Sr.M'HINDAKILI.GES
Member
- Jul 20, 2013
- 8
- 0
Tulianza na MUNGU tutamaliza na MUNGU tuombe sana jinamizi ccm tulitoe kabisa kwa pamoja tunaweza NGUVU y UMMA NI NGUVU YA MUNGU.
Mkuu Mchambuzi, kwanza nimegundua
kwamba katika tunachojadili hapa kwa kiasi kikubwa tuko kwenye page
moja. Ila pia nieleze masikitiko yangu kwamba katika post yako
nimegundua kuwa ile chapter ya kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
2005-2010 inayosema „Hali Ilivyo Duniani na Majukumu Yaliyo Mbele
Yetu" hujaipitia. Nasema hivi kwa sababu sehemu kubwa ya hoja
ulizoraise hapa zina majibu ya moja kwa moja toka kwenye chapter
hiyo.
Nimesikitika kuona kwa mfano Mbowe na wenzake wameona solution ya watoto wa form
four kufeli ni kuitisha maandamano ya kuilaani serikali. Nilimtumia
Dr. Slaa video ya Obama alivyojibu swali la kuporomoka kwa elimu
Marekani wakati yuko kwenye kampeni za Urais mwaka 2008 akiwa
mpinzani. Dr. Slaa Hakujibu kitu, lakini naamini kuna kitu
alijifunza iwapo aliangalia ile video.
Wazee wa Tanzania wa sasa wenye rika la miaka 65-80 waliofanikiwa, wengi
wao ni kupitia elimu (kwa maana ya ajira, hasahasa ajira
serikalini). Tukumbushane tu kuwa wapo watu walikuwa wanakataa
elimu, serikali ilikuwa inatumia adhabu ili watu wawapeleke watoto
shule. Kadri tunavyoshuka rika la chini kuna makundi ya
waliofanikiwa kwa elimu na ujasiriamali na hivi sasa wanaofanikiwa
kwa ujasiriamali wanakuwa wengi zaidi kuliko wanaotegemea elimu
(ajira). Mtu aliyekataa elimu akikosa personal progress hana wa
kumlaumu.
Ukiangalia watu uliosoma nao at a centain level sekondari au shule ya msingi,
utaona wapo ambao „hawajamake it". Kwenye post yako ya juu
ulisema kuwa wewe umefanikiwa na unachofanya ni kujaribu kusaidia
wengine. May be I should ask you, je ni nini kimekuwezesha wewe
kufanikiwa zaidi ya baadhi ya wenzako uliosoma au kukua nao? Jibu
linaweza kuwa na maelezo mengi, lakini lazima part of it iwe kuwa
ulifanya bidii.Na hapo ndipo tunapata jibu la swali lako la msingi
(in green), kuwa hard work ni msingi wa mafanikio nchini Tanzania.
Tukumbuke kwamba maendeleo ya sayansi hutokea kwa speed isiyotabirika. Jambo
ambalo tunatabiri litatokea miaka 20 ijayo anaweza kutokea mtu
akalifanya hata kesho kama jinsi historia ya binadamu kwenda mwezini
ilivyotokea bila kutarajiwa! Kwahiyo tusidhani tuna muda mwingi wa
kufikiria jinsi ya kudeal na hizi changamoto za teknolojia.
Haya yote ni maswali ambayo watu wa ulimwengu huu inabidi wayajibu. Haya
maswali tusiwaachie wamarekani na wajerumani peke yao. Wakati kijana
wa Marekani anajiuliza maswali haya, kijana wa Lushoto amekaa
kibarazani analalamika maisha magumu wakati amezungukwa na ardhi
yenye rutuba ilijaa mimea ya asili na míti ya matunda ambayo chini
yake kuna matunda yayiyooza yametapakaa!
Zemarcopolo, yani unataka kuni convince kweli kabisa in your sober mind kwamba majibu kwa maswali yangu mawili hapo juu kwenye bandiko langu namba 76, majibu haya yanapatikana kwenye Chapter ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2015??? I am sorry, kwa hili, watadanganyika tu wajinga wa huko mitaani na najua wapo wengi kwani mfumo uliopo umenyima uwezo wa kuchanganua mambo; Vinginevyo kwa sisi waelewa (pengine tupo wachache) hatukubaliani na hilo, na kwa CCM ya sasa, mtu anayekosoa chama sio tena ni shujaa wa kufanikisha ukombozi per kanuni ya chama kwa mujibu wa Mwongozo wa CCM (1982) isemayo kwamba "Kukosoa na Kukosoana Ni Silaha Ya Mapinduzi", katika nyakati hizi, mwana ccm anayepingana na siasa uchwara za CCM ni adui, hivyo mtampiga kila aina ya vijembe ili mradi kuaminisha watu kwamba watu kama sisi hatuitakii mema CCM, hatutambui mchango wa chama kwa taifa letu (tumajadili mabaya tu); Kwa kweli kama umefikia hatua ya kutoa majibu kwa maswali yangu muhimu hapo juu kwa kutumia Ilani ya uchaguzi 2015, katika hili sina hoja zaidi, kwani moja ya mapungufu ya ilani husika ambayo mimi kama mwana ccm najutia ni kwa sisi CCM kusahau kujali kwamba mapinduzi ya kweli ya wananchi wa Tanzania, hasa vijana na vizazi vya baadae ni Kuanzisha mchakato wa Katiba mpya ili vijana wa leo na watoto na wajukuu zetu waje pata Social, Economic and Political Justice ambazo taifa imezikosa kwa miaka 50; CCM tulishtuka baadae wenzetu Chadema walipo shinikiza juu ya suala la Katiba Mpya na umma kuunga mkono nguvu ya hoja; Hii ni aibu kwetu na haionyeshi seriousness yetu CCM katika kutatua matatizo ya wananchi and hence disqualifies most of your arguments kwenye bandiko lako la mwisho hapo juu;
Pia ni aibu kwetu CCM kuendelea kujichanganya na suala la Ajira Ya Vijana as a Timing Bomb as if tatizo hili is Alien or Hell-Sent; To us CCM, Politicis is supreme to everything, even to common sense and rationality, na hili limejitokeza kwa kiasi kikubwa sana katika majibu yako hapo juu kuhusiana na maswali yangu ya msingi kwenye bandiko namba 76;
Pia kama sikosei,kuna sehemu nimeona ukijadili wasiwasi wako juu ya jinsi gani sina ufahamu na kanuni fulani ya UVCCM au Dira yake kuhusiana na kuboresha maisha ya watanzania (hasa vijana); Sina uhakika kama unajua TANU YOUTH LEAGUE iliundwa kwa madhumuni yepi; Kama unaelewa, tafadhali rejea na majibu yako yaliyojitosheleza; Vinginevyo TYL haikuundwa kufanikisha uliyoyajadili; Licha ya hayo, nadhani kuna jambo kubwa zaidi la kuogopesha kutokana na hoja zako, nalo ni presentation as if mkombozi wa vijana Tanzania ni UVCCM; Really? On whose terms? Ndio maana kila nikikosoa Chama chetu cha CCM unakimbilia kujadii kwamba mimi ni mtu wa Bavicha? Inashangaza kwamba hata wewe hauna ufahamu kwamba majibu ya matatizo ya CCM tanzania hayapo UVCCM wala Bavicha; Sana sana tutaweza tatua matatizo ya vijana (sio yote lakini mengi) iwapo CCM tutakubali kuruhusu kuundwa kwa chombo huru cha vijana Tanzania - Baraza La Vijana Tanzania, ambalo halitakuwa na political or ideological orientation ya aina yoyote, na badala yake kusimamia maslahi ya vijana kwa kuangalia kwanza utanzania wao; Nadhani unaelewa fika kwamba ni sisi CCM ndio tumekuwa kikwazo cha kufanikisha uundwaji wa baraza hili, licha ya juhudi za wadau mbalimbali nchini;
[/COLOR]
Hivi hauwezi kujenga hoja kupingana na sera za Chadema bila ya kutaja majina ya mbowe, slaa n.k? Mbona mimi nikijadili mapungufu ya CCM sitaji majina ya viongozi wake lakini hoja inaeleweka? Kwani Chama ni Viongozi? CCM mara nyingine tunakuwa kama majuha, tunapoteza muda mwingi sana kujadili sijui dr slaa, sijui mbowe, sijui Tundu Lissu, Sijui Mnyika, as if hawa wakimalizika kisiasa au vyovyote vile, basi umma wa watanzania utamaliza kiu yao ya kujitafutia "maisha bora", kauli mbiu ambayo tumeiunda wenyewe kwa malengo ya kisiasa na sasa imekuwa counter-productive kwani hatuna POLITICAL WILL towards that end;
Suala la wewe kutuma video kwa dr slaa etc sio hoja, hoja ya msingi hapa ni je, kwanini kiwango cha elimu Tanzania kimeshuka na kufikia hatua ya kutia aibu kiasi hiki? Je, Chadema wana mpango gani mbadala wa kutatua tatizo hili, je mpango huo unaweza fanya kazi? Kama jibu ni ndio, katika siasa za demokrasia ya uliberali, kuwa na consensus katika masuala muhimu kwa taifa ni jambo la kawaida, sio kila kitu cha upinzani hata kama ni kizuri, basi tukikatae kwa sababu kinawapa wapinzani more political mileage; Ningependa tujadili chanzo cha kushuka kwa elimu Tanzania chini ya CCM bila ya kutaja majina ya Mbowe, Dr Slaa, kwani mimi sitakuwa na haja ya kutaja majina ya viongozi wa CCM bali mapungufu ya CCM kisera;
[/COLOR]
Hoja hii inaonyesha jinsi gani TANU/CCM ilianza vizuri na baadae kupoteza dira; Hakuna ambae ana hoji mafanikio ya Tanzania kielimu kwa watanzania waliozaliwa miaka michacha baada ya uhuru; Tunaongelea matatizo ya sasa kitaifa ambayo hata sisi ni mabingwa wa kuyajadili kama "timing bomb" i.e. ukosefu wa ajira kwa vijana; Swali hapa ni je, tumefikaje hapa?
Mimi umri umeenda kidogo, na wengi wetu tuliosoma miaka ile, bidii ndio ilitufanya tufanikishe malengo yetu; Tanzania ya leo, bidii haikutoi tena kwani tukiangalia tu mfumo wa elimu uliopo, mfumo ni wa kitabaka; Zamani haikuwa jambo la ajabu kukaa dawati moja na mtoto wa Rais, waziri mkuu, shule ya msingi ya sekondari; Haikuwa ajabu kuona mke wa waziri mkuu au waziri au mwanasheria mkuu ni mwalimu wa shule ya msingi; Yote haya yalikuwa yana inspire watoto in a variety of ways; leo hii ni kama vile there is an official policy kwamba wenye uwezo wa fedha wasome shule hizi, na wale wasio na uwezo basi waende shule zile...; Kama taifa tutafika kweli? Sidhani, sana sana tunajenga bomu kubwa kuliko lile la ukosefu wa ajira; Huko mbeleni, nchi itagawanyika katika matabaka makuu mawili makubwa, yote yakigombania the right to resources and opportunities....
[/COLOR]Seriously, do we even have a practical national science and technlogy policy? Hata ICT Policy hadi leo ni Rasimu (draft)....
Seriously? Kijana wa Lushoto akilalamika juu ya ukosefu wa fursa, hilo ni tatizo? Sisi kama serikali ya CCM, what do we do to build human capital ya nchi hii from the ground up? mind you Human Capital ni suala zima la Elimu na Afya; Je, watoto wa Lushoto, Ujiji, na Tukuyu kwa mfano wanapatiwa Elimu Bora na Afya Bora au Bora Afya na Bora Elimu? Wananchi wakianza kuhamaki, ni wajibu wetu kuwaelewa and go back to the drawing board, sio kuanza kusema eti kwanini kijana wa lushoto analalamika wakati amezungukwa na ardhi yenye rutuba na kila aina ya mazao; Huu ni mtazamo disturbing kidogo, hasa kutoka kwa watu kama wewe wenye uwezo wa kukaa na policy makers wa CCM na serikali yake;