TheMnyonge
JF-Expert Member
- Mar 25, 2022
- 739
- 1,871
Ndugu zangu, naandika nikiwa very down yaani, na kila nikifikiria nashindwa kujua what kind of friends do I have?
Nimekuwa na marafiki kadhaa ambao kwa mtazamo wangu nimekuwa nikidhani tunafaana, ila kumbe mimi ndo nawafaa wao tu.
Kumekuwa na hizi mambo ambazo baada ya kufikiria kwa kina naona hakuna haja ya kuwa na marafiki kabisa.
Kila wakiazima pesa jamaa zangu hawa HAWARUDISHI, wengine wanaazima then wanaanza kurudisha kidogo kidogo, naanza na hizi tatu za karibuni...
1. Jamaa alipatwa na bonge la dharura akiwa nje ya jiji, akaniomba nimuwekee 400,000/= akirudi anakuja ku-clear, (Mimi nafanya biashara ya miamala ya kifedha) nikamtumia jamaa a solve tatizo lake, siku mbili baadaye jamaa alirudi ila hakuwa anazungumzia chochote kuhusu pesa yangu, Mara wiki ikakata, nikamkumbusha kuwa ile ni pesa ya biashara na ipo kwenye mzunguko akasema "soon ntakurekebishia" ila kimya...(huyu ni mtu nimesoma naye, anafanya kazi na pesa najua anayo ila dhamira ya kurudisha hana!)
2. Hii imetokea mwezi mmoja uliopita, jamaa tupo naye kazini na ni rafiki yangu wa karibu kabisa, ghafla ulitokea msiba wa baba yake huko mkoani, Bahati mbaya hakuwa vizuri, kwa kuwa anajua kaofisi ka miamala hakapo vibaya sana akanifuata na kuomba nimpe 350,000/= then soon angenirejeshea, nikamsisitiza sana kwamba pesa ni ya biashara, aka-declear kwamba ile pesa ya mkono wa pole kutoka ofisini (ambayo ni 500,000) nitachuku 350,000 then inayobaki ndo atumiwe (maana hii pesa huwa inatolewa immediately inapotokea dharura ya aina yake)
Cha ajabu nilipokwenda kwa muhasibu kumwambia anipe hiyo 350,000 nikaambiwa jamaa aliitaka yote na wameshamtumia tayari, nikanyamaza, jamaa alirudi job, lakini pesa yangu haizungumzii kabisa, nikamkumbusha akaniambia atanipa mwisho wa mwezi, imefika mwisho wa mwezi akanipa 100,000/= kirahisi kabisa akaniambia nyingine mwezi ujao, nilishikwa hasira sana nikaondoka.
Jamaa wa tatu aliipata janga la kuunguliwa na vitu, katika kutafuta namna ya kusimama upya akaniomba 450,000/= katika hiyo alirudisha 250,000/= nyingine mpaka leo kimyaaa, sasa najiuliza aina huu ya urafiki wa kurudishana nyuma kuna ulazima wa kuendelea nao kweli?
Naombeni mbinu za kuishi bila interaction na marafiki, maana inafika mahali naona kama wanafanya makusudi kunikwamisha tu, na kwanini marafiki ndo wanakuwa wa kwanza kutuangusha?
Najiuliza kwani hawa jamaa wananionaje?