahakamani hakutegemei upo ktk Kiti au Umejiuzulu...!!!

Ingependeza sana kama mtu akishindwa kudeliver akiwa anajiuzuru. Hawa jama hatakama hawaperform hawajiuzuru mpaka raia wawavalie njuga ndio wanatoka tena kwa shida sana. Anyway tutasikia kama kweli kajiuzuru au la. Binafsi nilimshangaa Rais alipopinga kujiuzuru kwake kipindi cha mwanzo kwa kuwa sikuona anafanya nini cha kumbembeleza aendelee kuchakaza tanesco na wananchi kwa bill za ajabu ajabu zisizolingana na garama sahihi ya uzalishaji umeme.
 
Actually jamaa amedeliver kitu fulani pale Tanesco kwa kuboresha masurufu kwa wafanyakazi na hali bora kimaisha. Hii ishu ya Dowans imekuwa politicised mno na hata yeye Dr. Idriss nadhani alikuwa na jazba mno kuzungumza na vyombo vya habari hilo ni kosa lililofanyika. Angemtumia yule Badra Masoud labda ingeleta taswira tofauti kwa sababu yeye amehusishwa na kashfa ya rada. Lakini huwezi kulinganisha achievement ya Idriss na Mattaka . Kama unataka kuamini nenda Tanesco kawaulize watu wa chini watakavyokuambiwa. Hii Dowans ni kama chambo ambacho kitawaponza wengi.
 
akajiuzulu uko ndi kajimaliza,ushauri asijaribu..jk atamwasha na radar fasta akimbizane na ROYAL GREEN BUS
 
Actually jamaa amedeliver kitu fulani pale Tanesco kwa kuboresha masurufu kwa wafanyakazi na hali bora kimaisha. Hii ishu ya Dowans imekuwa politicised mno na hata yeye Dr. Idriss nadhani alikuwa na jazba mno kuzungumza na vyombo vya habari hilo ni kosa lililofanyika. Angemtumia yule Badra Masoud labda ingeleta taswira tofauti kwa sababu yeye amehusishwa na kashfa ya rada. Lakini huwezi kulinganisha achievement ya Idriss na Mattaka . Kama unataka kuamini nenda Tanesco kawaulize watu wa chini watakavyokuambiwa. Hii Dowans ni kama chambo ambacho kitawaponza wengi.

Mkuu hivi hicho ndiyo kipimo cha success? Well baada ya kufanya hayo ameongeza MW ngapi kwenye grid ya taifa toka amepewa huo u MD, amekusanya madeni mangapi na kiasi gani?, Ameboresha Tanesco infrastructure kwa kiasi gani?
 
Inawezekana kuwa amewekwa kutimiza mahitaji ya watu fulani. Ila sioni kuwa ataondolewa. Inawezekana pia kuwa aliamua mitambo ya DOWANS inunuliwe kutokana na vitisho ambavyo wanaotaka awafanyie mambo yao walimpa. Vitisho vya kufunguliwa mashitaka kwa mambo aliyowahi kufanya kinyume na mataratibu (Rada n.k).

Mawazo yako yanafanana na ya wengi humu JF,Task aliyopewa ni kununua Dowans ili senti itakayolipwa irudi kwenye chama chao CCM ili baadaye 2010 itumike kwa uchaguzi, CCM ikishindaa hiyo ndio salama yao wote mafisadi kwa miaka mingine mitano tu na baada ya hapo wataanza kutafuta fedha za uchaguzi wa 2015, kumbuka nilazima iwe vicious cycle ili wabaki salama hivyo Idrisa na madhambi yote yake mkuu kamwe hawezi kuyaona kwani kumweka mtu asiyemjua au mtu makini asiyetaka ujinga pale TANESCO itakuwa sawa na kujifungia ndani ya nyumba halafu ukawasha moto yaani kujiua kwa kukosa pesa za uchaguzi na kukosa kuchaguliwa kuongoza nchi, elewa kuwa Tanesco imekuwa uchochoro muafaka wa ku create majanga hewa ya nchi itakuwa giza, viwanda vitasimama, wagonjwa hawatatibiwa etc etc Mie bado naamini kwa kiburi chao na hasa kama hawakuwa na plan B basi watanunua mitambo ya Dowans kijeurijeuri, au wanaweza kuunda deal lingine kwa haraka haraka kama njaa hivi na vile alimradi wawe na pesa ya uchaguzi ili mafisadi wasipelekwe Ukonga baada ya CCM kushindwa au kupata kiongozi ndani ya CCM asiyependa ufisadi ambaye anaweza kuwapeleka jela kama kule Zambia, Malawi etc na hii ndio siri ya makundi ndani ya chama chao kwamwe hayataisha kwani hawaaminiani lakini wamekubaliana kuaaminiana
 
Mkuu hivi hicho ndiyo kipimo cha success? Well baada ya kufanya hayo ameongeza MW ngapi kwenye grid ya taifa toka amepewa huo u MD, amekusanya madeni mangapi na kiasi gani?, Ameboresha Tanesco infrastructure kwa kiasi gani?

Kwa kuongezea kwenye maswali yako mazuri Mkuu Nyambala, ni vyema kujiuliza pia;

1. Amezuia kiasi gani cha hasara kinachoikumba TANESCO hado sasa (kuibiwa kwa mafuta ya transformers, by-pass ya meter za Tanesco, fraud ya wafanyakazi wa billing, na vishoka n.k.)?
2. Ameboresha kwa kiasi gani mapato ya shirika?
3. Ameongeza kwa kiasi usambazaji wa huduma za umeme kwa watumiaji?
4. Ameongeza imani ya waTanzania kuhusiana na Tanesco kwa kiasi gani (kabla na baada ya DOWANS)?
5. Ana mipango gani ya muda mfupi/kati/mrefu wa kuinua ufanisi wa shirika, mapato yake na ukuaji wa infrastructure? Ana malengo gani positive?

Kama tukiweza kupatiwa majibu ya maswali hayo, itakuwa rahisi kusema ameleta maendeleo kwa TANESCO. Vinginevyo, inawezekana hakuna alilofanya la maana.
 
Actually jamaa amedeliver kitu fulani pale Tanesco kwa kuboresha masurufu kwa wafanyakazi na hali bora kimaisha. Hii ishu ya Dowans imekuwa politicised mno na hata yeye Dr. Idriss nadhani alikuwa na jazba mno kuzungumza na vyombo vya habari hilo ni kosa lililofanyika. Angemtumia yule Badra Masoud labda ingeleta taswira tofauti kwa sababu yeye amehusishwa na kashfa ya rada. Lakini huwezi kulinganisha achievement ya Idriss na Mattaka . Kama unataka kuamini nenda Tanesco kawaulize watu wa chini watakavyokuambiwa. Hii Dowans ni kama chambo ambacho kitawaponza wengi.

Mkuu lakini si unajua hatukumpeleka pale kuangalia maslahi ya wafanyakazi pekee lakini ni pamoja na maslahi ya watanzania wote?
Sasa kama kaweza kufanya vema upande wa wafanyakazi ni vema lakini kama ame mess upande mwingine no excuse. Hatuwezi kukubali huu kama utetezi wake maana si nyingi hili lingekuwa kama kiini macho maana hakuna namna ingebidi wapunguze wafanyakazi ili kuli manage shirika vizuri.
Je hapa inasaidia nini? Aondoke waje wa tz wengine wenye uaminifu na kazi wajenge nchi.
 
Mkuu hivi hicho ndiyo kipimo cha success? Well baada ya kufanya hayo ameongeza MW ngapi kwenye grid ya taifa toka amepewa huo u MD, amekusanya madeni mangapi na kiasi gani?, Ameboresha Tanesco infrastructure kwa kiasi gani?

Mmejificha wapi, na umeneja wa TANESCO mnaovyouweza?
 
Tetesi ni sehemu ya maisha ya binadamu,so sioni cha ajabu kwani hata mwenyewe jumapili nilisikia kwamba liyumba nae kafa but mpaka leo kimya.so ni tetesi tu
 
ajiuzulu tuuu kwani yeye nani???aendee zake...maana kwanza amewekwa kisiasa zaidi....kwenye usaili hata jina lake halikuwemo kabisaa....walikuwemo ma engineer 3.....yeye ametokea wapi?apumzike kwanza arudishe pesa zetu za rada....eboo hakuna cha uswahiba wala nini hapa...JK apate somo toka kwa mwenzake wa magadasca....power of people...
 
Hajajiuzulu yuko kazini anachapa kazi. Lakini nadhani aliyesema amejiuzulu ametumwa naye ili wapate kutuchezea mchezo wa kuigiza na apate kubembelezwa kama alivyobembelezwa wakati wa sakata la Kiwanda cha Saruji Tanga na hivi karibuni kabla ya kujitoa kununua Dowans. Nadhani kama JK aliweza kukataa barua ya kujiuzulu kwa marehemu Ballali aliyekua mgonjwa Marekani na akamtimua mtu anayeumwa mpaka akafa, sioni sababu ya kumtimua Dk. Rashidi hata kama ameandika barua ya kujiuzulu. Haki yake ni kutimuliwa. Kama alivyosema MPENDAZOE (Raia Mwema la leo) kwamba kama unataka usifuatwe na nzi (si yule wa Mwanakijiji) basi tupa kibudu kilichooza. JK aachane na VIBUDU ili inzi wasimfuate. Asipoangalia muda si mrefu na yeye ataanza KUNUKA (Kama hajaanza)
 
Ukisoma yale mahojiano yake na kamati ya Zitto utaona kuwa huyu bwana anatakiwa aondoke Tanesco ASAP kwasababu hana uchungu kabisa na hilo shirika.

Inaelekea tayari anao utajiri wa kutosha na pale anafanya tu kazi ili kulindwa na wakuu wenzake serikalini.

Inakuwaje ajue kuwa Richmond ndio Dowans halafu badala ya kulala nao sambamba ili wawalipe Tanesco anajaribu kutumia mlango wa nyuma wa kamati ya Zitto kuinufaisha Dowans zaidi?
 
Badra Msoud si alaajriwa kwa upendeleo wa wazi kumtetea huyo mkuu wake. Asome hapa JF atuambie kabla hajaondoka tanesco zile fedha alizokopa Billioni 300 shilingi za Tanzania mwaka 2007 KUTOKA mabenki saba ya hapa Tanzania ambayo walimpatia asilimia 5% kama rushwa zimetumika vipi? Je endapo mkataba wake Dr. Idris wa miaka 3 utakapokwisha Novemba 2009 na hakika hataongezewa ameweka mkakati gani wa kulipa hio pesa za Mabenki pamoja na riba yake ya Asilimia 15%. Kama haitawekwa wazi kwa nini tusiseme JK alimpeleka pale kama chuma ulete wakagawane huko uarabuni? Siku hizi Waswis wamekataa kupokea pesa chafu. Watanzania vinginevyo Deni la taifa litakuwa kwa sababu kusema ukweli tanesco ilivyo taabani hata wakiuza wafanyakazi wao hizi pesa hazilipiki he!he!...heeeee! Nimeambiwa serikali imetoa mdhamana kama ule wa Dowans kama sio kukuza deni la taifa na kuongeza umaskini ni nini!!!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom