Kwa nini CCM ikihofie CHADEMA?

Kwa nini CCM ikihofie CHADEMA?

Kama kuna fursa kama udaivyo wewe, CCM na serikali yake imeshindwa nini Kuifanya Dar iwe kama New York au L.A?CCM na serikali yake imeshindwa nini kupunguza vifo vya kinamama na watoto under 5,CCM na serkali yake imeshindwa nini kuwapatia watoto wote madawati na vitabu.Mpaka sasa 85% ya nchi haina umeme?Leo hii kila masika ikianza Dar na miji mingine TZ ni vipindupindu tu-halafu bila aibu unaifananisha Marekani na Tanzania!Fursa zilizopo Marekani hazijaja tu kwa kuota....zimetengenezwa na sera nzuri NA USIMAMIZI MADHUBUTI wa za serikali husika.Ulishasikia Wamarekani wanacheka na wansiasa/viongozi wazembe wasio na maadili na wala rushwa kama wafanyavyo ccm?Unakumbuka Bill Clinton alivyotiwa aibu ktk ishu yake ya umalaya na Monica Lewinski?Hapa bongo ni mara ngapi watu wamewapa wachumba zao ukuu wa wilaya,?Huko BOT ndo usiseme...its like a list of "Who is who" ya bongo politics!Wananchi wakianzisha vimigodi vyao ninyi mnavamia na kuwapa "wawekezaji"..alafu eti unakuja kuongea about fursa....FURSA my foot!

Tatizo lako unatumia akili za bavicha kufikiri. Hujui maana ya personal progress.

Unajua jinsi kipindupindu kinavyoambukizwa?

Wewe endelea kukaa kijiweni ukingoja chama cha siasa kije kikuletee personal progress.

Upeo wako wa bavicha ndio maana unadhani Marekani kila mtu anaishi vizuri, hujui kuwa personal progress inakuja kutokana na bidii na wala hutambui kuwa kila anayedai huduma bora anawajibika kujielezea amefanya nini katika kuipata hiyo huduma bora. Ila kwa vile wewe ni walewale bavicha type, siwezi kukushangaa...
 
Mkuu ZeMarcopolo Tanzania hakuna kitu chochote

Wafadhili wanakusaidieni kisha munawapa ardhi yenu kuna Madini wanaiba Dhahabu,Almasi, na Madini yote wanakuacheni na njaa yenu

nyie mumelala usingizi amkeni Wa-Tanzania. Viongozi wenu wanaweka mikataba ya miaka 100 kwa wafanya biashara toka nje ya nchi

kwanini iwe miaka mingi mikataba ya kuuza nchi hiyo?Wizi mtupu huo nchi ina mafuta,Gesi, na Madini lakini bado ni Masikini na omba

omba mpaka lini tutategemea misaada toka nje?wakati tuna utajiri tunaukalia wenyewe ? tujiulize kwanini tunakuwa Masikini?

Mkuu "The Chemical" unajua manufaa ya kunywa juice ya mapera?
 
Tatizo lako unatumia akili za bavicha kufikiri. Hujui maana ya personal progress.

Unajua jinsi kipindupindu kinavyoambukizwa?

Wewe endelea kukaa kijiweni ukingoja chama cha siasa kije kikuletee personal progress.

Upeo wako wa bavicha ndio maana unadhani Marekani kila mtu anaishi vizuri, hujui kuwa personal progress inakuja kutokana na bidii na wala hutambui kuwa kila anayedai huduma bora anawajibika kujielezea amefanya nini katika kuipata hiyo huduma bora. Ila kwa vile wewe ni walewale bavicha type, siwezi kukushangaa...
Kwa uzoefu wangu..ukiona mtu anaitetea saaana CCM na serikali yake ujue anatumia tumbo kufikiri....njaa tu ndo zinakusukuma kuandika utumbo humu....na labda ni uzembe wako tu kwamba hujui kuna uhusianao mkubwa tu kati ya personal progress na economic and social stability ya nchi.
 
We kalagha bhao.

Huwezi kuanza kulilia economic stability ya nchi wakati umezungukwa na opportunities kibao za personal progress ambazo umeshindwa kuzitumia! Wewe akili zako ni za bavicha ndio maana hujui kuwa your personal progress is part of national progress. Wewe ndiye mlipa kodi, ukiendelea kuwa mvivu ukingaoja chama kije kukupa ugali basi taifa litaendelea kuwa masikini, lakini ukinyanyua your behind and make use of abundancy of opportunities basi nchi itaendelea.

Anyway, kulala kwako ndio kunafanya wengine watumie vizuri opportunities zilizopo. Endelea kusubiri chama kikukomboe...
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...

Mkuu zeMarcopolo,

  1. CCM haikukubali vyama vingi kwa kupenda. Upepo ule ulokuwa ukivuma duniani kote isingeweza kuhimili kishindo chake (Urusi kusambaratika na Eastern block kuvunjika). Ulikuwa ni muziki wa mabwana wakubwa ambao kila mtu alitakiwa kuucheza. Tulikuwa tumeshafilisika kama nchi na tulihitaji misaada iliyokuja na shuruti zake.
  2. CCM kushika dola miaka 20 baada ya vyama vingi ina tafsiri nyingi. Uchanga wa upinzania ndilo jibu kubwa lakini pia CCM imekuwa inatumia nguvu nyingi ili kuudhoofisha upinzani hasa wakati ule ambao wengi wa wananchi waliokuwa na elimu ya kuongoza upinzani walikuwa wafanyakazi wa serikali. Vitisho na matendo ya uonevu waliyokuwa wanafanyiwa wafanyakazi wanaohisiwa tu, kuwa ni wapinzani viliwafanya wengi wao kukaa kimya kunusuru mkate wao lakini kwa siri wakiunga mkono upinzani. Kwa miaka 20 sasa, sekta binafsi imejijenga vizuri na wengi wetu hatutegemei tena huruma za mwajiri serikali. Ndiyo maana mpaka sasa wapinzani wengi ni wa sekta binafsi. Wafanyakazi wa serikali bado wanatishwa na kutendewa vibaya wanapojiunga na upinzani japo kikatiba ni haki yao. Hili ndilo kosa kubwa kwa CCM kwani wanafikiri wanaungwa mkono na wengi kwa kushinda chaguzi. Nafikiri bado wamelala japo kuna wachache wanajua ukweli huu na wanaogopa sana. Mtaji mwingine wa CCM ni kuungwa mkono na watu wa vijijini ambao bado wanatishwa na kukandamizwa aidha kwa ujinga wao au kwa kukosa elimu ya uraia. Sasa upinzania unapenyeza taratibu na kuelimisha huu umati ambao unatambua madhambi makubwa ya chama tawala. Hili ndilo tishio kwa CCM hapo 2015. Ndicho kisa cha CCM kuongeza nguvu za Green Guard ili kuwatishia wananchi ambao wataonekana kuunga mkono upinzani. Sambamba na hili, CCM wanatumia kila aina ya silaha waliyo nayo Polisi, Mahakama na watawala kuhakikisha kuwa haki kwa wadhulumiwa haitendeki na waathirika wanajutia kuunga mkono upinzani. Hayo yakitokea, wanahubiri majukwaani kuwa madhila wanayopata yamesababishwa na upinzani. Wanagandamiza, kwa nguvu zote sauti huru ya wanahabari (Kuwanunua, kuwatesa, kuwatishia - including vyombo vyao vya habari) wanaojaribu kuelezea ukweli wa yanayowasibu. Hii mbinu inashindwa kwa sasa kwa sababu ya utandawazi, na pia kuongezeka kwa WaTanzania wenye ufahamu kielimu. Mwaka 2015 hadithi itakuwa nyingine.
  3. CCM inaelewa kuwa upinzania unafanikiwa kuwashawishi wananchi kuukubali. Nachelea kusema kuwa CCM ilikuwa na nafasi nyingi sana za kugeuza watu waendelee kukikubali na wengi mpaka sasa wanaweza kugeuka kukifuata kama tu wangekuwa waelewa wa kinachosababisha wakataliwe (naamini wanakijua) na wananchi. Kutatua kwa dhati kero zote za wananchi ambazo hazihitaji pesa. Lakini kutekeleza hayo maana yake ni kubomoa uongozi wote wa chama na kusafisha uvundo wa siku nyingi uliokwisha poteza harufu. Hawataki kufanya hivyo kwani ni msingi wa kukiua chama chenyewe. Itabidi waamue ni upande upi wa upanga wakalie kwani kote kuna makali. Ukweli wangu ni kuwa sioni mkakati wa dhati wa CCM kurudisha imani kwa wananchi, ninachoona ni mkakati wa kuwarahisishia wapinzani kazi ya kubadilisha uongozi kupitia Mwigulu & Co who I think is probably unstable psychologically (I am sorry for this assertion na Mungu apishilie mbali).
  4. Kwa mwendo huu wa M4C, kutoa elimu ya uraia kwa umma, ukandamizaji wa wazi wa wapinzani wanajipambanua kuwa ndio watetezi wa haki za wanyonge, katiba mpya (ambayo naona CCM wanaichelewesha makusudi ili 2015 ifike uchaguzi ufanyike kwa katiba ya zamani) ambayo ingedhibiti uchakachuaji wa kura kupitia NEC, CCM ijiandae kwa lolote ikiwamo kuachia hatamu za uongozi kwa upinzani.

Babu yangu alikuwa anasema "Tusiandike kwa mate wakati wino ungalipo". Tusubiri 2015

Asante
 
Nchi yetu ina fursa nyingi sana. Kila mwenye macho anaziona na kila mwenye akili ananufaika nazo.
Wapo watu wamekaa chini ya kivuli na vibarazani wanagoja siku kije chama fulani kuboresha maisha yao. Watu hao ni kama vile wamejiingiza kwenye puto la disappointment, its just a matter of time kabla puto hilo halijapasuka.

Kwa mtanzania mwenye bidii, for personal progress, Tanzania has more opportunities than any Europen country can offer. Only USA can compete with Tanzania in terms of opportunies of personal progress.
And still we are poorest as we can be
 
We kalagha bhao.

Huwezi kuanza kulilia economic stability ya nchi wakati umezungukwa na opportunities kibao za personal progress ambazo umeshindwa kuzitumia! Wewe akili zako ni za bavicha ndio maana hujui kuwa your personal progress is part of national progress. Wewe ndiye mlipa kodi, ukiendelea kuwa mvivu ukingaoja chama kije kukupa ugali basi taifa litaendelea kuwa masikini, lakini ukinyanyua your behind and make use of abundancy of opportunities basi nchi itaendelea.

Anyway, kulala kwako ndio kunafanya wengine watumie vizuri opportunities zilizopo. Endelea kusubiri chama kikukomboe...
Daaah....unaipenda CCM mpaka nakuonea huruma😛ole sana mkuu lakini ukweli ni kwamba CCM yako imeidumaza hii nchi.Unaongea pumba za fursa hapa laki CCM hiyo hiyo ndo inayozima fursa za watanzania kibao....
1;Kushirikiana na mafisadi wa kilimo kwa kuchelewesha malipo ya pamba na korosho kila mwaka.
2;Kushindwa kudhibiti uuzaji wa pembejeo feki kama dawa na mbegu kwa wakulima(case in point madawa feki ya kuzuia wadudu kanda ya ziwa mwaka jana)
3;Kuzuia wakulima kuuza mazao yao kila wakati wa mavuno kama mmelima nyie!
4;Benki kuu kuruhusu kiasi cha riba kwa benki binafsi kufikia 22% and upward...
5;Matumizi mabaya ya kodi-30 bilioni ya vitafunio vya wakubwa unakumbuka?Hati chafu ktk halmashauri zetu je?
6;EPA,Meremeta,twin towers,Richmond.
7;Rushwa...kuanzia polisi.hosipitali,ardhi mpaka mahakamani....
Kwenye nchi yenye uzembe wa aina hii huoni kwamba hizo fursa zinaminywa daily?Unajua kiasi cha riba benki za Marekani na Uingereza?au unafananisha tu mambo kama layman!Tatizo lako kubwa ni kuangalia dunia huku ukiwa umevaa miwani yako ya kijani.
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...

Chama cha mapinduzi hakikuwa na ridha ya kukubali mfumo wa vyama vyingi na kumbuka mwl Nyerere katika kikao cha chama cha mapinduzi aliwauliza viongozi wa chama hichi kwa kuwatega kwamba wao viongozi wa chama cha mapinduzi wako tayari kukubali mfumo wa vyama vingi vya kisiasa nchini?jibu;kutoka kwa viongozi walikuwepo katika kikaa hicho mrehemu Mfaume Kawawa,Anne Abdallah na wengine wengi hapanaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!,mwl, akawaabia mnaona mlivyo waoga hamna uhakika kama tukianzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa mtashinda hatuwezi kuongozwa na chama ambacho kigonjwa hakina uhakika kama kitashida kitapoingia katika chaguzi na vyama vingine vya siasa.Uoga huu ndio unakimaliza chama cha mapinduzi.WATANZANIA HATUWEZI KUONGOZWA NA CHA KIGONJWA.
 
mkuu tukutuku hivi vyama vya kisiasa vya kibongoo vimeamuwa kuanzisha vikundi vya wanamgambo wa vyama kulikoni? Utafikiri tanzania hakuna

jeshi la polisi au jeshi la wananchi? Majangaa hayo majangaaa!!!!!!!!!!!!!!!!! Tanzania kwa miaka inayokuja mbele itakuwa kama lebanon

kutakuwa na vikundi vingi vya wanamgambo, natabiri wakristo nao wataanzisha vikundi vyao vya wanamgambo na wa-islam nao pia

wataanzisha vikundi vyao basi kutakuwa tanzania hakukaliki kila sehemu kuna vikundi vyenye silaha. Hivyo ndivyo alivyo tuachia urithi

wa nchi yetu yenye maziwa makuu baba wa taifa mwalimu nyerere?
jibu hoja iliyo wekwa sio kuanzisha hoja mpya kupitia mwenzako- tumia akili usitumie masbuli
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...

Hofu ya chama cha mapinduzi ilionekana pale.
Mwl,Nyerere katika kikao cha viongozi wa chama cha mapinduzi aliwauliza viongozi kwamba wako tayari kukubali mfumo wa vyama vingi vya siasa kikao hicho walikuwepo marehemu Mfaume Kawawa,Anne abdallah na wengine wengi,jibu lililotoka katika kikao hicho lilikuwa hapana!!!!!!,kwa mshangao mwl, Nyerere akawaambia ninyi leo hamna uhakika kama mkikubali mfumo wa vyama vingi vya siasa mtashinda,watanzania hawawezi kuongozwa na chama chenye ugonjwa(hofu) kama kitaingia katika uchaguzi wa vyama vingi kitashinda,ugonjwa (hofu) hii aliyoiyona mwl,Nyerere katika chama hichi ndiyo inayo kisumbuwa chama hiki inayopelekea chama hiki kuiba kura,matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola kuwatisha wapinzani na wananchi,kuwabambikizia wapinzani kesi za kutisha na mengine mengi.NI KWELI TUKIREJEA KAULI YA MWNAHARAKATI BABA WA TAIFA HATUWEZI KUONGOZWA WATANZANIA NA CHAMA KIGONJWA(HOFU)
 
Mkuu TUKUTUKU Hivi vyama vya kisiasa vya Kibongoo vimeamuwa kuanzisha Vikundi vya wanamgambo wa vyama kulikoni? Utafikiri Tanzania hakuna

jeshi la Polisi au Jeshi la wananchi? Majangaa hayo Majangaaa!!!!!!!!!!!!!!!!! Tanzania kwa miaka inayokuja mbele itakuwa kama Lebanon

kutakuwa na Vikundi vingi vya wanamgambo, Natabiri WaKristo nao Wataanzisha Vikundi vyao vya Wanamgambo na Wa-islam nao pia

Wataanzisha Vikundi vyao basi kutakuwa Tanzania hakukaliki kila sehemu kuna vikundi vyenye silaha. Hivyo ndivyo alivyo tuachia Urithi

wa nchi yetu yenye Maziwa Makuu Baba wa taifa Mwalimu Nyerere?

kwenu analinda polisi? Tumia japo akili kidogo uliyo nayo siyo ufuate mkumbo mkuu.
 
Wakati CCM inaruhusu mfumo wa vyama vingi ilijua kuwa kutakuwa na changamoto kwenye kushika dola. CCM ingekuwa inaogopa upinzani isingeruhusu uwepo.

Kuweza kushika dola miaka zaidi ya 20 tangu upinzani uanzishwe ni mafanikio makubwa. CCM imeweka rekodi ya kudumu madarakani zaidi ya robo karne tangu kuanzisha upinzani!

Kwahiyo wapinzani Tanzania kwa robo karne wameshindwa kuwaconvince wananchi waisahau CCM. Hiyo ndio hali halisi iliyopo hivi sasa.

Masuala ya mwaka 2015 tusubiri 2015, mpira dakika 90 ingawa muda wa nyongeza kwenye fainali upo na ikibidi penati...

kwa miaka yote 20 ingekuwa hamfanyi zengwe kwamba tuaningia katika uchaguzi huru wazi na haki nafikiri ccm ingeshapotea muda mmrefu. ila hila mbaya iliyonayo ccm kuwa mtu akiwa chama cha upinzani husani chenye nguvu basi hapo nongwa za ccm huzuka.
 
Mshindwa hakosi sababu.

Unajua ushindani ndani ya soko la dunia ulivyo?
Unajua ushindani ndani ya baraza kuu la umoja wa mataifa ulivyo?
Unajua ushindani katika jumuiya ya kimataifa?
Unajua ushindani wa makampuni makubwa duniani kupigania rasilimali duniani?

Hucho chama kinacholalamikia "zengwe" za CCM kinategemea kikiingia madarakani kitaongoza huku dunia nzima ikiwaacha bila zengwe?
 
Chama cha mapinduzi hakikuwa na ridha ya kukubali mfumo wa vyama vyingi na kumbuka mwl Nyerere katika kikao cha chama cha mapinduzi aliwauliza viongozi wa chama hichi kwa kuwatega kwamba wao viongozi wa chama cha mapinduzi wako tayari kukubali mfumo wa vyama vingi vya kisiasa nchini?jibu;kutoka kwa viongozi walikuwepo katika kikaa hicho mrehemu Mfaume Kawawa,Anne Abdallah na wengine wengi hapanaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!,mwl, akawaabia mnaona mlivyo waoga hamna uhakika kama tukianzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa mtashinda hatuwezi kuongozwa na chama ambacho kigonjwa hakina uhakika kama kitashida kitapoingia katika chaguzi na vyama vingine vya siasa.Uoga huu ndio unakimaliza chama cha mapinduzi.WATANZANIA HATUWEZI KUONGOZWA NA CHA KIGONJWA.

Story za vijiweni hizi...
 
Zemarcopolo anaishi kwenye utopia akipumua hewa ya Lumumba;eti ccm had an option to reject mfumo wa vyama vingi?hata kama mnalipwa na lumumba, watanzania wa leo wanajua maana na umuhimu wa liberal democracy;halafu hoja yako kwamba Tanzania is second to USA in terms of opportunities available kwa wananchi ni hoja ya kipuuzi;unatumia framework gani kufikia conclusion ya ovyo namna hii...

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom