Kwa nini askari wa Tanzania wanaona sifa kuvunja sheria?

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,259
2,124
Mara nyingi huwa naona kama kuna traffic jam magari ya askari polisi, magereza na JWTZ (na hata yanye namba zinazoanza na a ST, SU) wakitanua lakini magari ya raia yakitanua yanakamatwa. Jana jioni kama saa 2 usiku hivi karibu tugongane na gari la JWTZ kati ya Matumbi na Tabata maana baada ya kuona foleni upande wao (kutoea Buguruni kuelekea Ubungo) haiendi wakaamua kupita sehemu yetu (sisi tulikuwa tukielekea Buguruni kutokea maeneo ya Tabata) na kama kawaida yao huwa hawampishi mtu. Leo asubuhi pia niliona kitu cha aina ileile? Hivi mara zote huwa kuna emergency ya kuwafanya wafanye hivyo au huwa ni kwa vile wanajiona wako juu ya sheria? Nchi nyingine hata hapa Afrika askari wako mstari wa mbele kufuata sheria lakini hapa kwetu naona wako nyuma sana. Je, ndivyo wanavyofundishwa au wanatumia mwanya huu ambao "anything goes"?
 

katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
52
Magari ya ST, SU na haya ni ya askari? Na wewe tanua ukiona hivyo, hutakamatwa na utawahi kufika nyumbani. Siku nyingine na wewe fanya hivyo!
 

Dengue

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,815
1,037
Na wewe tanua. Ukisimamishwa waambie wakawasimamishe na wale pia.
 

kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,402
3,149
ulichokisema ni cha kweli. naona sheria za tanzania zimetungwa kwa ajili ya raia wasio na hadhi yoyote. waliopewa kusimamia sheria, polisi, ndio vinara wa kuvunja sheria. trafic anendesha pkpk hana helmet, gari havai mkanda. shuhudia lori, au pickup zinazobeba mahabusu zinavyo jaa. shuhudia polisi wanavyopiga watu makofi, mpaka upo msemo 'unauliza makofi polisi?' nahisi hata ushirikiano hafifu kati ya walinda sheria na wananchi unaletwa na kuona sheria c kwa wote.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom