Kwa nini bandari Tanzania itaendelea kuwa ‘kaa la moto’?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Na Beatrice Kimaro
Mchambuzi, Tanzania
th

CHANZO CHA PICHA,HABARI LEO
Ikiwa na bandari tatu kubwa upande wa bahari ya Hindi na nyingine kadhaa upande wa maziwa, Tanzania imekuwa kiungo muhimu kwa nchi zisizokuwa na bandari katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.
Bandari zake za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zimekuwa mlango muhimu wa bidhaa na biashara kwa nchi za Zambia, Zimbabwe, DRC, Malawi, Burundi, Rwanda na Uganda.

Kwa umuhimu huo wa biashara za kikanda na mchango wake kwa uchumi, serikali na kila kiongozi anayeingia madarakani, amekuwa akitupia sana macho eneo hilo la bandari.

Na haishangazi kuona katika kipindi cha miaka 10 iiyopita, mabosi takriban 6 waliteuliwa na kuondolewa kuongoza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wa sababu mbalimbali, nyingi zikihusishwa na utendaji na zingine ni ubadhirifu na ufisadi. Swali hapa Kwa nini bandari Tanzania imekuwa mwiba kwa watendaji wake?

Historia ya timua timua ya vigogo wa bandari​

TH

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Wiki hii Rais Samia amemuondoa mkurugenzi wa Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA), Eric Hamis ikiwa ni mwaka mmoja na miezi mitatu tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo.

Unaweza kujiuliza kwa nini ni muda mfupi sana, lakini kwa bandari ni jambo la kawaida ‘kuteuliwa asubuhi na kuondolewa jioni’.

Rais ametengua uteuzi wa Hamis ikiwa pia ni zaidi kidogo ya mwaka mmoja, tangu avunje bodi ya wakurugenzi ya mamlaka hiyo Desemba 4, 2021.

Huko nyuma, kulikuwa na Mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo Ephraim Mgawe aliyeondolewa Agosti 2012, kwa sababu ya kushuka kwa mapato ya bandari kutoka shilingi bilioni 36 hadi bilioni 23 mwaka 2011.

Madeni Kipande akakaimu nafasi ya Mgawe kabla ya kusimamishwa kazi na aliyekuwa waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wakati huo, Samuel Sitta, ambaye sasa ni marehemu, kwa tuhuma za rushwa na kupelekwa mahakamani na kesi inaendelea mpaka sasa. Aliondolewa kabisa Aprili 16, 2015.

Baada ya hape Awadh Massawe aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya Ukurugenzi kabla ya kutimuliwa ndani ya miezi mitatu tu kwa tuhuma za upitishwaji wa mizigo kiholela kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Nafasi yake ikachukuliwa na Deusdedit Kakoko ambaye aliondolewa April, 2021 kwa tuhuma mbalimballi zikiwemo ubadhirifu wa fedha. Akaingia Eric Hamis ambaye na yeye ameondolewa kwa sababu za kiutendaji.

Bandari ni dimbwi la asali chungu​

TH

CHANZO CHA PICHA,NMG​

Hakuna shaka bandari imekuwa na mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania. Kwa mujibu wa ripoti ya mapato ya TPA ya mwaka 2021 iliyochapishwa Februrari 2022, TPA ilikusanya shilingi bilioni 508 kati lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.1 kwa mwaka.

Mapato haya yanatokana na shughuli zake za bandari ikiwemo usafirishaji wa shehena za mizigo zinazofikia tani milioni 16, ikilenga kuongeza uwezo wake wa kupokea na kupakia shehena za mizigo hadi kufikia tani milioni 25.

Pamoja na mchango huu wa mapato na uchumi wa taifa hilo, upo wasiwasi kwamba mchango huo unaoonekana ni mabilioni ya shilingi upande mwingine unakosolewa kutokana na hali halisi ya shughuli nyingi za taasisi hiyo. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kiasi kilichokusanywa kwa mwaka 2021 ni chini ya nusu ya lengo la makusanyo.

‘Kwa shughuli za bandari na mapato yake, usipompata mtu muadilifu, mianya ya rushwa ni mikubwa, hivyo ni rahisi kuingia kwenye mtego, anasema Dkt Barnos William, mchumi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi.
Mapato yanayoingia bandarini yanatamanisha kwa watendaji wasio waadilifu. Ni asali na mtego wa panya. Inahitaji mtu mwema kuyaangalia na kusimamia, vinginevyo ni rahisi kuona na kusikia wengi wa watendaji wakinyooshewa vidole kwa tuhuma za rushwa na ubadhirifu wa fedha.

Bandari ya ‘longolongo’ na utendaji wa bakora​

TH

CHANZO CHA PICHA,AFP​

Wadadisi na wachambuzi wengi wa uchumi, wanaitaja bandari za Tanzania kwa mfano ya Dar es Salaam, kuwa moja ya bandari ya kimkakati na kifaida zaidi pengine kuliko bandari nyingi za ukanda Afrika Mashariki.
‘Bandari za Mombasa, Tanga, Mtwara na zingine kama za Djibouti, Sudan na Mauritius, zilivyokaa na miundo mbinu yake, zinaipa nafasi bandari ya Dar es Saaam kufanya vizuri zaidi’, anasema Dkt. William, mhadhiri wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi.

Lakini uendeshaji wake na kasi yake ya ukusanyaji wa mapato unatia shaka jambo ambalo hata Rais Samia Suluhu Hassan ameliweka wazi juma hili.

‘Siridhishwi kabisa na kasi za bandari, siasa zilizoko, longolongo zilizoko, mabandari yanaendeshwa kwa kasi kubwa (duniani), na biashara zinakua kwa kasi kubwa kupitia bandari, sisi bado tunasuasua,’alisema Rais Samia.

Kauli hii inadhihirisha mambo mawili makubwa; mosi ni kwamba kasi ya utendaji ni ndogo isiyokidhi matarajio na kuna longongo nyingi achilia mbali tuhuma za upotevu wa mapato yanayodaiwa kuishia mifukono mwa watu binafsi.

‘Tunasuasua, wawekezaji wanakuja, wanazungushwa mwanzo mwisho, nasema bandarini watu wafanye kazi, kwa hiyo tutatupia jicho vizuri kwenye masuala ya bandari, wale waliokabidhiwa bandari nataka tuelewane vizuri’, anasema Rais Samia. Saa chache baada ya kauli hiyo Mkurugenzi Mkuu Hamis akaondolewa.

Je matarajio ya mamlaka kuhusu bandari yataafikiwa?​

th

Ukisikiliza kauli za viongozi wa nchi tangu wakati wa Rais wa kwanza wa taifa hilo, Julius Nyerere mpaka rais wa sita, Samia, inakuonesha walivyo na matarajio makubwa juu ya bandari.

Rais Benjamin Mkapa wakati wa uhai wake, aliwahi kusema hataki mchezo na bandari, Rais John Magufuli alivyoingia madarakani tu 2015, maeneo ya kwanza kwanza kuyatembelea ilikuwa bandari ya Dar es Salaam.
‘Matarajio makubwa ya viongozi hasa kwa bandari ya Dar es Salaam ndiyo yanayowaondoa wakurugenzi na bodi ya mamlaka ya bandari, wakimteua mtu wanaamini atawavusha, lakini mwishowe wanaishia kutimuliwa na wengine kufikishwa mahakamani, anasema Dkt. William.

‘Bandari ya Dar es Salaam ndiyo jicho letu, bandari hii iifana kazi vizuri, nusu ya bajeti tunayoipanga kila mwaka itatolewa ndani ya bandari ya Dar es Salaam,’ lakini kama tutajipanga kufanya kazi vizuri, Kama bado tunakwenda na longolongo, hilo lengo hatutalifikia, anasema Rais Samia.

Bajeti ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa fedha 2022/2023 ni shilingi tiriioni 41, kwa kauli ya Rais Samia maana yake anaitazama bandari moja tu ya Dar es Salaam kuwa inaweza kuchangia mpaka tirilioni 20 kwa mwaka, ikiwa kutakuwa na usimamizi madhubuti na kuondolewa kwa longolongo.

Ni rahisi kujiuliza, matarajio ya namna hii yatafikiwa? kama watendaji wanaoendelea kuteuliwa hawatakuwa na namna ya kuifanya bandari hii na nyinginezo kutengeneza kiasi hicho cha mapato ama kuelekea kwenye kiwango hicho maana yake ni kwamba huenda tukaendelea kushuhudia mabadiliko ya kila uchwao kwenye mamlaka ya bandari.

Na mtihani huo ameushika Pasduce Mbossa anayekaimu nafasi ya kurugenzi mtendaji wa TPA, je ataweza na kuvuka kiunzi cha muendelezo wa watendaji wa mamlaka hiyo kuondolewa? chanzo. BBC
 
Na Beatrice Kimaro
Mchambuzi, Tanzania
th

CHANZO CHA PICHA,HABARI LEO
Ikiwa na bandari tatu kubwa upande wa bahari ya Hindi na nyingine kadhaa upande wa maziwa, Tanzania imekuwa kiungo muhimu kwa nchi zisizokuwa na bandari katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.
Bandari zake za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zimekuwa mlango muhimu wa bidhaa na biashara kwa nchi za Zambia, Zimbabwe, DRC, Malawi, Burundi, Rwanda na Uganda.
Kwa umuhimu huo wa biashara za kikanda na mchango wake kwa uchumi, serikali na kila kiongozi anayeingia madarakani, amekuwa akitupia sana macho eneo hilo la bandari.
Na haishangazi kuona katika kipindi cha miaka 10 iiyopita, mabosi takriban 6 waliteuliwa na kuondolewa kuongoza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wa sababu mbalimbali, nyingi zikihusishwa na utendaji na zingine ni ubadhirifu na ufisadi. Swali hapa Kwa nini bandari Tanzania imekuwa mwiba kwa watendaji wake?

Historia ya timua timua ya vigogo wa bandari​

TH

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Wiki hii Rais Samia amemuondoa mkurugenzi wa Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA), Eric Hamis ikiwa ni mwaka mmoja na miezi mitatu tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo.
Unaweza kujiuliza kwa nini ni muda mfupi sana, lakini kwa bandari ni jambo la kawaida ‘kuteuliwa asubuhi na kuondolewa jioni’.
Rais ametengua uteuzi wa Hamis ikiwa pia ni zaidi kidogo ya mwaka mmoja, tangu avunje bodi ya wakurugenzi ya mamlaka hiyo Desemba 4, 2021.
Huko nyuma, kulikuwa na Mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo Ephraim Mgawe aliyeondolewa Agosti 2012, kwa sababu ya kushuka kwa mapato ya bandari kutoka shilingi bilioni 36 hadi bilioni 23 mwaka 2011.
Madeni Kipande akakaimu nafasi ya Mgawe kabla ya kusimamishwa kazi na aliyekuwa waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wakati huo, Samuel Sitta, ambaye sasa ni marehemu, kwa tuhuma za rushwa na kupelekwa mahakamani na kesi inaendelea mpaka sasa. Aliondolewa kabisa Aprili 16, 2015.
Baada ya hape Awadh Massawe aliteuliwa kushika nafasi hiyo ya Ukurugenzi kabla ya kutimuliwa ndani ya miezi mitatu tu kwa tuhuma za upitishwaji wa mizigo kiholela kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Nafasi yake ikachukuliwa na Deusdedit Kakoko ambaye aliondolewa April, 2021 kwa tuhuma mbalimballi zikiwemo ubadhirifu wa fedha. Akaingia Eric Hamis ambaye na yeye ameondolewa kwa sababu za kiutendaji. chanzo. BBC
Hapo aletwe Ramadhan Dau ndiyo mwisho wa matatizo.
 
Tatizo sio Mkurugenzi wa mamlaka ya Bandari bali tatizo lipo kwa watendaji na wafanyakazi wa muda mrefu waliopo hapo Bandarini.
hao wafanyakazi wa muda mrefu ndio chanzo kikuu cha matatizo ya bandari, wapo wakongwe hapo ambao ni unttachable, miungu watu na wapiga fitina wakongwe, hao ndio wanapaswa waondolewa
 
Tena la moto sana

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Na Beatrice Kimaro
Mchambuzi, Tanzania
... haishangazi kuona katika kipindi cha miaka 10 iiyopita, mabosi takriban 6 waliteuliwa na kuondolewa kuongoza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wa sababu mbalimbali, nyingi zikihusishwa na utendaji na zingine ni
...
‘Kwa shughuli za bandari na mapato yake, usipompata mtu muadilifu, mianya ya rushwa ni mikubwa, hivyo ni rahisi kuingia kwenye mtego, anasema Dkt Barnos William, mchumi kutoka chuo kikuu cha Ushirika Moshi....
Tatizo la ubovu wa uendeshaji wa Mashirika na Taasisi za umma siyo la bandari tu. Ni ugonjwa tulionao tangu Baba wa Taifa alipotaifisha makampuni na mashirika binafsi na wateule wakayaongoza kama mali binafsi.

Ugonjwa huo umechochewa ubovu wa uendeshaji na sheria za kazi na ajira, ambazo zilitokana na Azimio la Arusha (kuhusu "miiko" na "masharti" ya uongozi), kwamba mwajiriwa anakuwa hagusiki (Azimio la Arusha limevunja nguzo kuu za maadili). Isitisho vyombo vya usimamizi pia vimeghubikwa na urasmu na umangimeza. Bila kusahau matumizi mabaya ya madaraka.

Kinachohitajika ni kuweka mfumo thabiti wa usimamizi na uwajibikaji na siyo kutafuta kampuni ya nje kuendesha Mashirika na Taasisi za Umma.
 
Back
Top Bottom