Kwa ninavyokujua wewe,,,,,!!!

Kwa ninavyokujua wewe,,,,,!!!

Kisoda2

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Posts
2,475
Reaction score
747
Siku moja umerudi na mning'ining'io(hanover) wako ongeza na usingizi mkali wa kukesha yapata kama saa tisa unusu ama kumi ndo umeingia kulala.
Yapata majira ya saa moja asubuhi mtu anakugongea mlango kwa nguvu(fujo/kero).

Unaamka ili kwenda fungua upate kujua nani huyo, unajikwaa kidole cha mwisho cha mguu kwenye mfumbati wa kitanda, kisha kwa mawenge ya kilichotokea tena unagonga ndoo ya maji nayo inamwagika.

Unafungua mlango unakutana na jamaa anakwambia nauza VOCHA za simu tena kakukenulia meno eti pozi la biashara!!
Utafanya nini? Kwa ninavyokujua wewe!!:whistle::whistle::whistle:​
 
Nimecheka hadi najishangaa. Anyway nitamwangalia tu. Simwambii nae chochote.
 
Nitamhurumia tu... kisha narudi kulala.. mengine baadaye
 
wee jamaa umenikumbusha mbali sana hiyo kujikwaa kwenye kitanda huwa inaumaga balaa unaweza kosa raha kama siku 2 hivi damu haitoki lakini daa
 
Nampa dekio afute maji niliyomwaga afu namkopa vocha kulipa hadi 2016 mwanzoni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom