ulichokisema ni cha kweli. naona sheria za tanzania zimetungwa kwa ajili ya raia wasio na hadhi yoyote. waliopewa kusimamia sheria, polisi, ndio vinara wa kuvunja sheria. trafic anendesha pkpk hana helmet, gari havai mkanda. shuhudia lori, au pickup zinazobeba mahabusu zinavyo jaa. shuhudia polisi wanavyopiga watu makofi, mpaka upo msemo 'unauliza makofi polisi?' nahisi hata ushirikiano hafifu kati ya walinda sheria na wananchi unaletwa na kuona sheria c kwa wote.