Kwa nini Dk. Idris Rashidi bado yuko kazini hadi leo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Dk. Idris Rashidi bado yuko kazini hadi leo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Feb 28, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idrisa Rashidi ni miongoni mwa watu kumi mashuhuri walioshiriki na kujipatia mabilioni katika kashfa ya radar. Wahusika wengine wakuu ni pamoja na Andrew Chenge, Sailesh Pragji Vithlani na Tanil Kumar Chandulal Somaiya.

  Iliwahi kutajwa kuwa mnamo May 1998, Chenge alimgawia nusu ya pesa za rushwa alizopata (kiasi cha Tsh. 750,000,000.00) Dr. Idris kupitia kampuni yake ya Langley Investments Ltd.

  Chenge akiwa Mwanasheria Mkuu wa serikali na Dr. Idris akiwa Gavana wa Benki Kuu walilipwa fedha hizo kwa ushiriki wao katika kufikiwa kwa mkataba wa ununuzi wa rada hiyo iliyouzwa kwa serikali na shirika la kuuza vifaa vya kijeshi la Uingereza, BAE System.

  Kufuatia kashfa hii, Chenge alilazimika kujiuzulu lakini Dr. Idris bado kajaa tele pale Tanesco akiwa Mtendaji Mkuu na hivi sasa anapendekeza serikali inunue mitambo ya Dowans.

  Kwa nini Dr. Idris Rashidi bado yuko pale hadi leo hii !! Ni siri gani anayo huyu fisadi ?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Mag3, labda fisadi huyu naye akifukuzwa kazi nchi itawaka moto. Maana ni mtu mzito siyo kama Mnali ambaye rungu la Rais lilimshukia haraka sana tena bila kuchelewa.
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mnashangaa ya Rashid kwanini msishangae ya Chenge, pamoja na ushahidi wote kupatikana bado anapewa majukumu nyeti serikalini.
   
 4. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hakuna ushahidi wa kumtia hatiani. Hii ni nchi ya demokrasia na utawala bora mzee.
   
 5. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha safi sana, hoja kama hizi zinafaa kupunguza hasira maana inabidi uchekeure we need revolution otherwise we still have long way to go
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Katika principles za utawala bora unamwaminije mtu mwenye questionable credibility????????? Tunarudi pale pale maadili si sheria! Maana yangu ni kwamba hata kama kisheria inawezekana hatia haionekani lakini je kimaadili inakuwaje watu kama Chenge na Dr Idris tuendelee kuwatumia kwenye mambo nyeti?????
   
 7. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #7
  Mar 1, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  MAG3,
  Tuendelee kushinikiza, Listi bado ndefu. Tutafika, tusikate tamaa. Kama JK hachukui hatua, nguvu ya umma itafanya kazi yake. Sasa tunazo taarifa kamili ya mgawo huo, si unajua JK hachukui hatua mpaka asukumwe. Tufanye kila jitihada, nazo fedha hizo zirudi, labda tutagawana tena kama tulivyofanya za EPA
   
 8. A

  Alpha JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Chenge is an elected official and hence not quite as easy to get rid of.

  Rashid is appointed and can be easily fired at any time with very little notice.
   
 9. B

  Baba Ubaya Senior Member

  #9
  Mar 1, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu hawa jamaa nchi wameifanya kama yao kiama chao ni 2010
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,295
  Trophy Points: 280
  Wajameni, bado hakuna ushahidi wa kumtia yoyote hatiani. Chenge alishatoa ushahidi vile vijisenti vyake ni urithi wa familia, si mnajua Wasukuma ni matajiri wa ng'ombe na almasi wanachezea bao. Tena Chenge ni mweupe mathalani ana madada 10 weupee na kila mmoja kaolewa na mahari ya milioni mia mia. Tule tujisenti ni twa kwake, kosa liko wapi?.

  Kuhusu Dr. Rashid, hakugaiwa mgawo, bali alikopeshwa hizo laki
  600,000 akaanzishe mradi wa kuku wa kienyeji, kosa liko wapi mbona hamuelewi?!.

  Mwacheni Chenge akajilie tujisenti twake kwa amani, mwakani atatupunguza kidogo kwa kununulia tujikanga, tufulana na kupika
  Pilau siku ya Jumamosi ya tarehe 30, October, 2010 ili tuendelee kukutana pale counter ya Dodoma Hotel kwa miaka mitano mingine.

  Hata Dr. Rashid mwacheni mpaka atosheke, malipo ya pensheni yake pia ataendelea kuuboresha ule mradi wa kuku, kwani tayari
  Deni la Chenge alishasamehewa tangu siku ya mkopo ndio maana hakuna mkataba wa kukopeshana.
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Dr. Idris Rashidi aliteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu baada ya kifo cha Gilman Rutihinda mwaka 1993. Aliweza kudumu hapo kwa kipindi cha miaka sita toka 1994-1999, kipindi kilichogubikwa na wingu zito la ufisadi lililohusisha hii Benki ya Wananchi. Katika kipindi hicho tulishuhudia serikali ikiingia mikataba mbalimbali iliyoifunga serikali na kuisababishia madeni makubwa.

  Baada ya hapo na katika kipindi cha miaka sita alifanya kazi katika taasisi tatu tofauti ambako inasemekana alijiuzulu kwa sababu zisizojulikana mpaka alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco. Mwaka 2007 alitingisha kiberiti kwa kutishia kujiuzulu lakini JK, kwa sababu zisizojulikana, akaamua kumtetea na kukataa kumkubalia .

  Je, ni uswahiba peke yake ama kuna zaidi ?
   
 12. 911

  911 Platinum Member

  #12
  Mar 2, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Hawezi ondoka kwa sababu alipotaka kuondoka mara ya kwanza kiranja mkuu alimzuia/alimrudisha.
   
 13. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Baba Ubaya ukiweza kunihakikishia hilo, wallah nitakuwa mwenye furaha sana. Ukweli sioni jinsi ambayo CCM itasulubiwa 2010 na kusababisha kiama chao. Sioni mikakati yoyote ya kuweza kuizuia CCM isishinde 2010.

  Ninachokiona tu ni kwamba, wanaCCM wazuri watakaa pembeni kuangalia mchezo wa wanaMtandao katika siasa. Mkuu, nchi hii itachekesha zaidi baada ya 2010, trust me.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Editorial: Tanesco management needs overhauling

  EDITOR
  THIS DAY
  DAR ES SALAAM

  ONCE again Tanzania Electric Supply Company management has reignited debate on the proposal to buy part of the second hand Dowans Holdings turbines. The giant state utility energy company is going through lean times with a lethargic financial position, aged and poorly maintained generation infrastructure and an incompetent management.

  When former central bank governor, Dr Idrisa Rashidi was appointed to head the state company last year, there was a ray of hope that the management had found a highly experienced man who would be able to turn its fortunes around.

  Then President Jakaya Kikwete appointed another highly qualified Tanzanian to head the company's board of directors. With the naming of Peter Ngumbulu, a former Treasury permanent secretary and International Monetary Fund director, things looked promising.

  Then Rashidi issued a lengthy press statement in the local media last week arguing in favour of buying Dowans turbines because of the growing electricity needs. His arguments which have managed to garner some support from credible politicians, are yet another attempt by crooked owners of the turbines to sell their plant at inflated prices.

  Nothing new has emerged in Dr Rashidi's arguments so far, except for continued rhetoric that seeks to convince taxpayers that using their money to buy used turbines is a wise idea. This latest attempt by the TANESCO management is nothing more than the continuation of crooked attempts by some people in our society who have turned our public offices into places where resources are siphoned by politicians and businesspersons.

  It is in the public interest to ensure that this latest attempt fails. Meanwhile, the appointing authorities should give Mr Ngumbulu's new board people with impeccable records to replace the current team some of whose personalities are subject to corruption related investigations.

  If there is need to buy turbines as the TANESCO management wants us to believe, then such a decision has to be made by a different management team headed by someone who is not implicated in another national scandal.

  Such a decision must also not consider in any way the purchase of Dowans turbines as they are second hand and therefore violate the 2004 Public Procurement Act. While the government and the appointing authority need to urgently consider the question of overhauling the giant utility company's senior management team to give it a new lease of life, it is important that the latest attempt be nipped in the bud.

  We urgently need serious people to manage TANESCO as the country heads towards a deregulated energy sector. Such individuals will need to be untainted visionaries, free of the baggage of corruption allegations and the proclivities of a past dotted with questionable purchases.

  This country has serious energy challenges to address and TANESCO has a central role to play in it other than than engaging in side games.

  We hope wisdom, integrity and patriotism, instead of selfishness, greed and bigotry will prevail when TANESCO's board and the parent ministry heed advice from parliamentary energy and minerals committee.
   
 15. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa siku zake zinahesabika. Just wait and see.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,956
  Trophy Points: 280
  Alitakiwa kufukuzwa kazi siku nyingi sana tangu pale ilipobainika kwamba Mzee wa Vijisenti alimuwekea Vijisenti vyenye thamani ya $600,000 kwenye bank account yake ya nje, lakini Mkuu wake wa kazi au Rais wa nchi hakuona kama hilo linastahili kumfukuzisha kazi. Si ajabu akamuomba ajiuzulu.
   
 17. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini mmsukume JK achukue hatua wakati yeye mwenyewe ni mhusika? Kwa hiyo yeye mmemtoa katika watuhumiwa wenu?
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nguvu za Dowans ni kali, zapofua uongozi Tanesco

  2009-03-03 11:01:11
  Na Muhibu Said


  Nguvu za kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, zimeifumba macho menejimenti ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kiasi cha uongozi huo kuipuuza Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo la umma, Nipashe imeelezwa.

  Habari za kiuchunguzi na vyanzo vya habari ndani ya Tanesco vimeithibitishia Nipashe kwamba Menejimenti ya shirika hilo pekee na kongwe la kuzalisha nishati ya umeme nchini, ilitangaza mapendekezo yake ya kutaka kununua mitambo ya kufua umeme wa dharura ya Dowans huku ikijua fika Bodi ilikuwa imetoa maelekezo kadhaa ya kuzingatiwa kabla ya tangazo hilo.

  Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya Tanesco kinaeleza kuwa miezi minne iliyopita bodi ilitoa maagizo matatu muhimu kwa menejimenti ya Tanesco, lakini hadi mwezi uliopita uongozi huo uliposema bado unafukuzia mitambo ya Dowans, ulikuwa haujatekeleza hata agizo moja.

  Hatua hiyo ya menejimenti ya Tanesco ambayo imeibua mjadala mkali miongoni mwa Watanzania na kuwagawa wabunge makundi mawili kupitia Kamati za Bunge, inaelezwa kuwa imeishtua Bodi hiyo.

  Kikao cha Bodi kilichofanyika Desemba 12, mwaka jana, kilihitimishwa kwa kwa kuiagiza menejimenti ya Tanesco kuteua wajumbe wawili kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ajili ya safari ya kwenda Houston, nchini Marekani kuangalia bei ya mitambo kama ile inayomilikiwa na Dowans.

  Ilielezwa kuwa agizo hilo lilitolewa kutokana na taarifa ambazo Bodi inazo, kwamba mitambo kama ile inayomilikiwa na Dowans, inauzwa kwa Dola za Marekani milioni 14 wakati mitambo ya kampuni hiyo, ambayo ni michakavu Tanesco wanataka kuinunua kwa Dola milioni 30, yaani zaidi ya mara mbili ya bei halisi.

  ``Hata hivyo, menejimenti ya Tanesco haikutekeleza agizo hilo,`` kilieleza chanzo chetu ndani ya Tanesco.


  Mbali na agizo hilo, Bodi pia iliitaka menejimenti ya Tanesco kukumbuka ushauri uliotolewa kwake na wanasheria wa shirika hilo kwamba kampuni ya Richmond ni hewa na mkataba na mitambo ya Dowans imetokana na kampuni hiyo, hivyo chochote kinachotokana na Dowans pia kitakuwa na utata.

  Chanzo hicho kimesema kwamba Bodi waliiagiza menejimenti ya Tanesco iwasiliane na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupata uhalali wa mitambo ya Dowans, ambayo imeirithi kutoka Richmond, pia waombe marekebisho ya sheria ya manunuzi.

  ``Lakini menejimenti ya Tanesco hawakufanya hivyo, badala yake wakaamua kutoa tangazo kwenye vyombo vya habari kutaka Bodi iidhinishe ununuzi wa hiyo mitambo ya Dowans. Bodi imeshtuka sana,`` kilieleza chanzo hicho.


  Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Adola Mapunda, alipoulizwa na Nipashe jana, alisema hawezi kuzungumza lolote kwa vile suala hilo liko mahakamani.

  Kutokana na kauli ya Mapunda, hata uongozi wa Tanesco haukupaswa kuzungumzia wala kutangaza mipango ya kununua Dowans hadi kesi dhidi ya shirika hilo imalizike.

  Wakati hayo yakijiri, habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana zinaeleza kuwa Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa leo kukutana na viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, ikiwamo menejimenti ya Tanesco na huenda hoja kuhusu Dowans ikawemo katika orodha ya mambo yatakayojadiliwa katika kikao hicho.

  Jumamosi wiki iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk. Idris Rashid, alitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kueleza hali ya umeme katika Gridi ya Taifa pamoja na mambo mengine, akapendekeza kuwa mtambo wote wa Dowans ununuliwe na serikali pamoja na vifaa vyote vya kuunganishia kwenye gridi.

  Hata hivyo, wakati Tanesco ikitoa taarifa hiyo, Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, alikaririwa na Nipashe akisema kuwa ni vigumu kununua mitambo ya Dowans kwa sababu licha ya kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na maazimio ya Bunge, kampuni hiyo imefungua kesi dhidi ya serikali na Tanesco katika mahakama ya usuluhishi huko Paris, Ufaransa.

  Kutokana na hali hiyo, Dk. Mwakyembe alisema anashangazwa na hatua ya Tanesco kung`ang`ania mitambo ya Dowans, wakati tayari wamiliki wake wamewashtaki serikali na Tanesco huko Ufaransa.

  Wakati Dk. Mwakyembe na kamati yake wakipinga vikali suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wiki iliyopita alikaririwa na vyombo vya habari akibadilisha msimamo wa awali wa serikali wa kutonunua mitambo ya Dowans kwa kusema kwamba, uamuzi huo si ufisadi.

  SOURCE: Nipashe
   
 19. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimemsikiliza kwa makini Mh. W. Ngeleja katika mahojiano yake na M.M.

  Nilichokielewa kuhusiana na issue nzima ya ununuzi wa mitambo ya Dowans ni kama ifuatavyo;

  1. Si lazima kununua mitambo ya Dowans (sasa wala baadae)
  2. Kwa kuwa Dowans inakusudia kuuza mitambo yao, serikali inaona ni vyema kujaribu kuangalia uwezekano wa kuwa mmoja wa watakaoinunua (labda kwa kuzingatia unafuu wa bei). Na kuwa Dowans inayoruhusa ya kuiuza mitambo kwa yeyote endapo tu, itahakikisha inalipa pesa za serikali (approx. $8m)
  3. Serikali bado haijaamua kununua mitambo hiyo. Bali haioni kuwa ni kosa kufanya hivyo
  4. Hata serikali isiponunua mitambo hiyo, itawajibika kununua mingine (kwa bei ya juu zaidi) katika kipindi kifupi kijacho kutikana na mahitaji ya uwekezaji (Mara/Mwanza)
  5. Kwamba kizuizi serikali ilichokiweka kwa Dowans kuchukua mitambo yake, kinatokana na deni la approx. $8m ambazo serikali inadai
  6. elimu/ taarifa zaidi zinatakiwa kutolewa ili wananchi waelewe kusudio la serikali
  7. Serikali inahisi kuwa endapo Dowans wakifanikiwa kuiuza mitambo yao kwa wengine, nchi itajikuta ikipungukiwa na nishati ya umeme, au kupoteza nafasi muhimu ya kutumia mitambo iliyokwisha fungwa na ikiwa tayari kutumiwa.

  Hayo hapo juu pamoja ne mengine machache yanaweza kuwa ndio maana halisi ya sakata hili.

  Mimi kwa mtazamo wangu, serikali ihakikishe hata kama itapata deal zuri kutika Dowans kuliko inavyoweza kupata sehemu nyingine duniani, ni vyema ikafuata sheria zote za manunuzi, ili ieleweke kwa wananchi na ikidhi matakwa ya sheria zetu na kuepusha usumbufu wa kashfa za viongozi. Naamini pia, kuwa serikali itakuwa makini kufanya tathmini ya bei halali za mitambo ili iweze ku-negotiate vizuri na pia iweze kuamua vyema. Serikali iweke manunuzi yote wazi, na ikiwezekana ipate baraka za Bunge ili isije ikakaangwa tena hapo Bungeni.

  Naamini kuwa kama serikali ina nia njema katika maamuzi haya, itafanya maamuzi yote hadi mwisho kwa umakini na uadilifu unaostahili.
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mimi nilichokielewa kuhusiana na issue nzima ya ununuzi wa mitambo ya Dowans ni kimoja tu nacho ni kuwa hatuna serikali makini. Serikali iliingia mkataba na watu isiowafahamu, Serikali inafanya biashara na kampuni isioifahamu na sasa serikali inataka kununua mitambo chakavu kwa kampuni ya hao hao wasiofahamika.

  Ninavyofahamu Serikali inayoweza kufanya mambo kama hayo haiwezi kudai ni Serikali halali. Na hapa ndipo yale madai kuwa hii Serikali iliingia madarakani kwa njia isiyo halali inathibitishwa. Kuliwahi kutolewa tetesi kuwa JK aliwahi kumtembelea Mohamed Gire, Houston, Texas kabla ya dili la Richmond lakini tetesi hii ilipuuzwa.

  Richmond na Dowans tuyaogope kama ukoma na bado. Dr. Idris Rashidi wa Tanesco is in it up to his eyebrows and only time will tell, Houston-Dubai Connection ?? yangu macho.
   
Loading...